Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewajibu baadhi ya mashabiki wa Klabu wa Simba wanaosema kwamba Yanga wamekwenda kufanya ushirikina kwenye uwanja wa KMC Complex baada kupeleka mechi yao pale dhidi ya Kiluvya FC.
Iko wazi, Uwanja wa KMC ni uwanja wa nyumbani wa Simba SC na Yanga akacheza mechi yao pale jana na kuibuka na ushindi wa bao 3-0.
“Jana tumecheza mechi yetu ya mazoezi pale KMC na tumesikia milio Mingi ikivuma, tuwaambie ule ni uwanja wa Halmashauri ya Kinondoni ni fedha zetu wanakinondoni tumejenga ule uwanja, KMC tumempa tu ausimamie.
“Sasa wewe uwanja sio wako unaongea ongea tunefata nini, wewe ni kwako? Na ule uwanja unapataje heshima kama Yanga haendi pale, watu wa mwenge jana wamefurahi sana kutuona sasa kama imewauma hameni na tutakuja tena.
“Ule ni uwanja wa halmashauri ya Kinondoni, ni kodi zetu zile, we unaumia kwako pale? Sisi tunacheza popote hata Bunju tukitaka tutacheza,” amesema Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA