SIMBA SC WAIACHA MBALI YANGA, WASHIKA NAFASI YA NNE KWA UBORA AFRIKA.
Baada ya kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, klabu ya Simba Sc y Tanzania imepenya kwenye orodha ya timu nne bora Afrika kwa viwango wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Simba Sc imefikisha pointi 43 na kukwea mpaka nafasi ya nne ya vilabu bora Afrika kwa viwango vya CAF nyuma ya kinara, Al Ahly wenye pointi 78, Mamelodi Sundowns pointi 57 na Esperance Sportive de Tunis wenye pointi 57 pia.
10 YA AFRIKA
1. 🇪🇬 Al Ahly — pointi 78
2. 🇿🇦 Mamelodi — pointi 57
3. 🇹🇳 Esperance — pointi 57
4. 🇹🇿 Simba SC — pointi 43
5. 🇲🇦 RS Berkane — pointi 42
6. 🇪🇬 Zamalek SC — pointi 42
7. 🇲🇦 Wydad AC — pointi 39
8. 🇪🇬 Pyramids FC — pointi 37
9. 🇩🇿 USM Alger — pointi 37
10. 🇩🇿 CR Belouizdad — pointi 36
simba tupo kwa ajili ya kukamilisha malengo yetu na si kulinganisha mafanikio yetu na timu zingine
ReplyDelete