Polisi Wafunguka Bwana Harusi Aliyetekwa Kigamboni, Tutachunguza Kama Kajipoteza au la


Polisi Wafunguka Bwana Harusi Aliyetekwa Kigamboni, Tutachunguza Kama Kajipoteza au la


Polisi wanaendelea na uchunguzi kufahamu kama Mtu aitwae Vincent Peter Massawe wa DSM amejipoteza mwenyewe kwa makusudi ama la, ikiwa ni siku kadhaa toka Ndugu zake watangaze kupotea kwake.


Taarifa ya Polisi imesema Jeshi hilo lilipokea taarifa za kupotea kwa Vincent siku chache baada ya harusi yake ambapo imebainika amekuwa akidaiwa zaidi ya Tsh. milioni 65 na Watu tofauti, hivyo wanachunguza kama amepotea kweli au amejipoteza sababu ya madeni.


“Kufuatia taarifa hii inayosambazwa katika Mitandao ya Kijamil, Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kulingana na ushahidi uliokusanywa kupitia kwa Watu mbalimbali na kupitia uchunguzi wa kisayansi uliokwisha fanyika hadi sasa, ni kweli taarifa za kupotea kwa Vincent Peter Massawe zilifikishwa Kituo cha Polisi Kigamboni Noveember 19,2024 na Mke wake” - Polisi.


“Upelelezi ulianza mara moja na kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa na harusi November 16,2024 na baada ya harusi alitafuta gari ya kuwarejesha Ndugu zake na Wageni wengine Moshi Mkoani Kilimanjaro, ushahidi mwingine uliopatikana ni kwamba wakati wa maandalizi aliazima gari ( T 642 EGU Toyota Ractis) kutoka kwa Jamaa yake ili imsaidie katika shughuli za harusi lakini hakulirejesha gari hiyo kwa Mwenyewe na badala yake November 18,2024 ambayo inadaiwa alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo alikuwa anaitilia mashaka ndiyo siku hiyohiyo aliuza gari hiyo kwa kiasi cha shilingi milioni 9 na akalipwa milioni 8 ikabaki milioni moja “


“Taarifa iliyopo inaonyesha kuwa siku hiyohiyo alimtumia Mke wake kiasi cha fedha ili alipe madeni mengine yaliyotokana na harusi ikiwepo Coaster aliyokodisha kuwarejesha Wageni wake Moshi, gari hilo aina ya Toyota Ractis limefuatiliwa na limekamtwa, ushahidi mwingine unaonyesha huyu Vincent Peter Massawe pia anadaiwa na Watu wengine wawili mmoja kiasi cha milioni 53 na mwingine milioni 16, ukweli wa tukio hili utafahamika muda si mrefu kama amejipoteza au laah kulingana na mtiririko wa ushahidi ulivyo na hili linategemea hasa tukipata ukweli kutoka kwa Mke wake kwani inadaiwa anao ufahamu mkubwa wa jambo hili, mwisho Umma utajulishwa taarifa zilizo sahihi kuhusu Peter Masawe” ——— Polisi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad