Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

6/18/2022

Rais Tshisekedi asema Rwanda inaendesha "vita ya kiuchumi"
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi ameituhumu Rwanda kuendesha vita ya kiuchumi na kujaribu kuinyakua ardhi ya Congo ili kujipatia rasimali kubwa ya madini.

Shirika la Habari la Associated Press limenukuu rais Tshisekedi  akisema hali ya usalama mashariki mwa Congo inaendelea kuzorota kwa sababu Rwanda inajaribu kudhibiti sehemu ya ardhi ya Congo yenye utajiri wa madini ya dhahabu na kobalti kwa manufaa yake.

Tshisekedi amesema kinachoendelea ni vita ya kiuchumi ya kuwania rasimali na Rwanda inayatumia magenge yake ya kigaidi.

Hapajawa na majibu yoyote kutoka nchini Rwanda kuhusiana na matamshi hayo ya Tshisekedi, ingawa Rwanda mara kadhaa imekanusha madai ya kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao waliukamata mji muhimu mashiriki mwa Congo mapema wiki hii.


 
Kwenye matamshi yake rais Tshisekedi  amewataka viongozi wa kimataifa ikiwemo waziri mkuu wa Uingereza kuikosoa Rwanda bila kificho pindi watakapohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola baadae wiki ijayo mjini Kigali. "Raia wa mashariki mwa DRC hawana hatia lakini wanashambuliwa na jirani yetu" amesema Tshisekedi.

Matamshi ya kiongozi huyo huenda yatachochea moto kwenye mzozo unaotanuka baina ya mataifa hayo jirani ya eneo la maziwa makuu.
Share:

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha na Wenzake Wapandishwa Kizimbani
Dk John Pima aliwahi kuwa Mkururgenzi wa Jiji la Arusha kabla ya Kutumbuliwa
MKURUGENZI wa zamani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na makosa nane katika kesi mbili za uhujumu uchumi.

Pima na wenzake watatu Innocent Maduhu (aliyekuwa mchumi wa Jiji), Nuru Ginana (mchumi), Alex Daniel (mchumi), wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Bittony Mwakisu na kusomewa mashitaka nane kwenye kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi.

Mbali na washitakiwa hao wanne, mshitakiwa mwingine ni Mariam Mshana ambaye alikuwa Mwekahazina wa Jiji hilo ambaye hakuwepo mahakamani hapo, ambapo upande wa Jamhuri umeiomba mahakama kutoa hati ya wito na kukamatwa kwa mshitakiwa huyo ambaye ni wa pili katika kesi zote.

Jamhuri imewakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Akisa Mhando na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Hamidu Simbano huku Dk Pima na Maduhu wakiwakilishwa na Wakili Valentine Nyalu.


 
Katika kesi ya kwanza inayowakabili Dk Pima, Mariam, Maduhu na Ginana wanakabiliwa na mashtaka manne ambayo ni ufujaji na ubadhirifu huku makosa mengine yakiwa ni matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa
Aidha washitakiwa hao wataendelea kukaa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ambapo kila mmoja anapaswa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka Sh32 milioni au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo, hadi watakapokamilisha masharti hayo.

Awali, Wakili Mhando aliwasilisha hati ya Mahakama hiyo kupewa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.


Mei 24 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji hilo kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

Watendaji hao walisimamishwa kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo katika kikao cha watumishi wa jiji kilichokuwa kinaongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa.

Kufuatia tuhuma hizo zilizotolewa na mbunge huyo, Waziri Mkuu aliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru kufuatilia suala hilo.

Kesi hizo zimeahirishwa hadi Julai Mosi mwaka huu ambapo watuhumiwa hao watasomewa maelezo ya awali.
Share:

Hoja Tano za Moto Bajeti ya Serikali


By Sharon Sauwa


Dodoma. Mjadala wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/23 ulianza jana bungeni, huku hoja tano zilizoibuliwa zikionekana kuwa moto zikigusiwa na wabunge tofauti.


Hali ikiwa hivyo bungeni, nje ya Bunge wadau wa bajeti, wakiwemo wafanyabiashara wenye viwanda, wataalamu wa uchumi na vyama vya siasa wameendelea kuichambua bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni Jumanne na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Mwigulu Nchemba


Miongoni mwa hoja hizo ni kuhusu nia ya Serikali ya kutaka wateule wanaoenguliwa kurudi kwenye mishahara yao ya zamani badala ya kuendelea na waliyokuwa wakilipwa wakiwa kwenye wadhifa.


Nyingine ni ya maofisa wa Serikali kukopeshwa magari ya ofisini ikilenga kubana matumizi na suala la kuondolewa kwa asilimia tano kati ya 10 ya fedha za mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kupitia halmashauri.


Pia, suala la kodi limeibua mambo mbalimbali kama kutoza asilimia mbili ya kodi kwenye madini, usafirishaji wa wanyama hai na uamuzi wa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 awe na Namba ya Mlipa Kodi (TIN) ili alipe kodi pale anapokuwa na kipato.


Mbunge wa kwanza kuchangia baada ya Kamati ya Bajeti kuwasilishi taarifa yake alikuwa Janejelly Ntate, mbunge wa Viti Maalumu ambaye alisema suala la kuwaondolea mshahara wateule wa Rais pale wanapoondolewa kwenye nafasi zao halitaleta tija.


“Hili linakwenda kuleta mgogoro kati ya watumishi na Serikali yao na vyama vya wafanyakazi,” alisema.


Alisema ukimhamisha mtumishi kutoka taasisi ya umma ambako kuna mshahara mkubwa na kumpeleka serikalini, hapunguziwi mshahara, lakini kwa wateule, Serikali inataka wapunguziwe mshahara pale wanaposhushwa madaraka.


“Jambo hili haliwezekani, Serikali ilitazame upya,” alisema.


Alisema Serikali kama inataka tatizo hili lisitokee, inapaswa kurudi kwenye mfumo wa zamani, ambapo wakurugenzi walikuwa wanachujwa na menejimenti ya utumishi wa umma tofauti na sasa.


“Hivi sasa hawa wateule mfano wakurugenzi wanateuliwa tu na mamlaka ya uteuzi, ndiyo maana mambo hayaendi sawa.


“Turudi kule tulikotoka, haya mambo ya fulani kaharibu toa, hayatakuwepo,” alisema mbunge huyo.


Mbunge huyo alishauri ili kushusha mshahara wa mtumishi, inatakiwa tume iundwe ambayo itatoa adhabu zitakazoakisi kitu ambacho Serikali inataka kufanya.


“Tume itajadili adhabu zitakazomfanya huyu mtumishi ashushwe cheo na apunguziwe mshahara kwa mujibu wa sheria au afukuzwe kazi, hivyo naiomba Serikali iliangalie hili upya,” alisema.


Lakini mbunge mwenzake wa Viti Maalumu, Judith Kapinga alisema ni vizuri vijana waandaliwe kushika nafasi za uongozi.


Hata hivyo, alisema hiyo haimaanishi kuwa vijana hawawezi kushika nafasi za uteuzi zinazopatikana serikalini.


“Nataka kushauri kama huyu mtu wakati wa uteuzi alikuwa katika nafasi ya juu serikalini, basi arudishwe katika nafasi ile, lakini si lazima nafasi zote za uteuzi zitoke serikalini.


Alisema wapo watu wa sekta binafsi ambao pia wanaweza kuteuliwa lakini waanze na mshahara utakaokuwa umepangwa na Serikali,” alisema Kapinga.


Hoja ya TIN


Katika hatua nyingine, Twaha Mpembenwe, mbunge wa Kibiti, alisema suala la kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 kuanza kulipa kodi limeleta mtafaruku ndani ya jamii na kuomba suala la kuwapa TIN vijana hao liwekwe wazi zaidi kwa Watanzania.


Alitolea mfano wa Uingereza kuwa kila anayefikisha miaka 18 anapewa kadi ya Taifa ya Bima na wanafanya hivyo ili mfumo umtambue mwanafunzi wakati anapomaliza masomo yake na kwenda kufanya kazi.


Akichangia hoja hiyo, Jerry Silaa, mbunge wa Ukonga, alisema kwa tabia ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaambia Watanzania kuwa kila mwenye umri wa miaka 18 apatiwe TIN wanajua watafanyiwa wanayofanyiwa wafanyabiashara.Hoja ya magari


Jambo jingine lililoibuka ni la watumishi wa umma kukopeshwa magari ili wayahudumie wao na kupunguza matumizi ya Serikali, ambalo Janejelly alitoa tahadhari kwa Serikali kuwa huenda suala hilo lisiwe na afya.


Alisema hoja hiyo ilishawahi kutekelezwa na Serikali ya awamu ya tatu, lakini Taifa lilipoteza viongozi wengi kutokana na ajali.


“Unakuta huyu kiongozi anatoka ofisini amechoka, anajiendesha mwenyewe kwenda nyumbani, anagongwa, saa nyingine anawaza mkuu wake wa kazi kampa mikakati ya ajabu ataifanyaje, mwishoni anagonga magari.


“Hili tuliangalie kwa mapana,” alisema.

Usafirishaji wanyama hai


Katika hatua nyingine, Silaa alizungumzia sauala la usafirishaji wa wanyama, akishauri kuimarisha mawasiliano ili kuepuka mambo yaliyojitokeza hivi karibuni, ya kuruhusu usafirishaji huo na baadaye ruhusa ikafutwa.


Alisema walikwenda Muheza mkoani Tanga na kukuta wasafirishaji wa vipepeo wanaathirika na zuio la Serikali la kusafirisha wanyama hai.


“Juzi Serikali ilitoa kauli hapa. Mimi nilielewa ni kusaidia wale wa vipepeo na wanaoshika mijusi na wanyama wengine wadogo, lakini kwa sababu haikushirikisha, ikatengeneza taharuki na Waziri wa Maliasili Dk Pindi Chana naye akajaa upepo akafuta lile agizo,” alisema.


Alisema matokeo yake waliokuwa wakisherehekea kufunguliwa kwa zuio hilo wakarudi tena kwenye masikitiko ya zuio la mwaka 2018.
Kodi ya wachimbaji wadogo


Vilevile, mbunge huyo wa Ukonga alisema kuongezwa kwa kodi ya asilimia mbili na kodi nyingine wanazotozwa wachimbaji wadogo, kunafanya kodi watakazotozwa kuwa asilimia tisa.


Mikopo ya halmashauri


Agnes Marwa, mbunge wa viti Maalumu yeye alilia na Serikali akitaka iangalie mahali itakakotoa asilimia tano ya fedha za halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa maeneo ya wamachinga badala ya kuitoa kwenye asilimia 10 zinazotengwa kwa ajili ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.


Mwananchi

Share:

Wamaasai Dar Waandamana Kukemea Upotoshaji

 

Kundi la jamii ya Kimaasai waishio Dar es Salaam, leo Juni 17, 2022, wameandamana katika Ubalozi wa Kenya na kuiomba serikali ya Kenya kuingilia kati upotoshwaji wa zoezi linaloendelea Ngorongoro, unaofanywa na Asasi za Kiraia pamoja na wanaharakati waishio nchini humo.


Wamaasai kutoka maeneo mbalimbali wamefanya maandamano ya amani hadi Ubalozi wa Kenya Tanzania, kuiomba serikali ya Kenya iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wanaharakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya Ngorongoro pamoja na tarafa ya Loliondo.


Wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya Wamaasai na serikali ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.


hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na Katibu wa Umoja huo anayetambulika kwa jina la Loishiye Lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la Emanuel.


hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la Loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa Ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la Handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo

Share:

Mawakili wa Mfalme Zumaridi waomba ahamishweMawakili wa upande wa utetezi katika inayomkabili Mfalme Zumaridi na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kama itawezekana mteja wao awekewe ulinzi au ahamishwe katika Gereza Kuu la Butimba alililopo hivi sasa kufuatia kuwepo kwa taarifa za kuuawa kwake ndani ya gereza.


Ombi hilo la Mawakili wa upande limewasilishwa hii leo Juni 17, 2022, ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Monica Ndyekobora, akawataka Mawakili hao kufikisha malalamiko hayo kwa uongozi wa Gereza Kuu la Butimba kwa ajili ya hatua zaidi huku akiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 30 ya mwezi huu.


Mfalme Zumaridi pamoja na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na imeanza kutolewa ushahidi ambapo leo hii shahidi namba moja ametoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza.

Share:

Mzozo wa Rwanda na DRC wazidi kufukuta

 Mzozo kati ya Serikali za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unaendelea kushika kasi huku Rais wa Kongo akiongoza Baraza Kuu la Ulinzi kupata majibu ya kwanini Warwanda wanaleta uchokozi.


Waziri wa Mawasiliano na Msemaji wa Serikali, Patrick Muyaya amesema baaada ya mkutano huo, serikali ilisema ilifikiria kusitisha mikataba yote iliyokubaliana na nchi hiyo jirani yake, ikimtuhumu kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23.


“Baraza la Juu la Ulinzi limechukua hatua zifuatazo, kwanza, wanaitaka Rwanda kuwaondoa mara moja wanajeshi wake wanaofanya kazi chini ya usiri wa kundi la kigaidi la M23, kutoka eneo la Kongo,” amesema Muyaya.


Katika hatua ya pili Waziri Muyaya amesema wanaiomba Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo isitishe kazi, itifaki zote za makubaliano na mikataba iliyohitimishwa na Rwanda hivi Karibuni.


Maendeleo mapya ya mgogoro huo, yanakuja baada ya maandamano kadhaa dhidi ya Rwanda kufanyika katika miji tofauti ya Kongo ambapo Jumatatu wiki hii Juni 13, 2022 mji wa mpakani wa Bunagana, ulitekwa na waasi na kuwalazimu maelfu ya wakazi kukimbia.


Rwanda na Uganda, zimekanusha kwa miaka mingi shutuma zilizopo za kuunga mkono kundi la M23, huku Serikali ya Rwanda ikivilaumu vikosi vya Kongo kwa kuwajeruhi raia kadhaa katika mashambulizi baada ya kuvuka mpaka.


Kundi la M23, lilipata umaarufu takriban muongo mmoja uliopita wakati wapiganaji wake walipoiteka Goma, jiji kubwa zaidi mashariki mwa DRC ambalo liko kando ya mpaka na Rwanda.


Hata hivyo, waasi hao walifukuzwa kutoka Goma na baada ya makubaliano ya amani, wapiganaji wengi wa M23 walijumuishwa katika jeshi la Taifa la DRC na mapema mwaka huu waasi hao walirejea, na kuanzisha mashambulizi dhidi ya jeshi la DRCongo baada ya kusema serikali imeshindwa kutimiza ahadi zake za muongo mmoja.


Rais wa Kenya Uhuru Kenyata alitoa wito kwa Kikosi kipya cha Kanda ya Afrika Mashariki kilichoanzishwa kuchukua hatua ya kulinda usala huku wakifanya jitihada za kuleta mapatano baina ya pande hizo mbili zenye mzozo uliotawala eneo la mashariki mwa DRCongo

Share:

Dkt. Pima na wenzake kizimbani kwa uhujumu uchumi

 


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi mbili za uhujumu uchumi zenye makosa nane.


Mbele ya Hakimu Mkazi, Bittony Mwakisu washtakiwa Dkt. Pima, aliyekuwa mchumi wa Jiji Inocent Maduhu, wachumi Nuru Ginana na Alex Daniel hii leo hii leo Juni 17, 2022 wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka nane kwa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi.


Mbali na washitakiwa hao wanne, mshitakiwa mwingine ni Mariam Mshana ambaye alikuwa Mweka hazina wa Jiji hilo ambaye hakuwepo mahakamani hapo, ambapo upande wa Jamhuri umeiomba mahakama kutoa hati ya wito na kukamatwa kwa mshitakiwa huyo ambaye ni wa pili katika kesi zote.


Serikali na CRDB zasaini hati ya makubaliano utunzaji taarifa za diaspora

Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Aksa Mhando na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Hamidu Simbano huku Dkt. Pima na Maduhu wakiwakilishwa na Wakili Valentine Nyalu.


Katika kesi ya kwanza inayowakabili Dkt. Pima, Mariam, Maduhu na Ginana wanakabiliwa na mashitaka manne ambayo ni ufujaji na ubadhirifu, huku makosa mengine yakiwa ni matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.


Hata hivyo, washitakiwa hao wataendelea kukaa Mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ambapo kila mmoja anapaswa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka Sh32 milioni au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.


Awali, Mei 24, 2022 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji hilo kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za jiji na tuhuma za kughushi nyaraka baada malalamiko yaliyotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo katika kikao cha watumishi wa jiji kilichokuwa kinaongozwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.


Kufuatia tuhuma hizo zilizotolewa na mbunge huyo, Waziri Mkuu aliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru kufuatilia suala hilo na kesi hizo zimeahirishwa hadi Julai Mosi mwaka huu kwa watuhumiwa kusomewa maelezo ya awali.

Share:

6/17/2022

UN yahofia ghasia Loliondo, Temu awatoa hofuMahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Juni 22, 2022 inatarajia kutoa uamuzi juu ya zuio la kisheria dhidi ya kuondolewa kwa wamasai katika maeneo yao, huku wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN), wakieleza hofu yao juu ya madai ya kumegwa kwa ardhi ya asili ya wamasai katika eneo la Loliondo lililopo Mkoani Arusha.


Kwa mujibu wa taarifa ya wataalamu tisa iliyotolewa jijini Geneva Uswisi Juni 15, 2022, imesema kitendo kinachoendelea eneo la Loliondo kinakosa uwazi na mashauriano baina ya Serikali na jamii ya wamasai, katika upangaji wa mipango na uamuzi na kuamua kuvihusisha vikosi vya ulinzi na usalama kulinda eneo lao hilo la kiasili.


“Tuna wasiwasi mkubwa na ripoti za vikosi vya usalama vya Tanzania kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi tarehe 10 mwezi huu wa Juni, kitendo kinachoripotiwa kusababisha watu takribani 30 kupata majeraha madogo na wengine makubwa sambamba na kifo cha afisa mmoja wa polisi,” wamesema wataalamu hao.


Wamesema, Juni 6, 2022 baada ya mashauriano ya faragha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela alitangaza uamuzi wa kugeuza eneo la ukubwa wa kilometa 1,500 za mraba kutoka eneo la kilometa 4,000 za mraba la ardhi ya vijiji linalojumuisha eneo la pori tengefu la Loliondo, kuwa pori tengefu.


Wataalamu hao wamesema mabadiliko hayo yanamaanisha kuwa wakazi 70,000 wa vijiji vya Ololosokwan, Oloirien, Kirtalo, na Arash villages,watalazimika kuhama.


Wakizungumzia eneo la Ngorongoro wamesema, “tuna hofu juu ya mipango ya Tanzania ya kuhamisha wamasai 150,000 kutoka eneo la hifadhi la Ngorongoro pamoja na Loliondo bila ridhaa yao au kujulishwa na kuamua kwa mujibu wa sheria za haki za kibinadamu za kimataifa.”


Katika hoja zilizojibiwa kwenye Mkutano wa 50 wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, jijini Geneva, Uswisi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa wa Geneva, Balozi Hoyce Temu amesema Serikali na wakazi wa Loliondo walijadiliana na kukubaliana kuwa kati ya kilometa za mraba 4,000 zilizopakana na vijiji 14, kilometa za mraba 2,500 zitumiwe na vijiji vya karibu kwa kujikimu kimaisha


“Baada ya serikali na jamii ya wakazi wa Loliondo kujadiliana na kukubaliana, kuwa kati ya kilometa za mraba 4,000 zilizopakana na vijiji 14, ilikubaliwa kuwa kilometa za mraba 2,500 zitumiwe na vijiji vya karibu kwa kujikimu kimaisha, na kilometa za mraba 1,500 ziwe kwa ajili ya uhifadhi chini ya serikali ya Tanzania au kwa jina jingine iwe pori tengefu,” amefafanua Balozi Temu.


Amesema, alama za mipaka zimeanza kuwekwa kwenye pori hilo tengefu la Loliondo, lakini watu wachache wenye nia mbaya ya mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuwapatia maisha bora wakazi wa Loliondo na kuendelea kuhifadhi eneo hilo kwa maendeleo endelevu, walianza kuandamana na kupinga mpango huo.


Balozi Temu amesema “katika hatua hiyo, baadhi ya waandamanaji walichukua picha na kuchanganya na picha ambazo hazikuwa za eneo hilo na Serikali i‭litoa wito kwa wale wanaodai kuumizwa ili sheria ichukue mkondo wake, lakini hakuna aliyejitokeza na wananchi wa Loliondo wanaendelea na maisha yao kawaida na kwa amani.”


ABalozi Hoyce Temu amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na majadiliano kuhakikisha wananchi wananufaika kiuchumi na kijamii na wawe na haki katika kufaidi ardhi yao.


Mwaka 2010, eneo la hifadhi ya ya Taifa ya Ngorongoro, lilitambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kuwa eneo la urithi wa dunia.

Share:

6/16/2022

Bashungwa Atoa Maagizo Michango ShuleniDodoma. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa shule nchini kuwashirikisha wazazi na walezi katika kupanga michango kabla ya kuanza kutoza.


Bashungwa amesema hayo leo Alhamisi Juni 16, 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migila.


Mbunge huyo alisema pamoja na Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi kwa elimu msingi bado kuna michango mingi ambayo ni kero kwa wazazi.


Ametoa mfano wa moja ya shule kijijini (hakuitaja) ya bweni ambayo wanafunzi wanatakiwa hadi kutoa mchango wa kitanda na kuna baadhi hadi chakula.


“Inapotokea mzazi ameshindwa kuchangia mtoto anaadhibiwa. Serikali inakauli gani kwa shule zinazotoa adhabu kwa wanafunzi ambao wameshindwa kulipa michango yao badala ya wazazi,”amesema Rehema.


Amesema kuwa upo mwongozo ambapo kamati za shule zinatakiwa kuwashirikisha wazazi na walezi.


“Ningependa kutoa maelekezo kwa walimu wakuu na wakuu wa shule kushirikisha wazazi ama walezi kupitia mwongozo ambao tumeutoa wa namna ambayo tunawashirikisha kwenye ile michango ambayo tunahitaji kuwashirikisha,”amesema.


Bashungwa amewaagiza wakuu wa shule na walimu wakuu wa shule kuwashirikisha wazazi, bodi za shule, kamati za shule na walezi kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

Share:

Uchaguzi Urais Kenya Unavyotoa Somo Tanzania

 


Kasoro ya Kenya kisiasa mpaka sasa ni ukabila na ukanda. Mathalan, mwaka huu baada ya Wakikuyu kutokuwa na mgombea urais mwenye nafasi ya kushinda, kulitokea ulazima wa mgombea mwenza.


Raila Odinga wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition na William Ruto, mwenye tiketi ya United Democratic Alliance (UDA), ndio vinara wa mbio za urais na wote wagombea wenza wao ni Wakikuyu kutoka Kanda ya Kati (Mlima Kenya).


Kwamba ilibidi Raila wa Nyanza na Ruto anayetokea Rift Valley, wafanye machaguo yenye kuwaridhisha Wakikuyu ili kujenga ushawishi mkubwa Mlima Kenya. Raila mgombea mwenza wake ni Martha Karua, Ruto yupo Rigathi Gachagua.


Shida kubwa ya Kenya ni kuwa ngome za kisiasa zinaundwa kwa nguvu ya ukabila na kanda. Yaani ukitaka kura za Wakamba lazima ubebwe na ‘samaki mkubwa’ wa ukambani, Kalonzo Musyoka ambaye ni Mkamba.


Unapohitaji kujizolea kura nyingi kwa waswahili wa Pwani, omba mkono wa mswahili Hassan Joho. Hiyo ni hali halisi katika maeneo mengine. Na hilo ndilo tatizo kuu la Kenya. Waluo na Mluo, Wakikuyu kwa Mkikuyu, Wakalenjin na Mkalenjin, na kadhalika.


Tanzania ilishavuka hilo eneo miaka mingi. Kabla ya uhuru, baada ya Tanganyika kuwa dola huru na hata ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hakuna ‘uzuzu’ wa kupiga kura kikabila, wala kikanda. Shukurani nyingi kwa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuufanya ukabila kuwa hauna maana mbele ya Utanzania.


Ukiacha ukabila, Kenya wanaipa somo Tanzania kuhusu namna bora ya kuzielekea siasa katika nchi za dunia ya tatu; kufuta ukiritimba wa vyama na kubebwa na mambo mawili ambayo ni haiba na agenda.


Kenya leo haiangalii ni chama gani kinagombea, anatazamwa mgombea, vilevile agenda anayobeba kwenye uchaguzi. Tanzania bado watu wanakumbatia vyama vya siasa kama dini. Huu ndio “ushamba wa kisiasa” usiotakiwa.


Pamoja na Kenya wameshavunja dari ya kioo katika siasa za ukiritimba wa vyama, bado zama mpya zinabebwa na masilahi binafsi kuliko muktadha wa kesho njema ya taifa hilo.


Mathalan; Kalonzo amelazimika kubaki Azimio la Umoja na kumpigia kampeni Raila kwa kuwa hana pa kwenda na ana ahadi ya kuteuliwa kuwa Waziri Kiongozi. Vilevile, Musalia Mudavadi na Moses Wetang’ula, wapo na Ruto kwa sababu ya nafasi za uongozi.


Ukiacha hilo, Wakenya wapo kwenye nyakati bora za kuifundisha dunia ya tatu kuwa vyama ni majukwaa tu ya kusaka dola na uongozi wa kisiasa. Mtu akija kuomba nafasi ya kuongoza, apimwe kwa agenda yake, rekodi zake kama zipo au historia yake.


Siasa za “chama chetu ndio mwarobaini wa matatizo”, hazina uhalali. Zimepitwa na wakati. Agenda ya wakati husika pamoja na aina ya wagombea, ndio mauzo yanayotakiwa sokoni.


Tanzania bado imekumbatia siasa za kiitikadi mithili ya dini. Kama ambavyo kila dini itakuja na ushawishi kuwa yenyewe ndio njia sahihi ya kwenda peponi, kadhalika vyama. Kila kimoja kinajenga ushawishi wa jumla kuhusu kesho ya nchi.


Uongozi mzuri haujengwi na propaganda za nchi ya ahadi, palipo na mito yenye asali na maziwa, bali huundwa kwa agenda na haiba ya mtu katika kutafsiri nadharia kwenda vitendo kiuongozi.


Kenya inafundisha kuwa sura ya leo kisiasa isikuongopee, ya kesho huyajui. Raila alipambana miaka 20 na Rais Uhuru Kenyatta, lakini leo wapo pamoja.


Ruto alikuwa ‘patna’ wa Uhuru katika safari ya urais, ila kuelekea Uchaguzi Mkuu Kenya unaotarajiwa kufanyika Agosti 9, mwaka huu, kila mmoja ameshika njia yake.


Mwaka 2002, Raila aliongoza vuguvugu la kuibomoa Kanu, kwenda kuunda Narc, sababu ikiwa kumkataa Uhuru kugombea urais. Raila akasimama na Mwai Kibaki dhidi ya Uhuru. Kibaki alishinda.


Mwaka 2007, Uhuru alimuunga mkono Kibaki kwa nguvu kubwa, aliyekuwa anashindana na Raila. Safari hiyo, Ruto alikuwa bega kwa bega na Raila. Wakati mwaka 2002, Ruto alimpigania Uhuru kwa nguvu kubwa.


Mwaka 2007, Ruto na Uhuru walinyukana, kila mmoja akimtaka wa kwake ashinde, damu ikamwagika Kenya.


Mwaka 2013, Uhuru na Ruto wakawa kitu kimoja dhidi ya Raila, ikawa hivyohivyo mwaka 2017. Baada ya miaka 20, Uhuru yupo kwenye maombi akiwataka Wakenya kumchagua Raila, kwani ndiye kiongozi anayewafaa na sio Ruto, aliyeshirikiana naye kuongoza serikali kwa miaka tisa.


Tanzania bado kuna siasa za watu kuitana wasaliti baada ya kutofautiana. Kenya imeshavuka huko.


Usije kustaajabu miaka mitano ijayo, Uhuru akasimama jukwaani kumwombea kura Ruto. Itategemea na mazingira ya wakati husika.


Imewezekana kwa Raila na Uhuru kuunganishwa na Mpango wa Kujenga Daraja la Maridhiano (BBI), haitashindikana siku Uhuru na Ruto watarejea mezani na kusafiri pamoja kutokana na agenda ya wakati husika.


Wakenya wameshavuka siasa za ubinafsi wa vyama na sasa wanaamini katika “umoja ni nguvu”. Raila na Ruto, wamehakikisha wanajenga kambi zenye kuviweka pamoja hadi vyama vidogo kabisa. Ni kwa sababu umoja ni nguvu.


Tanzania, bado kila chama kinataka king’ang’ane chenyewe kwenye uchaguzi. Kishinde ili kimiliki kila kitu kwenye dola.


Kisichangie madaraka na vyama vingine. Kingine kibebe kambi ya upinzani, kitambulike kama kinara wa upinzani.


Wakenya walishajifunza. Uchaguzi Mkuu mwaka 1992 na 1997, Rais Daniel arap Moi, alishinda kwa sababu wagombea na vyama vingine, walishiriki kwa dhamira ya kutaka kushinda. Wakagawa kura, Moi akashinda kiulaini.


Kenya ilifanya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Waliochuana kugombea urais walikuwa nane. Hata hivyo mechi ilikuwa ya wanne, waliosalia walisindikiza.


Moi (Kanu), alivuna asilimia 36.35, akashinda uchaguzi. Kituko ni kuwa Kenneth Matiba (Ford Asili), Mwai Kibaki (DP) na Jaramog Odinga (Ford Kenya), walipata kura jumla asilimia 62.9.


Hivyo, kama Matiba, Kibaki na Jaramog wangeungana dhidi ya Moi, pengine Moi asingeibuka mshindi. Kwa kuwa wagombea wa upinzani walitaka kila mmoja aoneshe msuli wake, ikawa nafuu kwa Moi.


Kama ulivyo msemo wa kuvuja kwa pakacha, mwaka 1997, wapinzani waliingia kwenye uchaguzi wakiwa wamesambaratika.


Moi akishinda uchaguzi kwa kupata kura asilimia 40. Wakati wapinzani, Kibaki, Raila Odinga, Michael Wamalwa na Charity Ngilu, walivuna kura asilimia 58.14.


Mwaka 2002, wapinzani walipoungana Narc, Kanu ikaondolewa madarakani. Mwaka 2007, ilijenga picha ya umuhimu wa kuungana, kisha mwaka 2013, siasa za Kenya zimetengeneza ‘fasheni’ ya ushirikiano wa vyama kuelekea uchaguzi.


Vyama sio dini, ni majukwaa ya kusaka uongozi na dola. Nyakati hizi ambazo vyama havizungumzi itikadi, isipokuwa agenda, Kenya inapaswa kuwa mwalimu mzuri.


Hasa vyama vya upinzani. Kutengeneza agenda na kuunganisha nguvu ili kuvuna matunda ya haiba za kila upande.

Share:

Makamu Wa Rais Apokea Gawio La Serikali Kutoka Nmb June 15

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameagiza Mashirika ambayo Serikali ina hisa kuhakikisha yanaanza kutoa Gawio kwa serikali mara moja, pia Taasisi zinazotakiwa kutoa asilimia 15 ya mapato ghafi kwa mujibu wa sheria zifanye hivyo kikamilifu na kwa wakati.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya kupokea Gawio la shilingi bilioni 30.7 kutoka kwa Benki ya NMB iliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2022. Amesema Mashirika ambayo yanategemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Serikali yanapaswa kuwa na  mikakati madhubuti na inayotekelezeka ya kupunguza utegemezi kwa Serikali na kumuagiza  msajili wa Hazina kuhakikisha  wakuu wa taasisi husika wanatekeleza maagizo hayo.


Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha na kuweka mazingira rafiki na endelevu ya kufanya biashara katika sekta ya fedha na sekta zote nchini. Pia ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii nchini (corporate social responsibility) sambamba na kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato. Amewaasa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuboresha  huduma za kijamii kwenye sekta mbalimbali kama afya,elimu na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na  kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na tabiawatu.


Kwa Upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Wizara itaendelea kusimamia maelekezo ya kuhakikisha taasisi za serikali na zile ambazo serikali ina hisa zinatoa Gawio. Aidha amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za sekta binafsi ili kuweza kuhakikisha zinafanya kazi vizuri.


Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Gawio la Serikali kutoka Benki ya NMB limeendelea kukua kila mwaka na kuwa endelevu mpaka kufikia bilioni 30.7 kwa mwaka 2022 kutoka bilioni 10.48 mwaka 2018. Amesema adhma ya NMB ni kuleta tija kwa wawekezaji ikiwemo serikali ambayo inamiliki hisa za asilimia 31.8.


Aidha Bi Zaipuna ameongeza kwamba Benki ya NMB itaendelea kuwa mdau mkubwa wa serikali katika kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kupitia uwekezaji katika sekta ya kilimo na biashara. Amesema mpaka mwezi Desemba 2021 jumla ya mikopo ya shilingi Trilioni 4.3 imetolewa kwa wakulima na wafanyabiashara.

Share:

6/15/2022

Jinsi Serikali itakavyookoa matumizi ya Sh500 bilioni

 


Katika mkakati wa kubana matumizi, Serikali inatarajia kudhibiti mambo kadhaa ikiwemo ununuzi na matumizi ya magari.


ADVERTISEMENT

New Content Item (1)By Tuzo Mapunda

More by this Author


Dar es Salaam. Katika mkakati wa kubana matumizi, Serikali inatarajia kudhibiti mambo kadhaa ikiwemo ununuzi na matumizi ya magari.


Hayo amebainisha  jana Jumanne Juni 14, 2022 bungeni mjini  Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.


Katika hotuba yake hiyo, Dk Mwigulu amesema watadhibiti matumizi hayo kwa kuzingatia waraka wa rais namba moja wa mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana matumizi ya serikali na waraka wa mkuu wa utumishi wa umma namba mbili  wa mwaka 2021 kuhusu utaratibu wa kutumia usafiri huo.


“Baadhi ya maeneo yenye gharama kubwa sana kwa serikali ni ununuzi wa magari,  mafuta ya uendeshaji,  vipuri na matengenezo,” amesema.


Amesema serikali inapanga kuchukua hatua za muda mfupi na za muda mrefu hivyo  lazima matumizi ya umma na ya watumishi  wote yaakisi ugumu wa maisha wanayopitia wananchi  kufuatia athari za Uviko-19 ili fedha zinazopatikana zifanye mambo muhimu.


“Hatua za muda mfupi zitakazochukuliwa ni kupunguza safari za ndani na nje, kukata fedha za ununuzi usio wa lazima, kupunguza ukubwa wa uwakilishi kwenye mikutano ya ndani na nje, na tutapimiana mafuta ya magari ya Serikali kila mwezi kufuatana na shughuli za lazima,” amesema.


ADVERTISEMENT

Wabunge na BOT watajwa


Katika maelezo yake, Dk Mwigulu amesema utaratibu huo unatumika kwa wabunge na hawajaacha kufanya shughuli majimboni mwao.


"BOT (Benki Kuu) wanapimiwa, baadhi ya taasisi za UN (Umoja wa Mataifa) wanapimiwa. Namwelekeza mlipaji mkuu wa serikali afanye uchambuzi wa wastani wa mahitaji ya mafuta kufuatana na aina ya majukumu, ulazima wa majukumu na ngazi katika utumishi," amesema.


Hatua zaidi


Amebainisha kuwa kwa upande wa hatua za muda wa kati na muda mrefu, anapendekezwa Serikali kubadili kabisa utaratibu uliopo kwa kuwakopesha magari watumishi wenye hadhi ya kuwa na gari la serikali wawe na magari yao wenyewe na wafanye matengenezo wenyewe.


"Wanunue vipuri wenyewe na masuala ya mafuta yaangaliwe kwa utaratibu utakaoonekana unafaa. Kwa sasa Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mitambo 373 na inatumia zaidi ya Sh558.45 bilioni  kwa ajili ya ununuzi wa magari,  mafuta ya uendeshaji, vipuri na matengenezo ambapo kwa sasa ni zaidi ya Sh500 bilioni,”amesema.


Amesema ununuzi wa magari, mafuta ya uendeshaji, vipuri na matengenezo kwa sasa ni zaidi ya Sh500 bilioni kwa mwaka.


Safari za mabosi na madereva


Ameeleza kuwa ukiondoa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mahakama, upande wa serikali wanabaki viongozi wakuu wa wizara, mashirika, wakala, mikoa, wilaya na miradi ambao wasimamizi watakuwa eneo la mradi muda mwingi na kwamba  kwenye makundi haya hawatazidi watano kwa taasisi na wengine wote wenye stahili ya gari la serikali wakopeshwe.


“Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, dereva na gari inapitishwa chini bosi anapanda ndege mpaka Mwanza au Mbeya kutoka Dar es Salaam na kurudi hivyo hivyo. Kuna utafiti wa siri ulifanywa, kwa siku moja yalibainika magari ya Serikali yaliyotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam yalikuwa 132, na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yakipishana kuja Dodoma yalikuwa 76 na mengine nane yalikuwa yamepinduka,” amesema.


Amesema utaratibu huo gharama za matumizi ya magari serikalini zitakuwa zimeokolewa  Sh500 bilioni ambazo zitaelekezwa  kwenye ununuzi wa dawa muhimu hospitali,  kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati na kutekeleza miradi ya maendeleo."


“Tumezidi kupenda ubosi magari makubwa kwa kila mtu serikalini, matumizi ya starehe wakati katika nchi yetu bado kuna watu wanapata shida kupata mlo mmoja," amesema.


Ameongeza kuwa serikali itaachana na mfumo wa sasa wa ununuzi wa umma  ambao umeshindwa kuleta tija kwa kuwa msingi wake mkubwa ni ulinganishaji wa zabuni zilizofunguliwa badala ya bei za bidhaa na huduma ambazo tunazijua.


“Mara nyingi bei hizi za ununuzi zimekuwa kubwa kuliko zile zilizopo sokoni kwa jumla na hata rejareja  na ingekuwa tunanunua kwa ajili ya nyumbani kwetu au kwa ajili ya kampuni zetu tusingekubali bei hizo,” amesema

Share:

Kimeumana... Mkuu wa Mkoa Feki Mikononi Mwa PolisiMtu mmoja Warren Max Mwinuka (20), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kujifanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera.


Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram wenye jina linalosomeka juma_homera.


“Mtuhumiwa Warren alikamatwa Juni 7, 2022 maeneo ya Mama John Jijini Mbeya, na alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa na kutoa namba yake ya simu ili kupokea, kutoa, kupeleka kero na shida mbalimbali,” ilisema taarifa hiyo.


Mtuhumiwa Warren Mwinuka mkazi wa eneo la Makondeko jijii Mbeya anatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Share:

Dr. Mwigulu " Mtanzania Anayefikisha umri wa Miaka Kumi na Nane Anatakiwa Kulipa Kodi"Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kwa kila Mtanzania atayefikisha umri wa miaka kumi na nane kwani atatakiwa kuanza kulipa kodi katika umri huo.


Dr. Mwigulu ameyasema haya leo wakati akiwasilisha Bungeni Dodoma mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 huku akinukuliwa akisema "Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi ambapo ili kutimiza amza hiyo Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"


"Kwakuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi ambapo kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"

Share:

Habari Njema Kidato cha TANO na SITA Sasa Kusoma Bure Tanzania

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ili kuwapunguzia gharama.

Kauli hiyo ameitoa  Jumanne Juni 14, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.


Dk Mwigulu amesema kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani 90,825 na kidato cha sita ni 56,880 na mahitaji ya fedha ni Sh10 3 bilioni.


“Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Rais alivyoielekeza Wizara, napendekeza kufuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, elimu bila ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita,”amesema

Share:

Mwigulu Nchemba "Tumekubaliana Kuongeza Ushuru wa Nywele Bandia"


"Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa
Heading 6704"

"Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali" ——— Dr. Mwigulu
Share:

6/14/2022

Wabunge Ving'ang'anizi wa Taarifa Wakati Wenzao Wanachangia BUNGENI WaonywaVikali

 


Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu, amewaonya wabunge wenye tabia za kuingilia wenzao wanapokuwa wanachangia ama kuuliza maswali na kutaka tabia ya kung'ang'ana na neno taarifa linakoma mara moja kwani wanawatoa kwenye reli wachangiaji.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 13, 2022, wakati akisitisha shughuli za Bunge hadi kesho saa 3:00 asubuhi, na kusema mara baada ya Bajeti Kuu ya serikali hakutakuwa na taarifa zisizo na msingi, kwani taarifa nyingi zimekuwa hazina maana.


"Waheshimiwa wabunge tumeona katika mijadala mbalimbali ndani ya Bunge letu, wabunge wengi tuna tabia ya kusitisha mchangiaji kwa kutoa taarifa na taarifa nyingi hazina msingi mna tabia ya kuharibu flow ya mtu aliyepewa muda mfupi kuchangia mambo ya msingi halafu wewe unasimama taarifa tena unakuwa king'ang'anizi taarifa, taarifa, halafu unasimama unasema hata jimboni kwangu ni hivyo hivyo kanuni zetu haziruhusu,"amesema Naibu Spika

Share:

Wamiliki wa Magari yaliyoua Iringa Wanatafutwa

 


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa, amesema wanaendelea kumtafauta mmiliki wa basi ndogo aina ya Costa pamoja na mmiliki wa lori aina ya Scania yaliyosababisha ajali na kuuwa watu 20 katika eneo la changarawe mjini Mafinga mkoani Iringa.


Kamanda Mutafungwa amesema kwamba wanawatafuta wamiliki hao kwa ajili ya mahojiano pamoja na dereva wa Scania kwani dereva aliyekamatwa ni wa ile gari ndogo.


"Tunamatafuta dereva wa Scania na mmiliki wake, na tunamtafuta mmiliki wa hiyo Costa lazima ahojiwe kwamba ilikuwje akaruhusu gari lake likabeba abiria kwenda Mbeya wakati halina leseni ya usafirishaji wa abiria,"amesema Kamanda Mutafungwa

Share:

Mungu Tusaidie...Mtafaruku Mpya Kanisa la KKKTSIKU chache baada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Konde, Geofrey Mwakihaba, pande mbili zinazohasimiana zimeingia kwenye mtafaruku mpya wa kugombea mali za kanisa.

Mtarafuku huo ulijitokeza juzi wakati wa Ibada ya Jumapili Kanisa la KKKT Ruanda, jijini hapa, mahali alipohamishia makao makuu ya Dayosisi ya Konde, aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo, Dk. Edward Mwaikali.

Hali hiyo ilisababisha Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wa kanisa hilo na kuwasweka mahabusu.

Waliokamatwa katika sakata hilo ni aliyekuwa Mkuu wa Jimbo la Mbeya Mashariki, Nyibuko Mwambola na Dk. Mwaikali, ambao walipelekwa mahabusu wanakoendelea kushikiliwa.

Kabla ya kukamatwa kwa viongozi hao, Mchungaji Mwambola akiwa madhabahuni alitoa taarifa kwa waumini wa kanisa hilo kuhusu uamuzi wao wa kujitenga na Kanisa la KKKT na kujiunga na Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki.


Hata hivyo, muumini mmoja alisimama na kuhoji uhalali wa uamuzi huo, ndipo alipochukuliwa na viongozi hao na kumwingiza kwenye gari na kutaka kuondoka naye kusikojulikana kabla ya mtu huyo kuokolewa na askari wa Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ulrich Matei, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kuwekwa mahabusu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana, Kamanda Matei alisema kwa kifupi kuwa wanawashikilia viongozi hao kwa ajili ya mahojiano zaidi.


“Ni kweli tunawashikilia Mchungaji Mwambola na aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Konde, Dk. Mwaikali kwa mahojiano zaidi, kwa sababu tunatambua kuwa mgogoro wa Dayosisi hiyo ulikwisha baada ya kusimikwa kwa askofu mwingine, lakini inaonekana wao bado wanaendelea na mgogoro huo,” alisema Matei.

Wakati hayo yakijiri, uongozi mpya wa Dayosisi ya Konde chini ya uongozi wa Askofu Mwakihaba, unadaiwa kuwatuma mabaunsa pamoja na madalali wa Mahakama, kufunga ofisi zilizokuwa zikitumiwa na uongozi uliopita wa Dk. Mwaikali zilizopo kwenye Kanisa la Usharika wa Ruanda.

Hatua ya kufungwa kwa ofisi hizo, ilisababisha waumini wa kanisa hilo, hasa wanaoaminika kuwa ni wafuasi watiifu wa Dk. Mwaikali, kukusanyika kuzuia uongozi mpya kufanya shughuli zozote ndani ya kanisa hilo kwa madai kuwa wao bado wanamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wao.

Mvutano huo wa waumini wa KKKT, ulisababisha Jeshi la Polisi kufika kanisani hapo ili kuwatawanya wafuasi wanaoendelea kumtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wao, na kupinga hatua iliyofanywa na viongozi wanaodaiwa kuwa wa askofu mpya kufunga kanisa hilo ili kulinda mali zote za kanisa zisitumiwe na askofu aliyevuliwa madaraka.


Mkuu wa Operesheni ya Jeshi la Polisi Mbeya Mjini, Johanes Bitegeko, aliwaamuru waumini waliozingira kanisa hilo kutawanyika mara moja kwa kile alichoeleza kuwa wanafanya mikusanyiko isiyokuwa rasmi.

Aliwataka waumini hao kuwa watulivu wakisubiri maamuzi kutoka mamlaka husika kutoa maelekezo ya kumaliza mgogoro huo ambao umedumu takribani miaka miwili sasa.

“Mgogoro huu bado unashughulikiwa, nawataka waumini kuwa watulivu, sisi kazi yetu ni moja tu kulinda usalama wa raia na mali zao na nyie mmekusanyika hapa bila sababu ya msingi, ondokeni mkaendelee na shughuli nyingine za uzalishaji mali na mambo mengine ya msingi kwa sababu mgogoro huu hautatuliwi chumbani, maamuzi yatakapotolewa kila mtu atajua na huduma zitaendelea, tunaomba muondoke,” aliamuru afande Bitegeko.

Dalali wa Kampuni ya Pamoja Auction Mart, aliyehusika kulifunga kanisa hilo, Lwitiko Mwamaso, alisema uongozi mpya chini ya Askofu Geofrey Mwakihaba, ulimwagiza kwenda kufunga ofisi za kanisa hilo, baada ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Mwaikali kutangaza Usharika wa Ruanda kujiunga na Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki.


Alisema tayari kanisa hilo limejiunga na kanisa jipya na kuamua kubadilisha bango kutoka Kanisa la Kuu la KKKT Dayosisi ya Konde Ruanda na kuweka linalosomeka ‘Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki’.

Emmanuel Mwaisanga, kutoka Usharika wa Sinai jijini Mbeya, alisema ameshtushwa kuona usharika wa Ruanda umejitenga na kuanzisha kanisa lao na kwamba hawako tayari kuona ushirika huo unajitenga kwa sababu ni watoto wa baba mmoja.

“Hakuna mtu atakayesimama na kusema amejenga usharika huo wa Ruanda bali kila mwana KKKT kote nchini alishiriki aidha kwa sadaka au njia nyingine kujenga, sio sawa waumini hao kuanza kujimilikisha kanisa hilo na kudai ni mali yao na kuanzisha kanisa lao,” alisema Mwaisanga.
Share:

6/13/2022

Vitambilulisho vya NIDA Vitakavyo Isha Muda Kulipiwa Elfu 20Vitambulisho vya Taifa vilivyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), 2013 vitaisha muda wake mwakani 2023 ambapo gharama za kupatiwa Kitambulisho kipya dhidi ya kilichopotea au kuharibika ni Shilingi 20,000 kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya NIDA usajili wa awali unaonesha hauna tozo, ingawa hofu ya Wananchi wengi ni juu ya utaratibu wa upatikanaji wa vitambulisho hivyo wa jinsi vinavyochukua muda mrefu pasipo uhakika wa kukipata.

“Japo hali ni ngumu lakini itatulazimu kulipia hiyo pesa hakuna jinsi lakini hofu yangu ni kuhusu upatikanaji wake umekuwa ni mgumu sana hata sijui wanakwama wapi,” alisema mmoja wa wananchi Martha Mbuto mkazi wa Makole Jijini Dodoma.

NIDA kupitia tovutu yake inaonesha gharama za kupata kitambulisho kipya kwa awamu ya pili dhidi ya kilichopotea, kuharibika au kuharibiwa ni Shilingi 30,000 kwa awamu ya pili na 50,000 kwa awamu ya tatu na zaidi.


Juni 8, 2022, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema vitambulisho vya Taifa vipo mbioni kutolewa baada ya kukamilika kwa mchakato wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kampuni ya utengenezaji wa kadi hizo.

Masauni aliyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Biharamuro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na kuelezea malalamiko ya Wananchi juu ya kukosekana kwa vitamabulisho hivyo kwa mchakato wake kuchukua muda mrefu.

“Wananchi wamekuwa wakilalamika sana na hasa maeneo ya mipakani lakini jitihada za Rais zinaonekana kwani ametupatia pesa ili kukamilisha vitambulisho, na tayari NIDA imesaini mikataba na kampuni yenye tenda ya utengenezaji wa kadi hizo,” amesema Masauni.


Alisema Wizara itahakikisha jambo hilo linamalizika kwa ufanisi baada ya Rais Samia kutoa Shilingi Bilioni 42.5 za kununua kadi ghafi zitakazokamilisha zoezi la utengenezwaji na ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Share:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger