Showing posts with label Kenyan News. Show all posts
Showing posts with label Kenyan News. Show all posts

5/09/2022

Fahamu vijembe vya Raila Odinga, William Ruto kabla ya Uchaguzi Mkuu

 


Nchini Kenya, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu, wanasiasa kwenye taifa hilo la Afrika mashariki wanaendelea kufanya kampeni za kuwaraia wapiga kura kuwachagua katika wakati wa uchaguzi huo.


Maneno makali yamekuwa yakishuhudia kati ya naibu wa rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga wote wanaotaka kumrithi rais Kenyatta anayemaliza hatamu yake ya kuongoza taifa hilo baada ya  miaka 10.


William Ruto anayewania kupitia mrengo wa Kenya kwanza, amemtaka Raila Odinga, ambaye anawania urais kwa tiketi ya Azimio la umoja kustaafu na kwenda na kuwachana na siasa.


Ruto, akiwa katika harakati zake za kutafuta uungwaji mkono magharibi ya Kenya, eneo ambalo kwa muda  sasa limeonekana kuwa ngome ya Raila, amesema kuwa Odinga hana uwezo wa kutekeleza jambo lolote njema kwa raia wa taifa la Kenya na hawezi maliza ufisadi.


Ruto aidha ameendelea kukashifu maafikiano kati ya rais Kenyatta na Odinga maarufu kama Handshake, hatua anayosema imechangia pakubwa uwepo wa mianya ya ufisadi nchini Kenya.


Naibu huyo wa rais vilevile ametaka Odinga kuwajibikia kupotea kwa fedha kwenye shirika la usambazaji dawa nchini humo KEMSA.


Mwezi jana, Raila aliahidi kuwa atamaliza ufisadi iwapo wakenya watamchagua katika kura za urais za agosti tisa akieleza kuguswa na jinamizi la ufisadi nchini humo.


Odinga ameendelea kusisitiza mpango wake wa kuwapa wakenya wote wasio na ajira shillingi elfu sita pesa za kenya unawezekana na anajuwa mahali pesa za kufanya hivyo zipo.


Kinara huo wa chama ODM kwa mara kadhaa katika vyombo vya habari na mikutano ya kampeni amekuwa akimtaja naibu rais William Ruto kama mtu asiwezakuelezea vyanzo vya utajiri wake.

12/16/2021

Maskini Akothee Arudishwa TENA Hospitalini ni Baada ya Siku Chache Kuruhusiwa Kurudi Nyumbani, Afunguka Haya


Mwanamuziki mashuhuri wa Kenya Esther Akoth ambaye hujulikana kama Akothee amefichua kwamba alikaa siku ya Jamhuri alikuwa hospotali baada ya kulazwa tena.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram akithibitisha kisa hicho, alipakia picha kadhaa akidai kwamba hakuwa na wakati wa kutumia siku yake ya Jamhuri na familia yake.

Hii Inasemekana ilitokea siku chache baada ya kudaiwa kuruhusiwa kutoka katika hospitali alikokuwa amelazwa kwa muda.

Siku chache zilizopita, Akothee alifichua kuwa alilazwa baada ya kuugua ugonjwa unaojulikana kama ND ambao ni uharibifu wa neva unaosababisha mishipa ya fahamu ya mtu kuhisi ganzi na baada ya hapo inadaiwa kuvimba.

Baada ya kupakia Picha akiwa kwenye kitanda cha hospitali aliandika ujumbe huu;

✍“Siwezi kuelezea kile kinachonila, lakini kinaendelea kufanya jambo lake kwa wakati mbaya zaidi. Tumekuwa hapa tangu Jumamosi na hii ni sherehe yetu ya jamhuri. Leo naweza kuinua kichwa changu 💪” Akothee Aliandika

11/08/2021

Ukame na Njaa Tatizo Tena Kaskazini Mwa Kenya




Mizoga ya mifugo iliyonyauka ni ukumbusho kwamba ukame umeingia tena kaskazini mwa Kenya, ikiwa ni hali ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa yanayokumba Pembe ya Afrika.


Mizoga ya mifugo iliyonyauka ni ukumbusho kwamba ukame umeingia tena kaskazini mwa Kenya, ikiwa ni hali ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa yanayokumba Pembe ya Afrika.



Wakati viongozi wa dunia wakihutubia mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa kimataifa huko Glasgow, Scotland wafugaji wanatazama wanyama wao wakiteseka kwa ukosefu wa maji na chakula. Yusuf Abdullahi anasema amepoteza mbuzi 40. ";Ikiwa watakufa, na sisi sote tunakufa," alisema.



Serikali ya Kenya imetangaza janga la kitaifa katika kaunti 10 kati ya kaunti zake 47. Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 2 wana uhaba mkubwa wa chakula. Na huku watu wakienda mbali zaidi kutafuta chakula na maji, watafiti wanaonya kwamba mizozo kati ya jamii inaweza kuongezeka


Wanyamapori wameanza kufa, pia, anasema mwenyekiti wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Subuli, Mohamed Sharmarke.

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger