Wamiliki wa Jengo la Ghorofa Lililoanguka Kariakoo Wafikishwa Mahakamani...


Wamiliki wa Jengo la Ghorofa Lililoanguka Kariakoo Wafikishwa Mahakamani...




Wamiliki wa jengo la ghorofa Kariakoo ambalo liliporomoka na kusababisha vifo vya Watu 29, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo November 29,2024 wakikabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia.

Waliofikishwa Mahakamani ni Leondela Mdete (49), Mkazi wa Mbezi Beach, Zainab Islam (61), Mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38), Mkazi wa llala ambapo wamesomewa mashtaka na Mawakili watatu waandamizi wa Serikali - Adolf Lema, Grace Mwanga na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini.

Kwa pamoja watatu hao wanadaiwa kuwa ni Wamiliki wa jengo lililoanguka Mtaa wa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusabanisha vifo vya Watu 29.

Inadaiwa Washtakiwa hao November 16, 2024 katika Mtaa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam, isivyo halali, kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu na kusabashisha vifo vya Watu 29.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad