Web

Hawawezi Kuufunga Uwanja wa Mkapa Waambieni CAF Waje Wakague Tena - Msigwa


Hawawezi Kuufunga Uwanja wa Mkapa Waambieni CAF Waje Wakague Tena - Msigwa


Baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) kutoa tangazo la kuufungia Uwanja wa Michezo wa Benjamin Mkapa, Serikali imesema walitakiwa kuwasiliana nao kabla ya kuufungia kwa sababu ulishakarabatiwa.

.

Akizungumza leo Machi 12,2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amethibitisha kupokelewa kwa tangazo la kuufungia uwanja huo leo asubuhi.

.

“Ni kweli leo wameamka na hiyo taarifa kuwa CAF wameufunga uwanja wa Benjamin Mkapa kwa sababu za dosari katika eneo la kuchezea. Ukaguzi wa CAF ulifanyika kama wiki mbili zilizopita na ulifanyika baada ya mechi ya Simba na Azam na kumbukeni sisi uwanja tulishautangaza kuufunga kupisha ukarabati,”amesema.

.

“Lakini hizi mechi zinakuwa na mashabiki wengi na mambo mengi ya kiusalama. TFF (Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania) likatuomba tunaomba tutumie uwanja, siku wamekuja pale uwanja ulikuwa umekatwa nyasi hadi chini kabisa. Kwa hiyo wachezaji walipokuwa wanacheza na unajua hizi mechi zina presha kidogo ukaenda unachimbika chimbika kidogo,”amesema

.

“Hata ‘derby’ (Simba na Yanga) kama ingefanyika juzi Benjamin Mkapa uko tayari. Baada ya tangazo lao la asubuhi tumewasiliana na TFF tukawaambia waambieni waje wakague leo uwanja,”amesema.

.

“Huwezi kukagua wiki mbili zilizopita halafu unakuja kuufunga uwanja baada ya wiki tatu, leo uwanja uko tayari mashine zimekuja, uwanja umeshakarabatiwa na uko tayari,” amesema Msigwa

.

“Kwa sisi kuendelea kutumia uwanja wakati unakarabatiwa unatuongezea gharama. Huu uwanja ulitakiwa kukamilika Agosti (2024) yaani hadi leo haujakamilika mmenielewa. Waje kuangalia uwanja umeshakarabatiwa na lile tangazo walitakiwa kutuambia kabla ya kulitoa,”amesema.

.

Source: [Mwanaspoti]

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad