Header Ads Widget


Simba Wajipange, Al Ahli Tripoli si TIMU ya Mchezo, ni watu na nusu

 

Simba Wajipange, Al Ahli Tripoli si TIMU ya Mchezo, ni watu na nusu



Simba wanaelekea Libya  kwenye mchezo wao wa kwanza CAFCC msimu huu, wanaenda kukutana na timu yenye ugumu hasa wakiwa kwenye ardhi yao ya nyumbani.


Al Ahly Tripoli kwenye uwanja wao wa nyumbani (Tripoli International Stadium) wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000 tangia February 2023 hawajawahi kupoteza mchezo wowote.


Kwenye kikosi cha Al Ahly Tripoli kuna mchezaji ametokea Esperance de Tunis msimu mwaka juzi Chaalali, huyu mwamba kwenye Transfer Market anavalue ya €900k (Tsh bilioni 2.705) anacheza eneo la Central Midfielder then wana Hamdou El Houni ni left winger ameshawahi kupita timu ya vijana ya Benfica ya Ureno lakini ametokea Wydad Casablanca ya pale Morocco ???????? value yake ni €900k.


Hii miamba ya pale Libya , Al Ahly Tripoli wanammiliki mchezaji mwenye Value ya €1.35 sawa na Tsh bilioni 4.057, mwamba amecheza Petro de Luanda Atletico ya Angola ???????? kabla ya kuelekea De Agosto na baadae Ä°ttihad Alex ya Misri: Agostinho Cristóvão Paciẽncia A.K.A Mabululu.


Ni mchezo wa kwenda na tahadhari kubwa, hawa Al Ahly Tripoli wapo vizuri sana wanatakiwa kuingia kwa discipline.


Post a Comment

0 Comments