Producer maarufu Bongo, Mazuu Record amesema kuwa msanii Rich Mavoko alilazimishwa kujiunga na Lebo ya Wasafi (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platnumz.
"Kipindi hicho Rich Mavoko ana-hit song kubwa kuliko Diamond, WCB walimpa machaguo mawili Rich Mavoko, kama anataka kuendelea na muziki aende WCB kama hataki abaki huko huko, mimi ikabidi nikate tamaa kwa sababu vita ya WCB ilikuwa kubwa na Rich Mavoko alikuwa amekataa kabisa kujiunga WCB ikabidi nimuombe.
"Siyo kwamba Rich Mavoko ndiyo alitaka kwenda WCB ni wao ndiyo walitaka yeye aende kwao, kwa sababu alikuwa ni mtoto msumbufu kuliko Kiba, Rich Mavoko ni msanii pekee ambaye anaweza kuimba kwenye namna yoyote unayoitaka wewe.
"Baada ya wimbo wa 'Roho yangu' kuzuiwa tuliamua kuja na wimbo mwingine ambao wadau walijitokeza wakatoa Milioni 40 kwa ajili ya kufanya wimbo pamoja na promotion ya wimbo wa ‘Pacha wangu’.
"Katika ngoma ambayo ilitusumbua sisi ni roho yangu, iliwekewea hadi vikao na hela ili isipigwe redio zote, Mimi na meneja wa Mavoko tulikaa tukaumiza kichwa ikafika mahala tukasema ngoja tutoe ngoma nyingine ya pili," amesema Producer Mazuu Record.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA