Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

6/16/2022

Simba SC imeanza na Moses Phiri, yamtambulisha rasmiHatimaye Klabu ya Simba SC imemtangaza Kiungo Mshambulia kutoka nchini Zambia Moses Phiri kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo, ambaye rasmi ataanza kuonekana kikosini msimu mpya wa 2022/23.

Phiri anakua mchezaji wa kwanza kutambulishwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2021/22, huku akitarajiwa kufanya makubwa msimu ujao 2022/23.

Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa, Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ambao rasmi utafikia ukingoni mwa 2024.

Simba SC ilianza kuhusishwa na mpango wa kumsajili Phiri msimu uliopita, lakini ilishindikana kutokana na mkataba wake na klabu ya Zanaco FC, ambayo ameitumikia kwa zaidi ya miaka mitatu.


 
Young Africans nao walihusishwa na mpango wa kumsajili Mshambuliaji huyo mwezi Januari mwaka 2022, nao pia waligonga mwamba, kufuatia Uongozi wa Zanzco FC kuweka ngumu kwa kisingizio cha kuhitaji huduma yake kwenye michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Barani Afrika).
Share:

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa CAFRais wa Shirikisho la soka barani Afrika  (CAF) Patrice Motsepe.
Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe. © AFP / Daniel Beloumou Olomo
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kawaida wa shirikisho hilo, utaoafanyika tarehe 10 mwezi Agosti.

CAF imesema mkutano huo wa 44 utafanyika katika jiji la Arusha, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa vyama wa soka barani Afrika na wadau wengine mbalimbali, kujadili maendeleo na changamoto za mchezo huo barani Afrika.

Kenya na Zimbabwe, zimefungiwa na Shirikisho la soka duniani  baada ya serikali zao, kuingilia masuala ya uongozi wa mchezo huo, kinyume na kanuni ya FIFA.


 
Mkutano mkuu wa 43 uliofanyika mwaka uliopita, ulifanyika jijini Rabat nchini Morocco.


 


Share:

Ali Kambwe 'Mambo 10 nilioyaona Mabingwa Yanga vs Coastal Union, Kuna Mabingwa wa Michongo na Kuna Mabingwa wa Mpira"

 


Mambo 10 nilioyaona Mabingwa Yanga vs Coastal Union


1: YANGA BINGWA🏆 PESA YA GSM, AKILI YA HERSI SAID, BUSARA YA MSOLLA NA UMOJA/UPENDO WA MASHABIKI UMEIFANYA TANZANIA KUWA YA NJANO NA KIJANI 💛💚


2: UNBEATEN CHAMPION ✊ YANGA BINGWA BILA KUPOTEZA MCHEZO. YANGA BINGWA AKIWA NA MECHI 3 MKONONI👏 QUALITY. QUALITY. QUALITY! Hivi ndio hadithi Fupi ya Yanga kwa msimu wa 2021/2022


3: BILA SHAKA JUMA MGUNDA AMEPATA DAKIKA 90 zenye somo kubwa kwake kuelekea Arusha kwenye Fainali.. Somo kubwa la mbinu! Ni kujiweka kitanzi shingoni kucheza na Yanga na ukawapa Faida ya namba Katikati ya uwanja. Kivipi?


4: Coastal Union walikuwa na mfumo wa 4-4-2 na walibadilika kwenye 4-2-4 wakishambulia. Mstari wao wa kwanza wa ulinzi wakachagua uwe wa juu [High Line Pressing]. Yanga wakawa na Quality ya kudili na presha yao Lakini Coastal wakamkosa kiungo mzuri wa chini wa kudili na ubora wa Feisal Salum


5: Yanga kwenye 4-3-3 .. Dickson Job na Bangala ni wazuri kwenye ‘Build Up’ .. Aucho na Sure Boy ni wazuri kwenye pasi.. Sopu alipokuwa na akili ya kushambulia tu, akaicha safu yake ya kiungo ikiwa kwenye muundo wa 2v3. Hii ikawa hatari sana kwao kucheza kwenye High Line


6: MAYELE✊ Top Striker! Mabao yake 16 msimu huu ukiyaweka kwenye tathimini nzuri utabaini idadi ya pointi alizochangia kwenye kuamua mechi.


7: NAMKUBALI SANA YANICK BANGALA! Ni vile tu tuko kwenye dunia inayoabudu namba kwenye mpira Lakini kwangu NI BANGALA ANASTAHILI KUWA MCHEZAJI BORA WA YANGA MSIMU HUU. Uwezo wake wa kubadilika uwanjani, utulivu kwenye maamuzi.. What A Player✊


8: Asante Nabi👏 Moja katika sajili bora alizofanya katikati ya msimu ni SURE BOY! Sure alikuja na Plan B ya Ufundi uwanjani.. Yanga waliweza kuwa na Approach tofauti wakiwa na Sure boy! What A Signing 🙌


9: Yule Akpan anajua mpira! Vicent Aboubakar asante kwa jasho lako! Wenye macho wameona. Fighting Spirit yake kwenye kugombania mpira wa pili kati yake na Farid Mussa ulikuwa kivutio sana uwanjani


10: DJUMA SHABANI 👏 ile Movement ya FeiToto.. Ile pasi yake kwa Mayele ni Class ya viwango vya juu sana! Well Done WANANCHI! Mmejua kumwagilia mioyo ya mashabiki wenu


Nb: Kuna Mabingwa wa michango na KUNA MABINGWA WA MPIRA 😃

Share:

Yanga Bingwa Ligi Kuu Bara....Mayele Atupia Mbili TakatifuMABAO mawili ya Fiston Mayele na moja la Chiko Ushindi yametosha kwa Yanga kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara 28.
MABAO mawili ya Fiston Mayele na moja la Chiko Ushindi yametosha kwa Yanga kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baada ya ukame wa misimu minne huku watani zao, Simba wakitwaa taji hilo mfululizo, Yanga imezinduka msimu huu na kutwaa kwa mara ya 28.

Shukrani za kipekee kwa mashabiki wa Yanga zimeelekezwa kwa Mayele usiku wa leo maana mbali na kupachika mabao hayo alitia asisti kwa Chiko aliyefunga bao lake la kwanza kwenye ligi tangu ajiunge na Yanga akitokea TP Mazembe.

Mayele alianza kupachika bao la kwanza kwenye mchezo huo dakika ya 34 kabla ya kumtengenezea Chiko na kupiga la ushindi kipindi cha pili.


Mabao mawili ambayo Mayele ametupia yanamfanya kurejea kwenye kilele cha wafumania nyavu Ligi Kuu Bara huku akimpiku bao moja mzawa, George Mpole mwenye mabao 15.

Awali Mpole alikuwa akiongoza orodha hiyo kwa tofauti ya bao moja kufuatia kupachika kwake bao kwenye mchezo uliopita wa Geita Gold dhidi Dodoma Jiji.

Ushindi huo unamaana kuwa Yanga imefikisha pointi 67 ambazo hakuna timu ambayo inaweza kuzifikia kwenye mchezo iliyosalia.


Licha ya Coastal kugeuzwa ngazi na Yanga kwenye mchezo huu inanafasi ya kulipiza kisasi kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC ambao watakutana.
Share:

6/15/2022

Ronaldo Kulipa Bilioni 47.8 Kujiandaa Kustaafu

 


Taarifa kutoa nchini Ureno zinaeleza kuwa Cristiano Ronaldo sasa atalazimika kulipa pauni milioni 17 za England sawa na Bilioni 47 na zaidi ya Milioni 889 za Kitanzania kwa ajili ya kujenga nyumba yake mpya huko 'Riviera' nchini Ureno ili aishi akistaafu soka.Cristiano Ronaldo na baadhi ya nyumba anazomiliki hadi sasa.


Mshambuliaji huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka 37, alinunua eneo kubwa sana Quinta da Marinha, kwenye pwani ya magharibi ya nchi yake ya Ureno mapema mwezi september mwaka jana, iliyopewa jina la utani la Mto wa Kireno ('Portuguese Riviera') kutokana na hadhi yake likiwa ni eneo la kifahari na la gharama kubwa.


Ripoti za hapo awali zilidokeza kwamba Ronaldo amepanga kuishi hapo na familia yake wakati atakapo tundika daluga. Nyota huyo wa mashetani wekundu pia anamiliki mali ikiwa ni pamoja na jengo la ghorofa saba huko Funchal mjini Madeira, ambako mama yake Dolores mwenye umri wa miaka 66 na kaka yake Hugo wanaishi baada ya kuinunua miaka miwili iliyopita.


Ronaldo, pamoja na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wake wanne, pia ana miliki nyumba ya kifahari mjini Turin nchini Italia aliyonunua wakati akiwa Juventus, pamoja na jumba la kifahari kwenye ngome iitwayo La Finca karibu na Madrid nchini Hispania.


Mpango huu wa kujenga nyumba mpya ni mali iliyopangwa kuongezwa hivi punde ingawa Ronaldo bado hajaonyesha kuwa tayari kustaafu kwa sasa, licha ya ujenzi huo kutarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao

Share:

Manara: Kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Yanga Tutaingiza Wachezaji 7-9, Morrison Ndani
Msemaji wa Yanga Haji Manara
MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa kulingana na mafanikio waliyokuwa nayo klabu ya Yanga msimu huu kikosi bora cha msimu kwa mtazamo wake kinatakiwa kiwe na wachezaji zaidi ya 7 hadi 9.

Manara ameongea hayo kuelekea mchezo wa timu yake dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 2:30 usiku.

Msemaji huyo ameongezea kwa kusema kuwa mchezaji wa Simba Bernard Morrison naye anastahili kuwemo kwenye kikosi hicho licha ya kucheza michezo michache ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.


Kikosi cha Yanga
Alipoulizwa kwanini Bernard Morrison, wakati amecheza michezo michache? Manara alijibu kuwa Bernard Morrison ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na ubora mkubwa unaomfanya aingie kwenye kikosi hicho.


 
Yanga itaingia uwanjani huku ikitarajiwa kukosa huduma ya nyota watatu Bakari Mwamnyeto ambaye ni majeruhi, Djigui Diarra ambaye hajapata mazoezi ya kutosha kutokana na kuwasili nchini muda si mrefu akitokea nyumbani kwao Mali pamoja na Kibwana Shomari ambaye ana jumla ya kadi tatu za njano.
Share:

Mchezaji Saido Aweka wazi Timu yake MpyaALIYEKUWA nyota wa Yanga, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ jana aliondoka nchini kurudi kwao Burundi huku akilidokeza Mwanaspoti, kuwa atarudi Bongo msimu ujao.

Saido aliyemaliza mkataba na Yanga, Jumapili hii alitinga kambini kuwaaga wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi na jana mchana alipanda ndege kwenda kwao, lakini akafunguka kuwa atarudi tena nchini.

Nyota huyo aliyeifungia Yanga mabao saba na kutoa asisti nne, ameeleza kuwa hatarudi Yanga, lakini msimu ujao atakuwa Tanzania.

“Naenda nyumbani kupumzika lakini nitarudi Bongo Mungu akijaalia. Sitarudi Yanga ila nitabaki kuiheshimu kutokana na nyakati tulizokuwa pamoja,” alisema.

Mwanaspoti linajua kuwa Saido anawindwa na timu tatu hadi sasa zikiongozwa na Simba ambayo tayari imeanza mazungumzo naye na ameipa masharti na vigezo anavyotaka ili asaini, sambamba na Azam na Singida Big Stars (zamani DTB). Alipoulizwa kuhusu ni timu gani kati ya hizo atarudi msimu ujao kucheza, aliweka wazi kuwa hadi sasa hajafikia mwafaka na timu yoyote lakini anaamini siku sio nyingi atasaini mkataba mpya.

“Timu zote hizo ni nzuri na baadhi tumezungumza nazo lakini sijasaini. Ni mambo madogomadogo ya kimkataba yamefanya nisisaini na kama yakitimizwa basi nitasaini Inshallah,” alisema, lakini Mwanaspoti linajua amefanya mazungumzo na Simba na kuwapa masharti ya mkataba wa mwaka mmoja ambao utakuwa na kipengele cha muda mwingi wa kucheza na kuondoka akipata timu.
Share:

6/14/2022

Barbara Gonzalez: Tumedhamiria Kuijenga Mo Simba Arena

 


Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez leo Jumanne (Juni 14) ametembelea eneo la Uwanja wa Mo Simba Arena lililopo Bunju jijini Dar es salaam, akiongozana na msanifu majengo (architect).


Barbara alifanya ziara hiyo iliyohudhuriwa pia na Waandishi wa Habari kwa lengo la kukagua mipaka na eneo ambalo litatumika kwa ujenzi wa Uwanja Mo Simba Arena, ambao kwa sasa unatumika kwa mazoezi ya vikosi vya klabu hiyo.


Akiwa katika zoezi la ukaguzi wa maeneo ya Uwanja huo Barbara alisema, zoezi la kujenga majukwaa na miundo mbinu mingine ya Uwanja wa Mo Simba Arena wamelidhamria na zimebaki siku chache kabla ya Bodi ya Wakurugenzi itakayokutana Ijumaa (Juni 17) ili kumpitisha mkandarasi.


“Tuna mpango wa kuboresha uwanja wa Mo Simba Arena, kuweka uzio na majukwaa ili watu wakija hapa wafurahie zaidi “


“Kazi ya bajeti tutapata kwa Architect lakini naona ikiwa chini ya Bilioni 2 kwa uboreshaji wa viwanja hivi vya mazoezi”


“Mimi kama CEO kazi yangu ilikuwa ni kutengeneza michoro kazi iliyobaki ni kuwaachia bodi kutoa marekebisho au kutoa ruhusa kuendelea,”


“Baada ya ruhusa ya bodi sasa ndiyo mtaona mambo yakianza kwenda kwa kasi zaidi sasa,” alisema Barbara Gonzalez

Share:

Zari Kanunua Nyumba?, Azindua Mjengo wa Kifahari Nchini Kenya

 


ZARI The Boss Lady; ni mwanamama tajiri Afrika Mashariki na Baby mama wa staa wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz ambaye wikiendi iliyopita alikuwa nchini Kenya akizindua mjengo mpya anaodaiwa kununua jijini Nairobi.


Nyumba hiyo aliyozindua ina mtindo wa ndani wa kipekee ambao hakuna kwa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Zari, alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya kununua nyumba katika Jiji Kuu la Kenya, Nairobi.

Alisema; “Niko huku kwa uzinduzi wa nyumba ya kifahari iliyojengwa kwa mtindo wa kisasa, ni mojawapo ya majumba usiyotarajia kuyaona Afrika Mashariki.”Zari Hassan maarufu kama Zari The Boss Lady amefanikiwa kupata watoto wawili akiwa na Staa wa muziki Afrika Diamond Platnumz kutoka Tanzania


Zari mwenye umri wa miaka 42 ni mfanyabishara kutoka nchini Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini. Alizaliwa mjini Jinja huko Uganda, wazazi wake ni Waganda kwa kuzaliwa.


Kiwango kikubwa cha utajiri wake kimetokana na uwekezaji katika nyanja za mali isiyohamishika au real estate, hoteli za kifahari za nyota tano huko Kampala na Shule ye Brooklyn huko Afrika Kusini.


Wapo wanaosema amenunua mjengo huo, lakini wengine wanasema alikwenda kufanya uzinduzi tu kwa kuwa ni balozi wa kampuni ya real estate (ya kununua na kuuza nyumba).

Cc; @sifaelpaul


Share:

6/13/2022

Haji Manara "Mashabiki Njooni Kwa Mkapa Siku ya Jumatano Mshuhudie Tukichukua Ndio"Klabu Yanga imewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Juni 15, 2022 siku ya Jumatano dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari, Afisa Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wachezaji wanapenda kuona mashabiki wanajitokeza kwa wingi ili kutoa hamasa kwa wachezaji ili waweze kushinda mchezo na kutangazwa kuwa mabingwa wapya msimu wa 2021/22.

Share:

Saido: Ishu yangu na Simba ipo hiviKIUNGO mshambuliaji aliyekuwa akikipiga Yanga, Said ‘Saido’ Ntibazonkiza amevunja ukimya na kueleza mustakabali wake kwa msimu ujao, huku akifunguka kila kitu juu ya ishu yake ya kutakiwa kuvaa uzi wa rangi nyeupe na nyekundu wa vijana wa Msimbazi, Simba.

Mashabiki wa Simba wameanza kuwatambia wenzao wa Yanga wakiwaambia “hamtaamini” baada ya kusikia kwamba mabosi wao wanamnyatia Saido na nyota huyo wa Burundi amezungumza na Mwanaspoti na kuanika kila kitu kilichopo juu ya dili la Msimbazi.

Saido aliachana na Yanga baada ya kuimaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi uliopita na sasa ni mchezaji huru na tayari mabosi watatu wa Simba walishawasiliana naye kwa vipindi tofauti na kumuwekea mkataba wa mwaka mmoja mezani.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Simba ilitaka kumsajili kwa mkataba huo mfupi, lakini naye aliweka masharti ikiwamo kutaka kipengele kitakachompa uhuru wa kutimka akipata timu nyingine, mbali na kupata nafasi ya kucheza kikosini.


 
Hata hivyo, mazungumzo ya pande hizo mbili hayakupata muafaka kwani mabosi walikuwa wanakuna kichwa juu ya sharti ya kupata wasaa mkubwa wa kucheza na kutimka akipata timu, japo Mwanaspoti linafahamu jamaa(Saido) ana ofa kutoka klabu mbili za Arabuni, Qatar na Saudi Arabia.

Akizungumza na Mwanaspoti, Saido alikiri kufuatwa na viongozi wa Simba sambamba na timu nyingine ikiwemo Singida Big Stars na kuweka wazi kuwa hadi sasa hajaamua wapi asaini.

“Zimekuja ofa nyingi mezani, wote hao unaowataja (Simba na Singida) nimeongea nao tu, ila sijasaini kokote. Kila upande kuna sababu zake na viongozi wa timu hizo wanazijua na huenda wanazifanyia kazi,” alisema Saido na kuongeza:


“Sitaki kuliongelea sana hili, tusubiri kwanza kila kitu kikamilike mtaambiwa wapi nitacheza msimu ujao.”

Kiungo huyo aliyeifungia Yanga mabao saba na asisti nne msimu huu, huku akiwa mmoja ya nyota walioisaidia timu hiyo kuganda kileleni kwa muda mrefu na kubakisha hatua chache ya kutawaza ubingwa, ikiwa ni baada ya kulisotea taji kwa misimu minne mfululizo mbele ya Wekundu wa Msimbazi.
Share:

ZA NDAANI KABISA: Wakala ampeleka Nabi SimbaINAWEZA kuwa habari ya kushtua sana kwa mashabiki wa Yanga, lakini ndivyo ilivyo kwamba wakala wa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, alilipelekea jina la kocha huyo kwa mabosi wa Simba ili kumtafutia kazi mpya.

Za Ndaani Kabisa, zinasema kuwa wakala huyo alilipelekea jina la Nabi kwa vigogo wa Msimbazi, baada ya awali klabu hiyo kuchomoa kumchukua ilipokuwa ikisaka kocha wa kuziba nafasi ya Sven Vandenbroeck aliyekuwa ametangaza kuachia ngazi siku chache baada ya kuifikisha timu hiyo makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Taarifa hizo zinasema Simba ilimkataa Nabi na kumchukua Didier Gomes aliyekuwa amepishana na Nabi ndani ya El Merreikh ya Sudan.

Gomes alijiondoa El Merreikh ilipotinga makundi na nafasi yake kuchukuliwa na Nabi ambaye alikaa kwa muda mchache kabla ya kufurushwa baada ya kuboronga makundi ikiwamo kutoka suluhu na Simba mjini Khartoom katika mechi zao za makundi msimu huo.

Inadaiwa kufanya vyema kwake akiwa na Yanga, kulimfanya wakala wa Nabi kuwarudia tena Simba ilipomtema Pablo Franco aliyekuwa ameziba nafasi ya Gomes, huku jeuri ya kuwapigia simu mabosi wa Wekundu ikitokana na mkataba wa mteja wake Yanga kuwa ukingoni.

Hata hivyo, Za Ndaani zinasema, mabosi wa Simba wameamua kumkaushia Nabi kuhofia wasizinguane na wenzao wa Yanga, pia msimamo wa Nabi wa kutaka kusalia Jangwani ili kuendeleza kile alichoanza nacho tangu ajiunge nayo Aprili mwaka jana, ndio imewatia ubaridi vigogo wa Msimbazi. Mkataba wa Nabi unatrajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu.

Nabi tangu ajiunge na Yanga, ameiongoza Yanga katika mechi za Ligi Kuu Bara 34, ameiongoza Yanga kucheza mechi 33 mfululizo bila kupoteza, ukiacha mchezo mmoja aliokuwa jukwaani siku ya kwanza ya kazi yake, timu hiyo ilipolala kwa Azam Aprili 25, 2021.
Share:

6/12/2022

Kitasa Afrika Kusini chajipeleka Simba


 
BAADA ya Simba kumnyatia kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio, hatimaye beki kisiki wa Burundi anayekipiga Afrika Kusini, Frederick Nsabiyumva amejipeleka Simba kiaina.

Misimu minne iliyopita, Simba ilikuwa mawindoni kuisaka saini ya beki huyo aliyekuwa Chippa United ya Afrika Kusini, ila ilishindikana kutokana na gharama za kuvunja mkataba na matakwa binafsi kuwa makubwa zaidi ya bajeti ya Simba.

Katikati ya msimu uliopita alimaliza mkataba na Chippa na kugoma kuongeza mwingine kutokana na timu hiyo kushindwa kumuongezea maslahi na kurejea Jomo Cosmos aliyoanzia maisha alivyotua Afrika Kusini kumalizia msimu na sasa yupo huru.

Mwanaspoti lilipiga stori na beki huyo juzi baada ya mechi ya timu ya taifa ya Burundi iliyofungwa mabao 2-1 na Cameroon kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kusema kwa sasa yupo tayari kujiunga na Simba.

“Misimu iliyopita kulikuwa na mazungumzo na Simba, ila hayakutimia kwa kuwa nilikuwa na mkataba na Chippa. Sasa niko huru na nipo tayari kuzungumza na timu yeyote,” alisema.

“Simba ni timu bora na inashiriki mara kwa mara michuano ya kimataifa hivyo hakuna mchezaji atagoma kuichezea kama wataelewana, ndio maana nimesema kama watahitaji huduma yangu basi ni suala la maongezi tu na tukifikia makubaliano basi nitasaini.” Simba inatafuta beki wa kati mwenye ubora kusaidiana na Henock Inonga na Joash Onyango msimu ujao wakishaachana na Pascal Wawa.
Share:

6/11/2022

Breaking: Yanga Yampitisha Injiani Hersi Ally Said Kuwa Mgombea Pekee Urais Yanga


Kamati ya Uchaguzi Yanga SC leo imetaja orodha ya Wagombea waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali katika Uongozi wa Yanga SC ambapo Injinia Hersi Ally Said @caamil_88 amekuwa Mgombea pekee aliyepitishwa kuwania Urais wa Club hii huku nafasi ya makamu wa Rais yakipita majina mawili ya Arafat Haji na Suma Mwaitenda.

Hata hivyo katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji ambapo kwa mujibu wa katiba ya Yanga itakuwa na wajumbe watano yamepitishwa majina 22 kati ya 27 likiwemo jina la Mbunge wa Manonga Seif Khamisi Gulamali.

Majina matano yaliokatwa kwa kigezo cha kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya kikatiba ni pamoja na Ayubu Shaibu Nyenzi, Sindilo Lyimo, Mustapha Salumu Himba, Kara Remtullah na Tobias Bosco Lingalangala

Share:

Hatimaye Wachezaji Chama, Bwalya Warejea Mazoezini SimbaChama anarejea mazoezini akiwa na kikosi hicho kutokana na kuuguza majeraha tangu alipocheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara Desemba 11, mwaka jana dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.
VIUNGO wa Simba, Clatous Chama na Rally Bwalya wameungana na timu hiyo katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena ikiwa ni siku moja tangu warejee nchini.

Chama alirejea jana akitokea kwao Zambia kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha mkewe, Mercy Mukuka kilichotokea Mei 29, mwaka jana.

Naye Rally Bwalya alitoka kwenye majukumu ya timu yake ya Zambia iliyokuwa inajiandaa na michezo ya kufuzu AFCON mwakani Ivory Coast.

Chama anarejea mazoezini akiwa na kikosi hicho kutokana na kuuguza majeraha tangu alipocheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara Desemba 11, mwaka jana dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.


Wachezaji waliofanya mazoezi ni, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Ahmed Feruzi, Pascal Wawa, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Gadiel Michael, Israel mwenda, Joash Onyango, Kennedy Juma na Henock Inonga.

Wengine ni Clatous Chama, Rally Bwalya, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Mzamiru Yassin, Taddeo Lwanga, Pape Sakho, Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Yusuph Mhilu na John Bocco.

Simba iliyopo chini ya Kaimu Kocha wake Mkuu, Seleman Matola baada ya Kocha Mkuu Pablo Franco kutimuliwa Mei 31, mwaka huu inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City Alhamisi hii ya Juni 16, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Share:

Klabu ya Liverpool ipo Tayari Kumuachia Mshambuliaji wake Sadio Mane


Klabu ya Liverpool ipo tayari kumuachia mshambuliaji wake Sadio Mane, ajiunge na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani kwa dau la pauni milioni 40.


Mane mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akishinikiza kutaka kuondoka wakati huu wa majira ya kiangazi.


Liverpool watakubali kuchukua kiasi hicho cha pesa ili kutunisha kibubu chao waweze kuinasa saini ya Darwin Nunez ambaye anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60.

Share:

Simba SC yashindwa kumsajili Victorien AdebayorMeneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally amethibitisha taarifa za klabu hiyo kusitisha mpango wa kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka Niger na klabu ya USGN Victorien Adebayor.

Adebayor alitajwa sana kuwa kwenye mipango ya usajili wa Simba SC, kufuatia kipaji chake kuwavutia baadhi ya viongozi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo, wakati wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22.

Ahmed amesema Simba SC imesitisha mpango wa kumsajili kiungo huyo, kufuatia mahitaji yake ya usajili kuwa makubwa, tofauti na matarajio ya klabu hiyo, ambayo msimu huu imeutema ubingwa wa Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

“Klabu yetu ya Simba SC imeachana rasmi na dili la kumpata Mshambuliaji wa Kimataifa wa Niger Victorien Adebayor, na hii ni baada ya kushindwana kwenye upande wa dau analotaka yeye” amesema Ahmed Ally

Hata hivyo Adebayor anatajwa kukamilisha dili la kujiunga na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane, na wakati wowote mwezi ujao atatambulishwa rasmi klabuni hapo.

Simba SC kwa sasa ipo kwenye mpango wa usajili wa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa, huku ikihusishwa na wachezaji kadhaa wa kimataifa.
Share:

6/09/2022

Simba SC yapangua hoja ya Chama kuvunja mkataba
Kiungo wa Kimataifa wa Zambia na Klabu ya Simba SC , Clatous Chama anatarajiwa kurejea nchini kesho Juni 10 mchana ili kuungana na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara. 

Chama aliondoka nchini wiki kadhaa kwa mapumziko mafupi sambamba na kujiuguza jeraha alililonalo na kumaliza matatizo ya kifamilia aliyokuwa nayo, ikiwamo kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kumbukumbu ya kifo cha mkewe, Mercy Chama aliyefariki dunia Mei 29, 2021. 

Kiungo huyo aliyerejeshwa nchini kutoka RS Berkane ya Morocco katika dirisha dogo baada ya timu hiyo kumsajili awali mwishoni mwa msimu uliopita, aliondolewa kikosi cha Simba siku chache kabla ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Yanga. 

Chama atarejea kesho (Ijumaa) Mchana nchini na moja kwa moja ataenda kambini kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi tano zilizobaki kukamilisha msimu huu. 


 
Kiungo huyo tangu arejee Msimbazi amefunga mabao manne na kuasisti moja katika ASFC, huku kwenye Ligi Kuu amefunga mabao matatu, licha ya kushindwa kutumika mara kwa mara chini ya Kocha Pablo Franco aliyetupiwa virago vyake Simba hivi karibuni. 

Share:

Urais Yanga Kumekucha...Ni Jeuri ya Pesa, RekodiKUMEKUCHA Jangwani. Vita ya nafasi ya Urais wa Yanga imeanza. Kuna majina makubwa kwa mashabiki na wanachama ambayo kabla kesho Jua halijazama yatapishana kuchukua fomu za nafasi hiyo.

Tayari ratiba ya uchaguzi huo chini ya Mwenyekiti, Malangwe Mchungahela inaonyesha zoezi hilo la kuchukua fomu litafikia tamati kesho Juni 9 likianzia Juni 5 na uchaguzi unafanyika Julai 10 mwaka huu.

Hatua ambayo itawaibua wagombea wengi leo na kesho kupishana kuziwahi fomu hizo ingawa baadhi walipanga kufanya kama sapraizi kwani siku nyingi hawajaonekana Jangwani.

Mwanaspoti limebaini kuna vikao vingi vinaendelea jijini Dar es Salaam vya kupanga mikakati huku baadhi ya wanaopanga kuchukua fomu wakitanguliza wapambe matawini kupima upepo lakini wanachunguza chini chini kujua nani mwenye nia ya kugombea hasa nafasi ya urais.


Karata hizo zinachezwa kiakili na kuna majina makubwa sita ambayo yanaviziana kuchukua fomu kuwania kiti hicho ingawa baadhi yao wapambe wao wameanza kuwanadi chinichini na kuhamasishana kujaa Jangwani siku ya kuchukua fomu.

Dk Mshindo Msolla amewaambia watu wake wa karibu lazima awanie tena kuendeleza mafanikio yake ya msimu huu.

Hata hivyo, Msolla atakuwa na vita nzito kutokana na majina mengine matano ambayo nayo yanakitaka kiti hicho ambayo yanaushawishi mkubwa kwa wanachama watakaopiga kura.


SEIF AHMEID

Hajasikika kwa kitambo kidogo Yanga lakini Seif Ahmeid ‘Seif Magari’ yumo. Kinara huyu ambaye alikuwa kwenye kamati ya mashindano inayokwenda kurudisha mataji alikuwa pacha wa Abdallah Bin Kleb katika kuisimamisha Yanga kwenye utawala wa Yusuf Manji, ambaye atachukua fomu kwa ushawishi wa makundi ya wanachama wa klabu hiyo.

HERSI SAID

Mhandisi Hersi Said ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, baada ya kuiwezesha Yanga kupitia nafasi yake ndani ya GSM na kamati ya mashindano sasa anataka kiti cha urais wa klabu hiyo na wakati wowote kuanzia leo atatua kuchukua fomu, Mwanaspoti limejiridhisha pia kutoka ndani ya klabu hiyo.

DAVIS MOSHA

Mosha ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga katika utawala wa Manji pia hivi karibuni msimu huu amekuwa akisafiri sehemu mbalimbali kuipa nguvu Yanga nyumbani na ugenini.

Mosha kama ilivyo kwa Seif anashawishiwa kwa kiasi kikubwa na makundi ya wanachama ambao wamemuahidi sapoti na kura za Urais na ameonyesha kuridhia ila ataibuka kama sapraizi.

ATHUMANI KIHAMIA

Mtu mzito mwingine ni Athuman Kihamia ambaye ni Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha akiwa pia kwenye Kamati ya Utendaji ya Yanga naye yumo katika vita hiyo, akipima upepo wa jinsi ya kuchukua fomu hiyo kwa kushtukiza.

ABBAS TARIMBA

Tarimba Abbas maarufu kwa jina la Thabo Mbeki ambaye ndiye muasisi wa mchakato wa mabadiliko akifanya hivyo miaka mingi nyuma naye anapiga hesabu za kuchukua fomu hiyo wakati wowote kuanzia leo akizidi kuweke ugumu wa kiti hicho.

Share:

Simba Yaifanyia Umafia Yanga kwa Straika wa Mabao, Apokea Ofa NonoUMAFIA! Ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya mabosi wa Simba kumfuata mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole na kumtangazia ofa nono ili asaini Msimbazi.

Inaelezwa kuwa Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kuonyesha nia ya kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo ambaye anachuana katika kuwania ufungaji bora na Mkongomani, Fiston Mayele wote wenye mabao 14.

Mpole ni kati ya washambuliaji wazawa walioonyesha kiwango bora katika msimu huu ambaye juzi aliifungia Stars bao la kuongoza katika kuwania kufuzu Afcon walivyocheza dhidi ya Niger ugenini mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.


Mpole amekuwa na msimu mzuri akiwa na jumla ya mabao 14 hadi sasa
Taarifa ambazo imezipata, Championi Jumatano, Simba imemfuata kimyakimya mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kuipata saini ya staa huyo wa Geita inayofundishwa na mzawa Fred Minziro.


 
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mshambuliaji huyo bado hajachukua maamuzi wapi atakwenda kati ya timu hizo mbili katika msimu ujao.

Aliongeza kuwa mazungumzo yanakwenda vizuri kati ya mshambuliaji huyo na timu hizo mbili kubwa hapa nchini zenye ushawishi wa usajili ambazo wachezaji wengi wanatamani kuzichezea.

“Tunafahamu tuna ushindani mkubwa katika usajili wa wachezaji wa ndani na nje ya nchi, lakini kama sisi Simba hatufanyi papara zaidi tutajipanga vema kuhakikisha tunafanikisha mahitaji ya wachezaji tutakaowahitaji.


“Mpole tupo katika mazungumzo mazuri kwa ajili ya kumsajili kama mipango ya usajili ikienda vizuri, kwani ni kati ya washambuliaji wazawa waliokuwepo katika kiwango bora msimu huu.

“Kama mipango itakwenda sawa, basi tutafanikisha usajili wa Mpole kwa ajili ya msimu uajo katika kuiboresha safu yetu ya ushambuliaji,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema kuwa: “Usajili wetu utafanywa na kocha wetu mpya atakayekuja kuifundisha katika msimu ujao.

“Usajili wetu hautakuwa na kelele nyingi kama ilivyokuwa kwa hao wenzetu, sisi usajili ukikamilika haraka tutauweka wazi.”

Share:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger