Mfahamu Muuaji Aliyetokea Kupendwa na Watu Wengi Marekani.....


Dunia na maajabu yake kutana na jamaa mmoja anaitwa Luigi Mangione muuaji aliyetokea kupendwa na wamarekani wengi haswa watu wenye hali ya chini baada ya kufanya tukio la kushangaza lillowaacha mdomo wazi mabosi mbalimbali wa makampuni.

Luigi Mangione anashikiliwa kwa kosa la kumuua mkurugenzi mtendaji wa shirika la afya nchini marekani brian thompson. Mauaji yametokea baada ya luigi kupata tabu ya kupatiwa huduma na Kampuni za bima ya afya haswa kipindi akiwa mgonjwa.

Makampuni mengi ya huduma ya afya unapojiunga huwa wanakata asilimia kadhaa ya pato lako ambapo unatumia kuhifadhi Ikitokea umepatwa na changamoto ukashindwa kutibiwa basi utaweza kutumia bima yako ili kuweza kupatiwa matibabu. Lakini kwa luigi haikuwa hivyo anasema alikua anakatwa pesa lakini inapofika wakati wa kutibiwa akiomba pesa kwa ajili ya Matibabu kupitia bima yake ya afya ilikua wanamzingua na kutokumsaidia.

Luigi alikua anasumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo kwa muda mrefu toka mtoto lakini alipokua anahitaji kufanyiwa matibabu yaliyogharimu pesa nyingi akaomba msaada toka Kampuni ya bima aliyojisajili wakamzungusha tu bila kumsaidia chochote akaamua kufanyiwa upasuaji ambao baada ya muda akakaa sawa lakini halikua anadaiwa pesa atazipata wapi kulipa ?

Akaenda kwenye ile ile kampuni ya bima kuomba pesa za Matibabu akalipe baada ya kufanyiwa upasuaji akakataliwa akachukua jukumu la kuamua kumuondoa uhai mkurugenzi mtendaji wa shirika la bima ya afya marekani. Akatengeneza silaha kwa mfumo wa 3D kisha akanunua risasi tatu na kuzipa majina ya Deny , Defend na Depose akiwa na maana ya kataa, tetea na ondoa.

Luigi Mangione amepelekwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ugaidi la kumuua bosi wa kampuni wa mashirika yote ya bima ya afya marekani lakini amekataa hivyo kesi yake itasikilizwa tena mwakani 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad