Mwijaku Apewa Siku 21 Kujitetea Dhidi ya Keshi Aliyofunguliwa na Kipanya

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Mwijaku Apewa Siku 21 Kujitetea Dhidi ya Keshi Aliyofunguliwa na Kipanya

Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam David Ngunyale ameahirisha kesi ya @masoudkipanya Kipanya dhidi ya Burton Mwemba, maarufu kama @mwijaku , hadi tarehe 24 Septemba 2024.


Wakili wa Mwijaku, Patrick Malewo aliomba muda wa ziada wa siku 21 kuwasilisha utetezi wa kimaandishi, kwa sababu muda uliotolewa awali ulikuwa umeisha ambapo Wakili wa Kipanya, Alloyce Komba hakupinga ombi hilo.


Mahakama imeridhia na kumpa Mwijaku muda huo wa nyongeza. Kesi itatajwa tena kwa ajili ya kupanga utaratibu wa usikilizaji.


Kipanya amefungua kesi hiyo ya madai namba 18911 ya mwaka 2024, Agosti 5, 2024 akiomba nafuu 12 ikiwamo kulipwa fidia kwa kukashifiwa mtandaoni na Mwijaku.


_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad