Web

Yanga Waitandika Azam Bila Uruma, Ice Cream Zimeingia Mchanga

 




Ice Cream Zimeingia Mchanga

Zamani wakati nacheza mpira mwalimu wangu Abel aliwahi kuniambia hivi

If you have control of the midfield, you have control of the game, and you have more chances to win.

Kwa ufupi kocha Abel alimaanisha ukiweza kutawala eneo la Katika mwa uwanja una nafasi ya kubwa ya kuitawala mechi na una nafasi kubwa ya kushinda mechi.

Azam pale chamazi walifanya kosa kubwa kukubali Yanga walichukue jiko la katikati ya uwanja.Azam walifanya makosa mengi ambayo

1.Yahya Zyaid +James Akaminko+Fei+Iddy Nado+Silha walishindwa kabisa kuweka presha ya kutosha kwenye mpira pale katikati dhidi ya mstari wa kiungo wa Yanga ambao ulikuwa na Duke+Max+Mudathir+Chama +Pacome

2.Hawakuzifunga nafasi vya kutosha ikawa rahisi kwa Chama+Pacome+Duke+Mudathir+Max kupasiana mpira na kulishambulia box la Azam kirahisi.

Yanga walikuwa Bora sana kwenye wakiwa na mpira mpira (off ball & on ball) Kivipi?

1.Na Mpira

Yanga wakiwa wanashambulia walikuwa wanakaa hapa 1-2-4-4 na walifaidika na

  1.1 Muda+Duke walikuwa bora kwenye kuitoa timu chini kwa pasi sahihi

  1.2 Idadi nzuri kwenye kulishambulia box la Azam wachezaji wasiopungua 7 (Max+Dube+Chama+Mzize+Boka+Kibwana)

2.Bila mpira

2.1 Yanga walikuwa mbwa mwitu kwenye kuweka presha kwenye mpira kwenye kila tukio kiwanjani wakati Azam wana mpira.

  2.2 Wachezaji wa Yanga walikubali kukimbia sana uwanjani ikawa rahisi kwao kupora mipira na kuwafanya Azam wasiwe huru wakiwa na mpira.

Zingatia

Yanga walikuwa bora sana kipindi kwa kwanza kuliko cha pili.

Azam muda mwingi wa mchezo hawakutoa mechi bora.

Ikangalombo mhhh🤔🤔

Full-time

Azam 1-2 Yanga

@omarrkombo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad