MCHEZAJI MARTINEZ AFUNGIWA NA FIFA KISA USHANGILIAJI WA KUSHIKA SEHEMU ZA SIRI
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez, amesimamishwa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA kwa "tabia ya udhalilishaji" na atakosa mechi mbili zijazo za Argentina.
Adhabu hiyo imetokana na matukio mawili katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Chile na Colombia. Martinez alirudia aina yake ya ushangiliaji wa kushika sehemu za siri ambapo alionywa namna hiyo ya ushangliaji tangu fainali ya kombe la Dunia mwaka 2022.
Kwa upande wa Shirikisho la Soka Argentina AFA, imeonyesha kutokubaliana na adhabu hiyo kwa mlinda mlango wao namba 1, Hivyo basi kipa huyo mshindi wa tuzo ya kipa bora kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, atakosa mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia kati ya Argentina dhidi ya Venezuela na Bolivia mwezi Oktoba,2024
0 Comments