Uongozi wa Singida Black Stars umemtumia barua Israel Mwenda na uongozi wake wote pamoja na nakala kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
Barua inamtaka aripoti kambini haraka ndani ya masaa 24 baada ya kupokea barua ya wito au ailipe Black Stars shillingi milioni 500 ambayo ni gharama ya kuvunja mkataba.
Awali mchezaji huyo aliyesajiliwa na timu hiyo kutokea klabu ya Simba, alinukuliwa akisema kwamba, waajiri wake wa sasa wamevunja makubaliano ya kimkataba kwa kutomlipa pesa zake za usajili, kama walivyokubaliana.
Hivyo kama wataendelea kukaa kimya, yeye atapeleka malalamiko yake FIFA, kuwashinikiza wamlipe pesa yake ya usajili iliyobaki.
Kwa jinsi hali inavyoonekana huenda suala hili likafika TFF kwenye ile kamati ya usuluhishi wa haki za wachezaji, kama lisipotatuliwa mapema.Sin
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA