Simba, Yanga kupigwa Benjamin Mkapa Oktoba 19

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Simba, Yanga kupigwa Benjamin Mkapa Oktoba 19

Mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu baina ya Simba na Yanga iliyopangwa kuchezwa Oktoba 19 katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam sasa itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku hiyohiyo kuanzia saa 11:00 jioni.


Mabadiliko hayo yametangazwa leo na bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB).


“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ya Ligi Kuu ya NBC ambapo imeipangia tarehe michezo 14 ambayo haikuwa na tarehe katika ratiba ya awali na kufanya mabadiliko ya tarehe katika michezo minne (4).


“Aidha Bodi imefanya mabadiliko ya muda wa michezo miwili huku mchezo mmoja ukibadilishiwa kiwanja kama ilivyoainishwa katika jedwali hapa chini, sababu ya mabadiliko hayo ikiwa ni kuondolewa kwa klabu za Azam na Coastal Union kwenye michuano ya CAF ngazi ya klabu.


“Ratiba kamili ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (www.ligikuu.co.tz),” ilifafanua taarifa hiyo ya TPLB.


Mabadiliko hayo ya ratiba yamezigusa zaidi Azam na Coastal Union ambazo mechi zao zilikuwa hazijapangiwa tarehe hapo awali ili kuendana na kalenda ya mashindano ya klabu Afrika sasa zimepangiwa.


Kwa Azam FC, mechi hizo ni dhidi ya KMC ambayo sasa itachezwa Septemba 19 na dhidi ya Pamba Jiji, Septemba 13 huku nyingine ikiwa ni dhidi ya Coastal Union, Septemba 22.


Kuna mechi ya Azam dhidi ya KenGold, Oktoba 29 na dhidi ya Singida Black Stars, Novemba 3.


Mechi za Coastal Union ni dhidi ya Mashujaa (Septemba 13), dhidi ya Namungo (Septemba 17), dhidi ya Kagera Sugar (Oktoba 28) na dhidi ya Singida Black Stars (Novemba 7).


Mchezo baina ya Simba na Yanga Oktoba 19 ni wa pili kwa timu hizo kukutana ndani ya muda usiozidi miezi mitatu baada ya miamba hiyo ya soka nchini kukutana Agosti 8 katika mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii ambayo Yanga ilishinda kwa bao 1-0.


Mechi ya mwisho kukutanisha timu hizo kwenye Ligi Kuu ilikuwa ni Aprili 20 mwaka huu ambayo Simba ilipoteza kwa mabao 2-1.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad