Rais wa Kenya, William Ruto ametangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Sudan, Salva Kiir Mayardit ambaye amemaliza muda wake.
Uamuzi huo umetangazwa katika Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jijini Arusha leo November 30,2024.
Itakumbukwa Salva Kiir alitangazwa kushika nafasi hiyo November 24,2023 kwenye Mkutano kama huo ambao pia uliridhia Nchi ya Somalia kujiunga EAC na kuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya.