6/22/2022

Msanii k2ga Kwenye Penzi Zito na Mwigizaji Love wa Jua Kali


Kwa haraka haraka si rahisi kuhisi msanii wa Bongo Flava angemtumia @love_juakali kama video Vixen kwenye wimbo wake, Si kwa ubaya, ila tumekariri kuona models wengi kama video vixens, au hata kama ni mnene basi awe amechora namba 8. Imekuwa tofauti kwa mchizi wa UK tokea familia ya wafalme, Kings Music, @k2ga_tz ambaye amemchukua mtoto mzuri Love Juakali na kumtuliza kwenye kichupa chake kipya cha RANGI RANGI na kitu kikawa lit.


Hadi sasa ngoma hiyo ipo No.15 kwenye Trending Tab ya YouTube Tanzania ikiwa na masaa 18 na zaidi ya views 88k.


Rangi Rangi link kwa bio ya mchizi wa UK, K2ga

Share:

Basi la Shule ya Msingi Samuu laua Mwanafunzi Wake Shinyinga Mjini
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Dereva wa gari la shule ya Msingi Samuu, Kassim Said Mahona (40) kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo Godlight Chisawilo (04) kwa kumgonga na gari la shule hiyo Mjini Shinyanga.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema mwanafunzi huyo amegongwa na gari hilo baada ya kushushwa na gari hilo akitokea shuleni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando tukio hilo limetokea Jumanne Juni 21,2022 majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga.

“Gari lenye namba za usajili T.151 DAG Toyota Coastar mali ya Malatia wa Shinyanga likitokea shule ya msingi Samuu kuelekea Majengo Mapya likiendeshwa na dereva aitwaye Kassim Said Mahona (40) na mkazi wa Nguzo Nane Shinyanga, lilimgonga mtembea kwa miguu Godlight Chisawilo (04) mwanafunzi wa shule ya chekechea Samuu na kumsababisha kifo chake”,ameeleza Kamanda Kyando.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na tayari mtuhumiwa amekamatwa.
Share:

Ajali ya Treni ya Abiria Leo Tabora...Mabehewa Yaanguka
Mabehewa sita ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora mpaka Dar es salaam yameanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi linaendelea kufuatilia kutokana na abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.

Share:

Kocha Nabi Avutiwa na SIMON Msuva


SIMON Msuva yupo nchini tangu mwaka jana baada ya kuzinguana na timu yake ya Wydad Casablanca ya Morocco na kupelekana Fifa, ila juzi alifunga mabao mawili kwenye mechi ya hisani ya timu Samakiba na kuiwezesha team Kiba kubeba ubingwa wa msimu huu kwa penalti.

Kumbe, kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alikuwa akimfuatilia dakika zote za mchezo zilizoisha kwa sare ya mabao 3-3, kisha kupigiana penalti na kuweka wazi kuwa kama kuna jina la mchezaji mzawa limesalia kikosi chake ni Msuva anayetamani awe naye.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi alisema anatamani kuongeza mshambuliaji mmoja mzawa, lakini kiu ni kuwa na staa huyo aliyewahi kukipiga na kung’ara na Yanga kabla ya kutimkia Difaa El Jadida ya Morocco kisha Wydad.

Nabi alisema anatambua Msuva ana mgogoro na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, lakini kama mabosi wake wanaosimamia usajili watamfungia kazi wanaweza kunasa saini yake.

“Nahitaji mshambuliaji mwenye kujua kufunga na kasi. Nipo hapa Tanzania kuna wakati ni jambo zuri kuendeleza wachezaji wa taifa hili. Natamani sana kufanya kazi na yule Msuva (Simon),” alisema Nabi.

“Msuva ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa. Napenda sana kasi yake, juhudi zake lakini kitu bora zaidi anaweza kufunga na kucheza nafasi nyingi. Nitafurahi viongozi wangu wakimpata.

“Sisi ni mabingwa sasa hapa Tanzania, tunakwenda kucheza mashindano ambayo kila mchezaji mkubwa angetamani kucheza, kwasasa najua Msuva ana shida na klabu yake, najua yataisha ila wakati huu ni kitu kizuri angekuja hapa Yanga aweze kupambana kujiweka sawa, atalisaidia taifa lake na hata sisi tutapata kitu.”

Nabi alisema anafahamu Msuva ana ndoto za kwenda kucheza soka nje, ila kama atakubaliana na mabosi wa Yanga atamruhusu wakati wowote kwenda kucheza.

“Nilimuona (Msuva) alikuja kwenye vyumba vyetu siku ambayo tuliwafunga Coastal Union. Sote tulifurahia kumuona wachezaji, makocha na viongozi alionyesha kuiheshimu hii klabu na kwamba anatambua alipita hapa na waliishi vizuri,” alisema.

“Kama atakuja hapa tunaweza kumpa mkataba mfupi ambao utamruhusu kuondoka wakati wowote akitaka kuondoka.” Kwa sasa Msuva anajifua na kikosi cha kituo cha soka cha vijana cha Cambiasso baada ya kuwa na mgogoro na timu yake ya Wydad ambao kesi yao ipo Fifa.

Share:

Mrembo Maarufu Kwenye Mitandao Poshy Queen Akana Kutengeneza Shepu Yake MatataPoshy Queen; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye amekuwa akizungumziwa mno juu ya kutengeneza shepu matata aliyonayo, lakini mwenye anasema hajawahi kufanya jambo kama hiyo.


Poshy Queenn anasema kuwa umbo lake matata (kiuno cha nyigu) linatokana na asili ya familia yake kwani hata mama yake ana shepu kuliko hata yeye.


Kwa baadhi ya watu wanaojua familia ya Poshy Queen ambao ni wenyeji wa jijini Mbeya wanasema ni kweli ni asili yao kwani ndugu zake nao wamejaaliwa shepu kama ilivyo kwa wanawake walio wengi kutoka jijini Mbeya.


STOLI: SIFAE LPAUL

Share:

Chris Brown “Msinilinganishe na Michael Jackson”

 


Mwanamuziki Chris Brown, ameendelea kuonyesha kutoridhishwa na kundi la mashabiki pamoja na wadau wanaolinganisha umahiri wake kwenye tasnia na ule wa nguli wa Pop Hayati, Michael Jackson huku wengine wakimtaja kama msanii bora zaidi yake.


Kufuatia kukithiri kwa aina hiyo ya maoni ya watu juu ya kumlinganisha Chris Brown na Michael Jackson, mwanamuziki huyo ameamua kuvunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa hapendezwi na aina hiyo ya maoni kutoka kwa mashabiki na wadau mbali mbali.


Breezy amesema maoni hayo ni sawa na upuuzi, likiwa ni jibu baada ya kuulizwa ni kwa namna gani huwa nachukulia suala hilo wakati akiwa kwenye mahojiano maalum na Big Boy Tv.


“Huwa najiweka mbali na mada hiyo, Maoni yangu kwenye hilo huwa ni kwamba nisingeweza hata kupumua au hata kuwa na uwezo wa kuimba kama huyu jamaa ‘Michael Jackson’ asingetokea duniani, yuko mbali sana, hakuna ushindani na yeye.” amesema Chris brown

Share:

Mgambo, ofisa mtendaji wadaiwa kuua mwanafunziMoshi/Siha. Ofisa mtendaji katika kata moja wilayani Siha mkoani Kilimanjaro na mgambo, wanadaiwa kuwatembezea kipigo wanafunzi wanne na kusababisha kifo cha mmoja wao anayesoma kidato cha pili.

Marehemu ambaye ametajwa kuwa ni Bright Arnold (14) na wanafunzi wenzake watatu wa shule ya sekondari Fuka wilayani Siha, wanadaiwa kupigwa ndani ya ofisi ya mtendaji huyo wa kata wakituhumiwa kuiba viatu.

Taarifa za mashuhuda zinaeleza wanafunzi hao walifungiwa katika ofisi ya mtendaji huyo hadi wananchi walipoingilia kati lakini wakati huo marehemu alikuwa hawezi kutembea na baadaye kupoteza fahamu.

Aliwahishwa hospitali ya Rufaa ya KCMC, lakini akafariki saa chache baadaye.


 
Ndugu, mashuhuda wafunguka

Akizungumza na Mwananchi, Ruth Munuo ambaye ni mama mkubwa wa marehemu alidai siku ya tukio Juni 17, 2022 akiwa anatoka kwenye shughuli zake, alipata taarifa za mwanawe huyo kuchukuliwa na mgambo na kupelekwa ofisi ya kata.

“Walimchukua wakidai ameiba raba na alikiri kuzichukua na kuonyesha zilipo, lakini walimpiga wakimtaka aonyeshe wenzake, kwa kweli alipigwa kipigo ambacho hakustahili mtoto hata kama alikuwa na makosa,”alidai.

Aliongeza: “Jambo la kusikitisha ni kwamba tukio hili lilifanyika katika ofisi ya kata ambako tunajua ndiko kimbilio letu wanyonge, na nilipofika nilimkuta amevimba kila mahali na ana hali mbaya sana.’’


Kwa upande wake, Elisifa Mrang’u ambaye ni shangazi wa marehemu, alidai siku hiyo saa 5 asubuhi, alielezwa kuwa kuna kijana aliyekuwa ameongozana na mgambo wa kata, walimchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka ofisi za kata akidaiwa kuiba viatu.

“Nikiwa sielewi chochote kwenye saa 11:00 jioni nilipita ofisi hizo, nikawaona watu na wanafunzi wakichungulia dirishani na mlangoni, nikauliza kuna nini nikaambiwa kuna wanafunzi wameiba wanapigwa.”

“Nikaambiwa alipoulizwa alikiri na alimtaja mtu aliyekuwa navyo, lakini kaniambia mgambo hao waliendelea kumpiga na kumtaka ataje vitu vingine walivyoiba na watoto wengine wanaoshirikiana huku wakiendelea kumpiga.”

Alidai kuwa aliamua kusogea kuangalia akamuona mtoto wao (marehemu) akipigwa na mgambo wawili na mtendaji kata wakitumia marungu na mateke.


 
‘‘Ni tukio nililolishuhudia mwenyewe.Nilishuhudia akipigwa na walikuwa watoto wanne...,’’ alisema.

Baada ya kichapo

Alidai walipotoka nje watoto watatu waliweza kusimama, lakini Bright hakuweza kusimama kabisa kwa kuwa alikuwa ameumizwa sana kwenye magoti na kichwani.

Alibebwa na wananchi na kukimbizwa hospitali Kibong’oto kwa pikipiki,”alidai ndugu huyo.

Inadaiwa baadaye hali yake ilizidi kuwa mbaya akahamishiwa Hospitali ya KCMC na kesho yake alifariki dunia na kusema, tukio hilo limemuumiza sana maana wangeweza kumpeleka kwenye vyombo vya sheria kama amefanya kosa.


Naye mjomba wa Marehemu, aitwaye Baltazary Mmary alilaani kitendo hicho na kueleza kuwa ni tukio la kikatili na kinyama na linapaswa kukemewa na vyombo vyenye mamlaka ili kuepusha tena tukio kama hilo kutokea.

Kauli ya viongozi Siha

Juni 17, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alikaririwa akisema ofisa mtendaji pamoja na mgambo, walikuwa wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwapiga watu kadhaa na kusababisha Bright kulazwa KCMC.

Lakini jana na juzi alipotafutwa ili kuzungumzia kifo cha Bright aliyekuwa amelazwa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kuwa amefariki, simu yake iliita bila majibu na wakati mwingine kupokelewa na mlinzi wake.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Thomas Apson alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kusema bado hajapata taarifa kamili kuhusiana na kilichotokea na kuomba kupewa muda ili kulifuatilia kwa karibu na kubaini chanzo cha kifo hicho.

“Kifo hiki kinauma nami nimeumia sana, lakini kifo hiki kina mambo mengi, na sijapata taarifa sahihi wala taarifa ya daktari inayoeleza chanzo chake. Naomba muda nilifuatilie niweze kupata taarifa sahihi,”alisema mkuu huyo wa wilaya.


Mwananchi
Share:

Kilimanjaro: Mwanamke auawa na temboSaumu Hassan mwenye umri wa miaka 32, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo akiwa shambani katika kitongoji cha kijiweni wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea farehe 19 mwezi huu majira ya asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa shambani akichimba viazi.

Amesema mwanamke huyo alikutwa amefariki dunia baada ya kujeruhiwa na tembo, ambapo alipata majeraha makubwa kwenye mwili wake.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Maigwa ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapokwenda shambani, hasa wale ambao wamepakana na hifadhi.
Share:

Mamelodi Sundowns yaiita Simba SC Afrika KusiniMabingwa wa Soka Afrika Kusini Klabu ya Mamelodi Sundowns wamepangwa kuialika Simba SC katika michuano maalum ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/23.

Mamelodi Sundowns imepanga kuzialika timu tatu kutoka nje ya Afrika Kusini, ambazo zitatoa ushindani wa kweli kwenye michuano hiyo itakayopigwa kwa juma moja.

Kwa mujibu wa Meneja mawasiliano wa klabu ya Mamelodi Sundowns Shupi Nkgadima amesema maandalizi ya michuano hiyo yanakwenda vizuri na wanaamini yatazisaidia timu shiriki kwa ajili ya msimu ujao.

Klabu nyingine zinazotajwa kuwa kwenye mpango wa kualikwa ni Mabingwa mara tano wa Afrika TP Mazembe kutoka DR Congo na Al Hilal ya Sudan. Michuano hiyo inatarajia kuanza rasmi Julai 29.


 
Simba SC imewahi kuandaa michuano kama hiyo (Simba Super Cup) iliyochezwa mapema Mwaka 2021 jijini Dar es salaam, huku timu za TP Mazembe na Al Hilal zikialikwa.
Share:

Rais Samia Ashusha Bei Ya Maji Vijijini

Wizara ya maji imetangaza Rasmi Bei elekezi za Gharama za Maji vijijini na kufanya uchambuzi wa Bei za Maji kwenye Vyombo vya watoa huduma za Maji ngazi ya Jamii na kuzionya jumuiya za maji kuzingatia maelekezo hayo kwani haitawafumbia macho watakaokwenda kinyume.

Waziri wa Maji Juma Aweso ameziweka wazi bei za kikomo kwa ndoo ya lita 20 kama ifuatavyo ikiendana na mifumo/nishati inayotumika kusukuma Maji ambapo Mfumo wa Nishati ya mafuta ndoo ya lita 20 ni shillingi 50, Mfumo/Nishati ya Umeme Jua shillingi 30, Mserereko Shillingi 20 Umeme wa Tanesco shillingi 40 na Pampu za mkono Bei iwe shillingi 20.


Amesema Bei za Ukomo kwa mita ya ujazo itakua shillingi 2,500/= kutoka shillingi 5,000/= ilivyokua na hivyo Bei za ukomo kwa ndoo ya lita 20 itakua shillingi 50 badala ya shillingi 100 ya awali.


Awali amesisitiza kuwa hii ni dhamira ya dhati ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kazi ya Wizara ni kutekeleza maono hayo kwa kuwapunguzia mzigo wanancho vijijini.


Pia Aweso ametoa vifaa vitakavyotumika katika utendaji kazi ikiwa ni pikipiki 250 kuongeza kwenye 145 zilizokwisha kugawiwa awali mwaka jana ikiwa ni jumla ya 395 kwenda kuboresha utendaji kazi, ufuatiliaji, usimamizi na utekelezaji wa majukumu sekta ya maji vijijini

Share:

Mwenyekiti Wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya CCM

 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mpinduzi ( CCM ) kilichokutana  tarehe 21 Juni 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Share:

HESLB Yaanza Kuwadai Shilingi 10.6 Bilioni Waliokopeshwa Law School Of Tanzania


 

HESLB imesaini mkataba wa makubaliano na Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania), kuanza kudai wanasheria walionufaika na  mikopo, Juni 21,2022.

Wanasheria 5,025 waliokopeshwa zaidi ya Shilingi Bilioni 10.6 kama mikopo wakiwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria Tanzania Tanzania (Law School of Tanzania -LST) watapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).


Akizungumza wakati wakisaini mkataba wa makubaliano hayo  Juni 21, 2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw.Abdul-Razaq Badru amesema kuwa Bodi hiyo imekuwa na uzoefu na utayari wa kutekeleza jukumu hilo na kuwakumbusha wanufaika hao kujitokeza na kurejesha.


“Tumejipanga kuanza kuwahudumia kuanzia Julai 1,2022 hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu hawa kurejesha fedha hizi pamoja na zile walizokopeshwa wakiwa wanafunzi wa shahada za kwanza ili ziwanufaishe vijana wengine wa kitanzania wanaohitaji”. Amesema Bw.Badru.


Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud amesema wanasheria hao ni wale walionufaika na mikopo ya elimu wakiwa wanafunzi wa LST kati ya mwaka 2008 na 2015 wakisoma Stashahada ya Juu ya Uanasheria kwa Vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) wakati Sheria ya HESLB ilipokuwa hairuhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa.


“Tunashukuru kuwa mikataba waliosaini walipokuwa wanafunzi -wanasheria ipo wazi kuwa LST inaweza kuipa kazi ya kukusanya madeni haya taasisi yoyote ya umma au binafsi  na hivyo basi baada ya mazungumzo tangu 2019, leo tumefikia hatua hii”. Amesema Jaji Dkt.Benhajj Masoud


HESLB ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na majukumu makuu mawili, kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa elimu ya juu na pia kukusanya fedha za mikopo zilizoiva ambazo zimetolewa na Serikali kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994/1995

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo June 22

 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo June 22


Share:

6/21/2022

Samaki mkubwa zaidi duniani wa maji baridi avuliwa MekongSamaki mwenye uzani wa kilo 300 (lb 661) aliyevuliwa katika mto Mekong nchini Cambodia ndiye samaki mkubwa zaidi wa maji baridi kuwahi kurekodiwa, wanasayansi wanasema.

Samaki huyo (stingray) amempiku mwenye rekodi ya awali, samaki aina ya kambare mwenye uzito wa 646lb (293kg) aliyevuliwa nchini Thailand mwaka wa 2005.

"Katika miaka 20 ya kutafiti samaki wakubwa katika mito na maziwa katika mabara sita, huyu ndiye samaki mkubwa zaidi wa maji baridi ambaye tumewahi kukutana nao au ambaye amerekodiwa mahali popote ulimwenguni," Zeb Hogan, mwanabiolojia katika mradi wa uhifadhi unaofadhiliwa.

Hakuna uwekaji rekodi rasmi au hifadhidata ya samaki wakubwa zaidi wa maji baridi duniani.


 
"Kupata na kuweka kumbukumbu za samaki huyu ni jambo la kushangaza, na ni ishara chanya adimu ya matumaini, hata zaidi kwa sababu imetokea katika Mekong, mto ambao kwa sasa unakabiliwa na changamoto nyingi," aliongeza Dk Hogan.

Mradi wa uhifadhi unafanya kazi na Utawala wa Uvuvi wa Cambodia kuanzisha mtandao wa wavuvi ambao huwatahadharisha watafiti iwapo watakamata samaki wakubwa au walio hatarini kutoweka.

Stringray kubwa ya maji baridi ni spishi iliyo hatarini kutoweka. Huyu ni stingray wa pili kuchunguzwa na timu hiyo tangu Mei - yule wa awali alikuwa na uzito wa kilo 181.
Share:

Mwanafunzi darasa la saba auawa, adaiwa kunyofolewa macho 
Geita. Mtoto Johnson Thomas (14) mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Buhalahala mjini Geita amekutwa amefariki dunia na mwili wake kutupwa pembeni ya mto karibu na Barabara ya Buhalahala kwenda Kijiji cha Nyakato.

Tukio la mtoto huyo kuuawa ni tukio la tatu ndani ya wiki mbili ambapo watoto wengine wawili mmoja akiwa na miaka miwili aliuawa kwa kukatwa shingo na mwingine wa miaka saba inadaiwa alilawitiwa na kubakwa kisha kukatwa shingo wilayani Nyang’hwale mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea Juni 18 saa 11 jioni katika Kijiji cha Buhalahala.

Amesema mtoto huyo alitoka nyumbani kwao Juni 12 kwa usafiri wa bajajaji akielekea Buhalahala kushona sare za shule na mara ya mwisho alionekana na mwanafunzi mwenzake akielekea barabara inayokwenda ofisi za GPH. Tangu siku hiyo hakurejea mpaka mwili wake ulipopatikana Juni 18.


 
Kamanda amesema mwili huo umekutwa na majeraha mguu wa kushoto kama ulipondwa na kitu kizito ambacho hakijafahamika.

Naye msemaji wa familia ya mtoto huyo, Theophil Mkwata amesema mwili huo umekutwa unyayo umekatwa na jicho  kunyofolewa.

Kwa mujibu wa Kamanda uchunguzi uliofanyika umebaini unyayo ulikuwa umepondekapondeka na jicho kuumia.


Hadi sasa hakuna aliyekamatwa na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.


Share:

Waendesha boda boda Kahama kuchoma moto Gari lililosababisha ajariNa Victoria Robert , Kahama
Waendesha bodaboda pamoja na wananchi wenye hasira kali wamedaiwa kuchoma moto gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 975 DHH na kusababisha uharibifu mkubwa wa gari hilo kuteketea kwa moto.
Hatua ya boda boda hao pamoja na wananchi ya kuteketeza gari hilo kwa moto imekuja baada ya mwenzao aliyefahamika kwa jina la Hiali Mgina (38) mkazi wa mtaa wa majengo wilayani humo kugongwa
Share:

Gigy Money afunguka kulishana cake mdomoni na Wema

 


Gigy Money amejibu kuhusu gumzo lake la kulishana cake mdomoni na baadhi ya mastaa walio-show love kwenye 'Birthday Party' yake kama Wema Sepetu, Lulu Diva, Amber Lulu na Mimi Mars.

Gigy Money amesema amefanya hivyo kwa sababu stick zilikuwa zimeisha pia kitendo hicho ni ishara ya upendo

Share:

Simba SC yakanusha uvumi wa Bernard Morrison

 


Uongozi wa Simba SC umesema hauna taarifa zozote kuhusu Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison kuwasilisha ombi la kutaka Barua ya Kumuachia (Release Letter), ili kumpa nafasi ya kuendelea na Maisha yake ya soka nje ya klabu hiyo ya Mismbazi.


Mwezi uliopita, Morrison alipewa ruhusa ya mapumziko na Uongozi wa Simba SC hadi mwishoni mwa msimu huu, kwa madai ya kwenda kumaliza matatizo yake ya kifamilia nchini kwao Ghana.


Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Magungu amesema, hawana taarifa za mchezaji huyo kuwasilisha ombi la kutaka Barua ya Kuachiwa, na wanashangazwa kuona taarifa hizo zikisambaa kwa kasi kubwa katika Mitandao ya Kijamii.


Mangungu amesema Simba SC inafahamu bado Morrison ni mchezaji wao halali, na hakuna mahala popote ambapo klabu hiyo iliwahi kuthibitisha imeachana naye.


“Morrison bado ni mchezaji wa Simba SC, tunashangazwa kuona taarifa za kutuomba Barua ya Kumuachia (Release Letter), tulimpa ruhusa ya kwenda kwao kwa ajili ya matatizo ya kifamilia,”


“Mkataba na Morrison na Simba SC bado haujakwisha, anaendelea kupata stahiki zake kama mtumishi mwingine wa klabu hii, hatujawahi kutoa taarifa popote kwamba hatutaendelea naye, na hatuna taarifa zozote za yeye kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa na klabu nyingine.” Amesema Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu.


Mapema leo Jumanne (Juni 21) asubuhi, Mwandishi na Mchambuzi wa Michezo kupitia kituo cha Radio Clouds FM Shaffih Dauda alinukuliwa akisema: “Bernard Morrison anaomba release letter kwa Simba, lakini Simba hawana presha wanataka mpaka mkataba wake utamatike kisha wamkabidhi barua


Inasemekana kuna muda aliwaambia kuna klabu ya nje inamtaka, Simba wakamwambia watume offer yao watapokea ofa na watampa release letter


Taarifa za kuaminika ni kuwa anataka kujiunga na Yanga, Simba wanafahamu hilo kwahiyo hawana tatizo zaidi ya kusubiri mwisho wa mkataba”

Share:

Barbara "Simba SC Haijafeli Usajili, Tulieni Mtaona"

 


Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez amesema hadi sasa klabu hiyo imeshindwa kuipata saini ya mchezaji Victorien Adebayor aliyekua anaitumikia klabu ya USGN ya nchini Niger.


Simba SC ilijihusisha na usajili wa Mshambuliaji huyo, baada ya kuridhishwa na uwezo wake aliouonesha kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2021/22.


Barbara amesema hadi sasa Simba SC haijafeli katika usajili wa mchezaji yoyote waliyemdhamiria kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, zaidi ya Adebayor anayedaiwa kutua kwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane.


“Kumekua na taarifa nyingi kuwa tumeshindwa kuwasajili wachezaji kadhaa, sio kweli hata kidogo, tunakiri kumkosa Adebayor pekee yake, lakini kwa wengine ambao tumewadhamia tupo katika hatua nzuri za kuwasajili na watacheza Simba SC msimu ujao.”


“Simba SC inatajwa sana kwa sababu mawakala wengi wanaitumia klabu yetu kuwapandisha thamani wachezaji wao, lakini nikwambie tu tupo makini na tumeshalifahamu hilo, tunasajili kimya kimya.”


“Muda utakapofika tutawatangaza wachezaji tuliowasajili kwa ajili ya klabu yetu, Mashabiki na Wanachama waendelee kuwa watulivu, Uongozi wao upo kazini na utakamilisha kila hatua iliyoidhamiria katika usajili.” Amesema Barbara.


Simba SC imedhamiria kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, baada ya kushindwa kufikia lengo msimu huu 2021/22, huku ikipoteza mataji yote ya Tanzania Bara.

Share:

Zari Amzidi Kibenteni Wake Miaka 25, Wafuasi Wake Wampinga, Awajibu Kuwa…

Mwanamama tajiri Afrika Mashariki, raia wa Uganda mwenye maskani yake Durban nchini, Zari akiwa akiwa na mpenzi wake.
Zari The Boss Lady; ni mwanamama tajiri Afrika Mashariki, raia wa Uganda mwenye maskani yake Durban nchini Afrika Kusini na baby mama wa staa wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi, kwa sasa ana mpenzi mpya ambaye ni mdogo mno kiumri almaarfu kibenteni.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya burudani nchini Uganda, Zari mwenye umri wa miaka 41 (amezaliwa Septemba 23, 1980) anatoka kimapenzi na mvulana ambaye yeye (Zari) amemzidi kwa zaidi ya miaka 25.

Inasemekana mvulana huyo ni mkubwa kuliko mtoto wa kwanza wa Zari ambaye ni Pinto Ssemwanga.


 
Baadhi ya wafuasi wa Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram waliojaribu kupingana na maamuzi yake hayo ya kutembea na watoto wenye umri sawa na watoto wake wa kuwazaa, Zari aliwajibu kuwa yuko tayari kutembea na mtoto mwenye umri sawa na mtoto wake wa mwisho ilimradi tu awe na uwezo wa kukidhi haja zake za kimahusiano.

Kumbuka kuwa mtoto wa Zari wa mwisho kwa sasa ni Prince Nillan ambaye hajafikisha hata umri wa miaka kumi hivyo ishu hiyo imeibua mjadala kama wote.

Zari amekuwa na mwanaume huyo miezi kadhaa baada ya kutengana na kibenteni mwingine aliyetambulika kwa jina GK Chopa.
Share:

Yanga Yashauriwa Kutoa Milioni 20 Kukamilisha Usajili wa Morrison Kutoka Simba SCMCHAMBUZI wa soka nchini kupitia kipindi cha Krosi Dongo cha Global TV ameushauri uongozi wa Yanga kufanya mazungumzo na uongozi wa Simba ili kutafuta namna ya kukamilisha dili la kumsajili kiungo mshambuliaji raia wa Ghana Bernard Morrison.

Simba SC ilitangaza kumpa mapumziko mchezaji wake Bernard Morrison hadi mwisho wa msimu huku pia ikimtakia mafanikio mema na kumshukuru kwa mchango wake ndani ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmed Ally ni kwamba Morrison ana mkataba na klabu hiyo unaotarajiwa kumalizika mwezi Agosti hivyo kama kuna klabu yoyote ile inahitaji huduma ya Morrison ni wazi italazimika kuingia katika meza ya mazungumzo na klabu ya Simba au isubiri hadi kutamatika kwa mkataba wake.


Jembe ameishauri Yanga kutoa Milioni 20 kumsajili Bernard Morrison kutoka Simba SC
Kupitia kipindi cha Krosi Dongo Saleh Jembe amesema:

“Yanga wanaweza kusema sisi tunaweza kumkosa lakini hata nyie baada ya mwezi mmoja atakuwa siyo wenu kwahiyo mnaonaje kama mkichukua hata milioni 20 halafu mkatuachia sisi tukamuwahi ili tuweze kumuingiza kimataifa, Ingekuwa hizi klabu zinaweza kuwa na mazungumzo mazuri yenye maelewano hakuna haya mambo ya machagizo ya kuzifanya timu zionekane zina uadui na nini, ingeweza kuwa ni jambo rahisi sana kwasababu ukiangalia Simba haiwezi kuwa naye ndani ya mwezi mmoja.”


Bernard Morrison mchezaji wa Simba SC
Simba na Yanga zote zinaendelea na harakatai zao za usajili ili kuimarisha vikosi vyao ambapo kwa Yanga tayari imeshamtambulisha mshambuliaji raia wa Zambia Lazarous Kambole aliyetokea klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini huku Simba nao wakimtambulisha pia Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zambia Moses Phiri kutoka klabu ya Zanaco ya nchini humo

Share:

Ole Sabaya Aivaa Takukuru Akisema ‘Gerezani si Pikiniki’
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania,Lengai Ole Sabaya amecharuka mahakamani na kudai mashtaka dhidi yake ni ya uonevu ndiyo maana upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi ili kesi hiyo ianze kusikilizwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka saba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro yakiwemo kuunda genge la uhalifu, rushwa na utakatishaji fedha.

Alitoa shutuma hizo jana Jumatatu tarehe 20 Juni 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Hatua hiyo ya Sabaya kuja juu ilitokana na mawakili wa upande wa mashtaka kuomba muda zaidi kwa kile walichodai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika wakati 1 Juni 2022 walidai upelelezi umekamilika na kuomba ahirisho fupi kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya awali ya makosa yao.


Sabaya alidai mahakamni hapo kuwa huko magereza siyo sehemu nzuri na hawaendi pikiniki hivyo upande wa mashtaka kuendelea kudai upepelezi haujakamilika ni kuendelea kuwatesa bure.

“Mheshimiwa naendelea kusisitiza kesi hii ni ya uonevu, leo mimi nafanyiwa hivi na ni mtumishi wa umma je hao ambao siyo watumishi wa umma ni wangapi wanaofanyiwa haya? Ikumbukwe mheshimiwa tulitolewa gerezani usiku katika mazingira ya kutisha,” alisema Sabaya

Alidai wanaomshitaki huku akiitaja Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wanajua mashitaka hayo ni ya kutengeneza ndiyo maana kila mara wanadia upelekezi haujamalika kwa sababu hawana ushahidi ni kile wanachomshitaki nacho.


Kesi hiyo ilikuja tena kwa mara ya tatu ambako wakili wa serikali, Velediana Mleza aliomba ahirisho la siku 14 kwa madia upelelezi haujakamilika hali ambayo iliwalazimu mawakili wa upande wa utetezi kuja juu.

Mawakili hao Hellen Mahuna na Hekima Mwasipu wadai 1 Juni 2022 upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba ahirisho fupi ili kuwasilisha nyaraka za kuipa mamlaka mahakama ya hakimu mkazi kuanza kusikiliza shauri hilo na kuwasomea washitakiwa maelezo ya awali ya kosa.

Waliutaka upande wa mashitaka kuwa makini na kile wanachowasilisha mahakamani kwani wateja wao wanahitaji kutendewa haki huku pia wakiendelea kusisitiza mshitakiwa wa kwanza, Lengai Ole Sabaya ni mgonjwa.


Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Hakimu Mshasha alikubaliana na hoja za upande wa utetezi na kuutaka upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi huo na kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 4 Julai 2022 itakapotajwa tena.


Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine ni, Silivester Nyegu, John Aweeyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, shitaka la kwanza ni la kuunda genge la uharifu shitaka linalowahusu washitakiwa wote ambako Februari 2021, Sabaya akiwa mtumishi wa umma kama mkuu wa wilaya ya Hai alikiuka majukumu yake ya kiutendaji kwa makusudi na kwa nia ya kutekeleza jinai walijipatia Sh.30 milioni.

Shitaka la pili lilimhusu Sabaya peke yake ambako anadaiwa Februari 2021 wilayani Hai kwa nia ya kutenda kosa alishawishi na kudai rushwa ya Sh.30 milioni kutoka kwa Godbless Swai na tarehe hiyo hiyo alijipatisa Sh.30 milioni kama rushwa kutoka kwa Elibariki Swai kwa nia ya kuzuia taaarifa za kiuchunguzi kuhusiana na ukwepaji wa kodi.
Shitaka la tatu na la nne liliwahusu washitakiwa wanne, Silvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey ambao wanadiawa kwa pamoja kuwa mnamo Februari 2021 huko wilaya ya Hai walisaidia kutendeka kwa jina.

Wanadaiwa katika tarehe hiyo washitakiwa hao walimsaidia Sabaya kuweza kushawishi na kumsaidia kupata Sh.30 milioni kutoka kwa Alex Swai huku pia wakidaiwa kumsaidia Sabaya kujipatia manufaa asiyostahili kwa kujipatia Sh.30 miliuoni kutoka kwa Alex Swai.

Sabaya pia anadaiwa katika shitaka la sita linalomhusu yeye mwenyewe kuwa alitenda kinyume na na mamlaka yake kwa kutumia nafasi yake kama mkuu wa wilaya kwamba alinajisi nafasi yake ya mkuu wa wilaya kwa kuanzisha mashitaka dhidi ya Alex Swai kuwa amekwepa kodi na kujipatia Sh.30 milioni kwa manufaa yake na wenzake wanne.

Shitaka la saba ni la utakatishaji wa fedha linalowahusu washitakiwa wote ambako Februari 2021 huko wilaya ya Hai kwa pamoja na kwa nia moja walijipatia Sh.30 milioni huku wakijua fedha hizo ni zao la uharifu.

Baada ya kusomewa mashitaka yao, washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri ya uhujumu Uuchumi hadi kupata kibali cha mahakama kuu.Share:

Habari za Ndani Kabisa Zinasema Simba Wagoma Kumpa Release Letter Bernard Morrison


Bernard Morrison anaomba release letter kwa Simba, lakini Simba hawana presha wanataka mpaka mkataba wake utamatike kisha wamkabidhi barua


Inasemekana kuna muda aliwaambia kuna klabu ya nje inamtaka, Simba wakamwambia watume offer yao watapokea ofa na watampa release letter


Taarifa za kuaminika ni kuwa anataka kujiunga na Yanga, Simba wanafahamu hilo kwahiyo hawana tatizo zaidi ya kusubiri mwisho wa mkataba

Share:

Simba Imetangaza Kumwachia Mchezaji Paschal Wawa Baada ya Mkataba wake Kumalizika


Simba imetangaza kumwachia Sultan @WawaSerge baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Klabu ya Simba imesema, mechi ya mwisho ya Wawa akiwa ndani ya uzi wa Msimbazi itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar.

Share:

Mbosso ‘Afunguka’ Kuwa na Maradhi ya Moyo

 


Mwanamuziki mahiri wa Bongo fleva, Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso amefunguka juu ya kupambana na ugonjwa wa moyo, unaodaiwa kusababishwa na maumbile ya kuzaliwa.


Akizungumza na kipindi cha Fresh mwisho wa juma lililopita, Mbosso amesema amekuwa akipambana na ugonjwa huo kimya kimya na kuwajulisha watu wachache tu wa karibu yake.


Mbosso ameweka wazi kuwa wakati mwingine hupitia wakati mgumu kutokana na kuwa usingizi na wakati mwingine hupata maumivu ya mwili kupita kiasi.


“Ndiyo nina matatizo makubwa ya moyo lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri, nafanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kudhibiti hali hiyo lakini wakati mwingine napata shida hata kufanya mazoezi kwa vile nina maumivu,” amesema Mbosso.


Huku akibainisha kutopenda kuongelea chochote kuhusu masuala yake binafsi, lakini amesema tayari amewajulisha baadhi ya wanafamilia, watu wake wa karibu na mabosi wake akiwamo msanii Diamond Platnumz juu ya tatizo linalomsibu.


“Bosi wangu mmoja alikuwa anajua, mama yangu pia anafahamu hali hiyo na pia nilimjulisha Diamond pamoja na wazazi wenzangu ila binafsi huwa sizungumzii mambo yangu binafsi mara kwa mara,” aliongeza.


Aidha, Mbosso ameweka wazi kuwa daktari aliyemfanyia uchunguzi amebaini kuwepo kwa mafuta mengi mwilini kwake ambayo yameziba sehemu ya mishipa ya damu hali inayopelekea wakati mwingine kukumbwa na tatizo la kutetemeka.


Mwimbaji huyo amesema kwamba yuko tayari kusafiri kwa ajili ya matibabu ambayo ilikuwa ayafanye muda mrefu lakini alichagua kusubiri ili kuweka mambo sawa na kuiacha familia yake katika hali nzuri kwakuwa matibabu hayo yatachukua muda mrefu.


Ugonjwa anaougua Mbosso unajulikana kwa jina la Atherosclerosis, ukiwa ni wa hali ya kawaida ambao hutokea wakati dutu nata iitwayo plaque kujilimbikiza ndani ya mishipa na uundaji wa plaque huzuia mtiririko wa damu kuenea vizuri kwenye viungo vya mwili na tishu.


Maumivu ya kifua na upungufu wa kupumua ni dalili za kawaida za hali hiyo ambayo madaktari wanasema husababishwa na ulaji wa juu wa cholesterol, shinikizo la damu na kuvuta sigara.

Share:

Viwanja vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga
Kwa Mapinga tunavyo viwanja kuanzia sqm 400, sqm 600, sqm 800, sqm 1000, sqm 1500 na sqm 2000 
Bei ya sqm ni TZS 15,000 na viko umbali wa km 2 tu kutoka main road (dar to Bagamoyo Road).
Huduma za umeme na maji zipo.

Kwa Bunju vipo viwanja ukubwa wa sqm 1000, sqm 1500 na sqm 2000 na Bei na sqm moja ni TZS 40,000

Jipatie kiwanja safi kwa maisha ya sasa na ya badae.

Piga simu kwa mmiliki
0758 603077
Share:

Harmonize Apagawa na WIMBO wa Sarafina "Upo Nyonyo" Kisa Kajala Masanja


'Real Recognize Real' hivyo ndivyo unavyoweza kusema, hii ni baada ya mwimbaji @saraphina__tz kumshukuru @harmonize_tz kwa kusapoti wimbo wake mpya uitwao "UPO NYONYO" kwa kujirekodi akiimba wimbo huo.


"Y’aaaaaaallll 🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻 @harmonize_tz , thank you so much for your support 😩😩😩😩😩 🙌🏻🙌🏻 bless u 🙏" ameandika Saraphina kupitia ukurasa wake wa Instagram.


@harmonize_tz alishare kipande cha video akiiambia wimbo wa Saraphina kupitia insta story yake akiwa na Dj wake, Dj Seven na kuisindikiza na maneno kuwa wimbo huo mpenzi wake @kajalafrida anaupenda sana mpaka amesababisha na yeye aupende.


"My woman love this song (Upo Nyonyo) kila siku. Yoo is a banger, nasikiliza all night. Ukirudi (Kajala) utanikuta nishaishika Upo Nyonyo. Someone tell Queen Fina, this is another anthem @saraphina__tz " - ameandika Harmonize.


"Upo Nyonyo" ni wimbo wa TATU kwa Saraphina kuuachia mwaka 2022, na umapata mapokezi makubwa kwa mashabiki wake. Nyimbo zake nyingine ni pamoja na "Wamerudiana" na "Number One" alizoziachia mapema mwaka huu

Share:

Wanafunzi 4 Wafariki Baada ya Ajali ya Boda Boda na Lori Mapinga, Mwanafunzi Aliekuwa Anaendesha Boda Aliwabeba Mshikaki Wenzake Watatu

 


Wanafunzi wanne wamefariki Dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongwa na Lori, katika kitongoji cha Kihara kata ya Mapinga wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.


Akizungumza na TimesDigital mwenyekiti wa Kitongoji cha Kihara Simon Kilian amesema, ajali hiyo ilitokea juzi jioni ambapo Pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na mmoja wa wanafunzi hao, iligonga kingo ya Barabara na Wanafunzi hao kuangukia barabarani hali iliyosababisha kukanyagwa na lori hilo.


“Wanafunzi walipoangukia Barabarani Lori lilikuwa katika mwendo kasi na kuwakanyaga, na hawa wanafunzi waliweza kutambulika kwa sababu mmoja aliazima Pikipiki ndipo mwenye Pikipiki akawajulisha wazazi wa wanafunzi hao.” Alisema Kilian.


Mwenyekiti Kihara amesema mara baada ya tukio hilo miili ya wanafunzi hao ilipelekwa kituo cha afya Karage, na baadae wazazi walifika ili kuitambua miili hiyo, baada ya wazazi kuitambua miili ya watoto wao ililazimika kuwazika kutokana na hali zao kuwa mbaya.


Katika hatua nyengine Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Gregory Mushi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Share:

Mbunge ahoji misafara ya viongozi kusababisha foleni barabarani

Dodoma. Mbunge wa Kyela, Ally Jumbe ameeleza  kero wanayoipata watu wakati wakisubiri misafara ya viongozi kupita kwenye barabara mbalimbali nchini.

Akichangia bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2022/23 leo Jumatatu Juni 20,2022, Jumbe amesema usalama wa viongozi nchini ni  muhimu lakini usalama huo kuna maeneo unawakwaza Watanzania.

“Utakuta kiongozi wetu anasafiri ama anapita sehemu saa tano  asubuhi lakini magari yanaanza kufungiwa kupita kuanzia saa 12 asubuhi."

"Spika hili halikubaliki katika teknolojia ya sasa hivi ni nani amewahi kufanya utafiti wa madhara yanayotokea? Mfano mtu alikuwa anaenda mahakamani, halafu akafungiwa mnajua ni watu wangapi  wameshindwa kufika mahakamani,” amehoji.


 
Ameomba watumie njia rahisi ambayo viongozi wanaweza kusafiri hata kwa  helkopta akibainisha kuwa kwa sasa Tehama inafika  maeneo mbalimbali na kuhoji kwanini hazitolewi taarifa mapema za barabara zinazotumika wakati viongozi wanapita.

“Kama unawahi sehemu uwahi kuondoka. Katika uchumi huu tunaokwenda muda ni muhimu sana tusichezee muda huu,” amesema.

Amesema juzi walikaa kwenye mzunguko (hakuutaja) kwa zaidi ya dakika 40 wakati wanakwenda bungeni lakini baada ya muda huo waliruhusiwa kuendelea na safari bila kiongozi kupita.


“Hii sio nchi ya kujenga uchumi wa blablaa, tujengee uchumi uliokamilika,” amesema.


 
Share:

Nicola Traldi akamatwa kwa kumshambulia na kumjeruhi mpenzi wake Miss Chanty (EX wa Eric Omondi)


Nicola Traldi akamatwa kwa kumshambulia na kumjeruhi mpenzi wake Miss Chanty (ex wa Eric Omondi)

VIDEO:


Share:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger