Mlela atoa Siri kwa nini Achague Sehemu ya Kuzikiwa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Mlela atoa Siri kwa nini Achague Sehemu ya Kuzikiwa

Licha ya kuwa katika jamii inaonekana kama jambo la kutisha, kushangaza na kuogopesha akisikika mtu akizungumzia mazingira ya kuhifadhiwa kwake baada ya kufariki lakini kwa mwigizaji Yufuph Mlela mapema ametoa maagizo ya kuzikwa makaburi ya Kinondoni na siyo mwili wake kusafirishwa.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Septemba 1, 2024 ameandika, "Ikitokea nimefariki(nimekufa) mwili wangu utazikwa makaburi ya Kinondoni Ufipa(home) sisafirishwi popote,"


Mbali na kuandika ujumbe huo Mlela ameiambia Mwananchi kuwa sababu kubwa ya kuandika ujumbe huo ni kutotaka maiti yake igombaniwe.


"Hisia zimenituma nitoe ujumbe huo na ninamaanisha kweli, huwezi kujua siku nitayofariki duniani nimeandika ili hata siku nimefariki ndugu zangu wakataka kugombania sehemu ya kuzikwa nakuwa nimeamua wapi nizikwa ili nitoe utata.Maiti inatakiwa kuzikwa na siyo kusumbuliwa nataka kuzikwa sehemu ambayo nimezaliwa, nimekua na maisha yangu ninapoyaendesha,"amesema.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad