Header Ads Widget


TATIZO NI BALEKE AU YANGA PEKEE

 

TATIZO NI BALEKE AU YANGA PEKEE

Inawezekana Jean Baleke amejiunga na Yanga, lakini siyo pendekezo la kocha Gamondi. Kama angekuwa kocha mwenye uwezo, basi angejua wapi na jinsi ya kumtumia Baleke ipasavyo.

Kwa mtindo wa mchezo wa Yanga, sidhani kama Baleke anashindwa kuf fit katika mfumo huu. Akiwa na Simba, Baleke amefunga magoli mengi ndani ya box (6), akionyesha uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kufunga.

Tukichambua washambuliaji wa Yanga, inabainika kwamba wengi wao wamefunga magoli ndani ya 18, na hii inaashiria kwamba mpira unawafikia wakiwa katika nafasi nzuri ya kufunga.

Hiki ni kitu ambacho Baleke anaweza kufanya vyema, kwa sababu yeye ni mshambuliaji anayejiwekea mazingira mazuri ya kufunga magoli.

Baleke anapenda kukaa ndani ya 18 na si nje, hivyo ni muhimu timu itengeneze nafasi nyingi kwenye eneo hilo ili apate fursa ya kufunga. Tangu alipojiunga na soka la Tanzania, tayari ana magoli 7 aliyofunga ndani ya box.

Post a Comment

0 Comments