Kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa Uganda, Khalid Aucho amewaambia mashabiki wa klabu yake kupitia mtandao wake wa Instagram kuwa ataendelea kusalia klabuni mpaka pale rais wa klabu hiyo, Eng. Hersi Said atakapoamua kusema inatosha.
Khalid Aucho ni moja kati ya mchezaji muhimu kwenye kikosi cha wananchi, kwa kutambua hilo mashabiki wamekuwa wakihitaji kiungo huyo aendelee kusalia mitaa ya twiga na jangwani ambako ndio maskani ya mabingwa hao wa kihistoria.
Aucho anasema ataendelea kusalia Yanga sc kwasababu anaipenda klabu lakini pia anawapenda mashabiki wa klabu hiyo, hivyo ataendelea kuipambania timu mpaka pale Rais wa klabu hiyo atakapoona inatosha tena kupata huduma ya kiungo huyo.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA