Esma Platnumz, dada wa Diamond Platnumz, ameeleza machungu yake kupitia Instagram baada ya kugundua kuwa ameibiwa na watu waliodai kuwa ni wawakilishi wa kampuni ya simu. Esma platnumz alikumbwa na tukio hilo alipoamua kuwasaidia watu watatu waliovaa mavazi rasmi na kuonekana kama wawakilishi wa mtandao wa simu. Walipokuwa dukani kwake, alikubali kuwapa vitambulisho vyake kwa kuwa alikuwa na shida na laini yake.
Hata hivyo, baada ya wao kuondoka, aligundua kuwa walikuwa wamepata namba yake ya siri na kutumia app ya simu kuingia kwenye akaunti yake ya M-Pesa, ambapo walijitumia pesa na kuchukua mikopo isiyo ya halali. Esma ameeleza kuwa amevunjika moyo na kuomba jamii iwe makini na watu wanaojifanya wawakilishi wa simu, huku akitaka kampuni ya Vodacom kuchukua hatua dhidi ya wizi huo.
0 Comments