Taarifa za Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, beki wa kulia Israel Mwenda, ambaye tulieleza kwamba amepanga kufikisha malalamiko yake FIFA.
Sasa kuna habari mpya kumhusu mchezji huyo aliyesajiliwa na Singida Black Stars, awali alikuwa ameongezewa mkataba na Simba lakini aliomba kutafuta changamoto mpya, na ndipo Simba wakamruhusu akaondoka, huku nafasi yake akizida Kelvin Kijili aliyetokea Singida Big Stars pia.
Israel Mwenda amesema kwamba timu yake ya sasa, imevunja makubaliano ya kimkata na yeye hana pa kwenda kwa sasa, kwani dirisha la usajili limekwisha fungwa.
“Nipo kwenye mchakato wa kuvunja mkataba, nyie subirini mtapata taarifa, Singida wapo nje ya makubaliano tuliyokubaliana. Mpira wetu una changamoto sana. Halafu baadae utasikia wazawa wana matatizo”
“Nitaenda wapi sababu dirisha limefungwa? Hela niliyonayo inanitosha kuishi hata misimu minne bila kucheza mpira, kiufupi ni kwamba sina timu” Israel Mwenda.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA