Ni muda umepita sasa tokea purukushani za kampeni zianze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Mengi tumesikia,mengi tumeona na mengi yametokea.
Hapa tulipofikia sasa ni dakika za lala salama.
Nawauliza nyie mnaojiita wanamabadiliko mmejipanga vipi?
Binafsi pamoja na umasikini wangu hivi ninavyoandika hapa nimesafirisha jamaa zangu wawili kutoka mikoani huko warudi huku Dar walikojiandikishia.
Wengi tunataka mabadiliko,lakini tujiulize tunashiriki vipi kwenye kuyaleta hayo mabadiliko?
Nitamshangaa sana yule ambaye ushiriki wake kwenye mabadiliko ni kupiga kelele huku JF na kwenye mitandao mingine ya kijamii au vijiweni.
Wakati huu tuliofikia sasa sio wa kuangalia/kujadili porojo za nani kasema nini bali kuunda mikakati mizito ya ushindi.
Kila mmoja ajiulize hapo nyumbani unapoishi wote wapo kwenye maeneo/karibu na walipojiandikishia?
Kama kuna ndugu yako kajiandikishia kijijini arudi alikojiandikishia n.k
Tukumbuke kuna wengine hawana hata shida ya nauli,hawa tuwape elimu na hamasa ya kwenda kupiga kura.
KURA YAKO PEKEE HAITOSHI KULETA MABADILIKO.