Wakati mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize akiendelea kuhusishwa na klabu ya Wydad, mashabiki wa timu hiyo wamevamia kwenye ukurasa wake wa Instagram wakimkaribisha kwenye timu yao.
Baada ya Mzize kufunga bao kali la pili jana kwenye mechi ya kwanza ya ligi, Yanga ikishida kwa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar akaweka chapisho akiandika maneno "Kesho ni fumbo usimdharau mtu kwa uwezo ulionao au udhaifu alionao."
Baada ya hilo baadhi ya mashabiki wanaodhaniwa wa Wydad, wamechangia kwa kutuma ujumbe chini ya chapisho hilo.
Mashabiki hao wamekuwa wakimpongeza Mzize huku wengine wakimkaribisha Wydad inayotajwa kumuwania mshambuliaji huyo.
Wakati mashabiki hao wakituma ujumbe huo, Meneja wa Habari wa Yanga, Ally Kamwe naye akawa mmoja wa waliotuma ujumbe akiandika mshambuliaji huyo hauzwi.
Kauli hiyo ya Kamwe haikuwazuia mashabiki hao kuendelea kumkaribisha Mzize kwenye klabu yao ambayo inapambana kusuka kikosi kipya kitakachoirudishia ufalme wa mataji baada ya kuyumba kwa misimu miwili
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA