Shamsa Ford: Vijana Tafuteni PESA Muache Kudhalilika

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Shamsa Ford: Vijana Tafuteni PESA Muache Kudhalilika


Msanii maarufu wa Bongo Movies, Shamsa Foed amewashauri vijana kufanya kazi na kutafuta pesa ili waheshimike kwa wanawake badala ya kudhalaulika.


Shamsa amesema hayo baada ya Shilole kumtimua mumewe, Romy 3D huku akidai kuwa hakuwa na msaada wowote kwake zaidi ya kula na kulala tu ndani.


"Najua nikiongea haya Shilole atanichukia ila acha niseme kwamba alichomfanyia Rommy sio kitu cha kiungwana, kumwambia mwanaume wako kuwa alikuwa analala tu ili ufurahishe watu mtandaoni wakati unajua kabisa amekufanyia mengi mazuri ni kumvunjia heshima mume wako hata kama mmeachana.


"Naumia sana nikiona wazazi tunawasomesha watoto wetu wa kiume ili waje watupe heshima wawe na kazi zao alafu unakuja kuona mtoto wako anadhalilishwa kuwa ni king'asti, chuma ulete inaumiza sana. Vijana fanyeni kazi jamani kuepukana na aibu ndogondogo ambazo zinaepukika," amesema Shamsa Ford.


Comments:

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad