10/26/2020

Wanawake Watakiwa Kuvua Nguo za Ndani Kukaguliwa Kabla ya Safari


 Australia imeonesha kusikitishwa kwake na Qatar baada ya wanawake kuripotiwa kukaguliwa ndani ya maungo yao walipokuwa wakijaribu kuingia kwenye ndege kutoka Doha kuelekea Sydney.

Uchunguzi huo unaripotiwa kufanyika baada ya wafanyakazi katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamand kumkuta mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wake bafuni.

Kuna ripoti mchanganyiko kuhusu kama mtoto alikuwa hai au alikuwa amekufa.

Raia 13 wa Australia ni miongoni mwa wanaoelezwa kuwa walifanyiwa uchunguzi.


Walibebwa kwenye gari la kubebea wagonjwa na kuambiwa wavue nguo zao za ndani kabla ya kuchunguzwa, Channel Seven iliripoti.

Wanawake hao hawakuambiwa kwanini walikuwa wakichunguzwa kabla ya kuingia kwenye ndege ya shirika la Qatar tarehe 2 mwezi Oktoba.

Serikali ya Australia imewasilisha suala hilo kwa mamlaka za Qatar.

''Tumewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu tukio hilo kwa mamlaka za Qatar na tumehakikishiwa kupata taarifa za wazi na kina kuhusu tukio hilo muda mfupi ujao,'' msemaji wa wizara ya mambo ya nje na biashara aliwaambia wanahabari nchini Australia.
Share:

Shelisheli Inavyoipa DUNIA Tuition ya Kisiasa

 


OKTOBA 22, mwaka huu, Shelisheli walianza kufanya uchaguzi wa Rais. Walikamilisha Oktoba 24 (juzi). Kiongozi wa chama cha Seychelles Democratic Alliance, Wavel Ramkalawan, ameshinda.


Ramkalawan, mchungaji wa Anglican, amemshinda Rais Danny Faure. Kabla ya ushindi huo, Father Ramkalawan alishagombea urais wa Shelisheli mara sita bila mafanikio. Ya saba kashinda.


Shelisheli ilipata uhuru mwaka 1977, ikawa chini ya mfumo wa chama kimoja. Mwaka 1993 ilikaribisha mfumo wa vyama vingi. Wakati huo wote, chama tawala cha United People’s Party ambacho sasa kinaitwa United Seychelles Party, kikawa kinashinda. Safari hii imekuwa mara ya kwanza kwa chama cha upinzani kushinda mamlaka ya Serikali Shelisheli tangu uhuru.


TUITION YA SHELISHELI


Baada ya matokeo kutangazwa, Father Ramkalawan na Rais Faure, walitokeza mbele ya vyombo vya habari pamoja.


Ramkalawan akasema: “Mimi na Faure ni marafiki wa karibu. Uchaguzi sio mwisho wa mchango wa kila mmoja kwenye nchi yake. Katika uchaguzi huu hatukuwa na mshindi wala mshindwa. Mshindi wa jumla wa uchaguzi huu ni nchi yetu, Shelisheli.” Wakati Father Ramkalawan akisema hayo, Rais Faure alikuwa akitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na kilichosemwa.


Kipindi hiki ambacho dunia ipo kwenye harakati za uchaguzi katika nchi nyingi, tunashuhudia visa vya chuki na siasa za kung’ang’ania madaraka, Faure na Ramkalawan wanaionesha dunia kwamba uchaguzi ni kwa ajili ya nchi. Kukubali matokeo inawezekana. Mshindi na mshindwa wanaweza kupeana mikono kwa upendo.


Kipidi hiki Guinea na Ivory Coast wanahesabu idadi ya watu waliopoteza maisha kisa uchaguzi. Rais Donald Trump akigoma kutamka kuwa akishindwa uchaguzi ataachia madaraka. Rais Faure na Father Ramkalawan wanaipa somo kubwa dunia.


Faure na Ramkalawan ni somo pia kwa Tanzania. Tunakwenda kwenye uchaguzi Keshokutwa (Oktoba 28). Yapo mazingira na zipo kauli tata. Tanzania ni nchi kubwa. Tunahitaji siasa za heshima, zenye utii wa demokrasia. Wananchi ndio waamue kesho yao. Jukumu la wanasiasa ni kuheshimu uamuzi wa wananchi.


Uchaguzi wa Tanzania si wa tume, polisi wala jumuiya ya kimataifa. Ni wa Watanzania.


Ndimi Luqman MALOTO

Share:

Upinzani washinda uchaguzi UshelisheliRamkalawan, ambae ni kasisi wa zamani wa kanisa la Anglican alimshinda rais Danny Faure baada ya kuwania urais bila maafanikio kwa miongo mitatu.


Share:

Wafuasi wa Trump na Biden hawatakubali matokeo ya uchaguzi- ukusanyaji maoniWafuasi wa ugombea urais Marekani hawatakubali matokeo ya uchaguzi wa Novemba iwapo mgombea wanayemuunga mkono atashindwa

Share:

Mazrui apatikana, Abdalla hajulikani alipo ZanzibarMeneja wa kampeni wa chama cha upinzani cha ACT wazalendo visiwani Zanzibar, amesema kwamba alikuwa ametekwa nyara Jumapili na kutishiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, huku mgombea ubunge wa chama hicho akiwa bado hajulikani alipo, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28.


Share:

10/25/2020

Mdada Aliyekwambia kujua Kuzungusha Kiuno ndo Tiketi ya Kupata ndoa Kakudanganya..

Kila mwanamke anavitu vyake alivyojiwekea, ambavyo anataka mwanaume wa ndoto zake awe navyo. Ikitokea akampata Mwenye hivyo vitu basi huona kamaliza kila kitu, anajisahau, anafurahia vile anavyoviona kwa nje na kitandani, badala aanze kumsoma huyo Mwanaume. Kama ni husband material.

Wanawake ndio wanaongoza kwa kulizwa Sana kwenye mahusiano kuliko wanaume, kwasababu mwanamke akishampata mwanaume aliyekuwa anamtaka basi atampenda kwa kila kitu, moyo na mwili wake wote kwa haraka wakati yeye mwanaume hakupi vyote anakuangalia kwanza mpaka atakapoona kweli ndio kitu anachokitaka ndio ataanza kukupenda kwa ukweli sasa. Lakini akiona hakuna kitu atakuchukulia poa poa na baadaye anakupotezea, sasa wewe uliyekufa na kuoza lazima upate ugonjwa wa moyo.

Mwanamke usiende kwenye mahusiano kwa kuangalia picha ya nje, anza kwanza kumwangalia Kama anaweza kuwa Mume na je unampenda kweli, ukijihakikishia hapo anza kuwa wife material msaidie mwanaume hata kwa mawazo tu sio unakaa tu kazi yako wewe ni kuzungusha kiuno tu.

Inatakiwa ukiingia kwenye maisha ya mwanaume mwenyewe anakiri hakuna mwanamke Kama wewe. Unambadilisha hata Kama hakuwa muoaji ajue umuhimu wa mke na kutaka kukuoa.
Share:

Benard Membe Azungumzia Kuhusu Barua Inayosambaa MitandaoniMgombea wa Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, ametoa sababu ya kuandika barua iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikieleza kuhusu kujitoa kwenye kinyanganyiro cha Urais wa Tanzania bara.


Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter leo, amethibitisha kuwa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni kuwa ni ya kweli na yeye ndiye aliyeandika barua hiyo.


“Barua inayosambaa ya tarehe 24/9 ya kujiondoa kwenye mbio za Urais ni ya kweli, niliandika baada ya kutofautiana na msimamo wa Viongozi wangu wa kutaka nimuunge mkono Tundu Lissu. Hata hivyo barua hiyo ilikataliwa kwa sababu maneno " msimamo wa viongozi wangu" yanawatia hatiani.” amesema Bernard Membe


Aidha katika barua hiyo inayosambaa iliyoelekezwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif, na Katibu Mkuu wa cha hicho , Membe aliahidi kujikita katika kuwasaidia madiwani na wabunge wote wa chama hicho.


Share:

Mazrui wa ACT-Wazalendo 'atekwa' na watu wasiojulikanaNaibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana baada ya gari lake kugongwa eneo la Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Share:

Magufuli: Sumaye ni Mwana CCM, Alikumbwa na MapepoMgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli amesema kilichomtokea Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye hadi kuhamia upinzani ni mapepo lakini sasa roho mtakatifu amemuokoa.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Babati Jumapili Oktoba 25, Magufuli amesema “Sumaye ni mwana CCM halisi aliyepotea kwa bahati mbaya kutokana na mapepo yaliyomkumba siku za nyuma


“Nakushukuru sana umefanya uamuzi mzuri. Huyu alikuwa waziri mkuu nikiwa waziri wake. Kama ilivyo kawaida Mungu alipoumba malaika wengine wakagoma wakatupwa duniani, wale ndio wakamgusa Mzee Sumaye miaka kadhaa akahamia chama ambacho ni cha ajabu.
Bahati nzuri Mzee huyu alijifunza mapema akawakimbia amerudi CCM karibu sana baba. Sumaye ni mwadilifu, hicho chama hakikumfaa, chama kinachosimama hadharani na kumtukana kila mmoja, chama kisichokuwa na staha.”
Amesema,” Ninamshukuru roho mtakatifu aliyekugusa Mzee Sumaye na ukarudi nyumbani, kufanya kosa si kosa kurudia kosa ndio kosa. Ninajua umefika nyumbani hongera Mungu akubariki na uzao wako,” amesema Magufuli.


 


Sumaye aliyekuwa waziri mkuu mwaka 1995-2005, alihamia Chadema mwaka 2015 siku chache kabla ya uchaguzi na mapema mwaka huu alirejea CCM baada ya kushindwa kura za maoni za kuwania uenyekiti wa Kanda ya Pwani katika uchaguzi ndani ya chama.

Share:

Obama amkosoa Trump kushindwa kudhibiti COVID-19Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemkosoa vikali Rais Donald Trump na serikali yake hapo jana juu ya namna alivyoshughulikia janga la ugonjwa wa COVID-19 nchini humo, wakati wa hotuba yake mbele ya wafuasi wa mgombea urais wa Democratic Joe Biden. 

Obama amesema Trump hawezi kuwalinda Wamarekani, wakati anashindwa hata kuchukua hatua za msingi kujikinga yeye mwenyewe, akimaanisha kulazwa kwa rais huyo hospitalini wiki kadhaa zilizipita baada ya kuambukizwa virusi vya corona. 


Kura za maoni ya umma zimeendelea kuonyesha kuwa Biden anaongoza kinyang'anyiro hicho cha urais dhidi ya Trump wa chama cha Republican. 


Aidha Obama amemkosoa Trump kwa kusema uwongo hadharani, pamoja na kushindwa kukemea tabia ya Wazungu kujipa hadhi ya juu nchini humo.


Share:

IGP Sirro aonya vikundi vilivyopanga kufanya vurugu ArushaMkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amesema jeshi lake limepata taarifa za kuwepo kwa baadhi ya vikundi vichache katika Jiji la Arusha vyenye nia ya kuharibu amani siku ya uchaguzi na kutoa onyo kali kwe wote wenye mpango huo.


IGP Sirro ametoa kauli hiyo Jijini Arusha baada ya kuzungumza na askari polisi zaidi ya 700 watakaosimamia mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini kote Jumatano ijayo.


Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi pia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuimarsha amani na utulivu siku hiyo ya uchaguzi.


Share:

Mambo matano ya kumfanya mwanamke apagawe kwakoKuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana 
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.

Share:

Kiongozi wa Al-Qaeda Abu Muhsin al-Masri auawa AfghanistanVikosi maalum vya Afghanistan vimemuua kiongozi muhimu wa kundi la Al-Qaeda ambaye pia alikuwa akitafutwa na Marekani, idara ya ujasusi ya Afghanistan imesema.


Abu Muhsin al-Masri, Mmisri aliyechukuliwa kama kiongozi nambari mbili wa kundi la Al-Qaeda mwenye ushawishi zaidi katika kundi hilo katika kanda hiyo ya India, aliuawa katika mkoa wa Ghazni katikati mwa Afghanistan, Idara ya kitaifa ya usalama nchini afghanista imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.


Idara hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya operesheni hiyo na hakuonyesha ni lini ilifanyika. Jina la Al-Masri liko kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa sana na shirika la upelelezi la FBI la Marekani.


Al-Masri alikuwa ameshitakiwa nchini Marekani kwa kutoa ufadhili wa bidhaa na raslimali kwa shirika moja la kigeni linalohusika na ugaidi na pia kwa njama ya kuwauwa raia wa Marekani.

Share:

Gwajima na Tarimba Watoa Tathmini ya Ushindi Wao Uchaguzi MkuuMeya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye sasa ni Meneja wa Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima akizungumza kwenye mkutano huo.


WAGOMBEA Ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo la Kawe na Kinondoni leo, wametoa tathimini ya kampeni walizopiga na jinsi walivyowafikia wananchi na kubaini ushindi wa kishindo wanaotarajia kuupata katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.Gwajima akizungumza kwenye mkutano huo leo.


Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar, leo Gwajima ambaye alikuwa na Meneja wake wa Kampeni, Benjamini Sitta amesema kwa kampeni aliyofanya jimboni humo kwa mikutano ya hadhara na kuwafikia wananchi nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa kijiwe kwa kijiwe na kushuhudia kero wanazokumbana nazo wananchi wa jimbo hilo na kumfikishia Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye naye amemuahidi kumsaidia kuzitatua ni ishara tosha ya ushindi wake wa kishindo.Mkutano huo ukiendelea.


Naye Meneja wa Kampeni wa mgombea wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia, aliyemuwakilisha mgombea Abbas Tarimba alisema kutokana na umahiri wa mgombea huyo na kampeni walizopiga wanatarajia kupata ushindi wa kishindo.Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia ambaye sasa ni Meneja wa Kampeni wa mgombea ubunge jimbo hilo, Abbas Tarimba akionesha kitabu chenye tathmini waliyofanya.


Mtulia amesema mgombea urais kupitia chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mengi kwenye jimbo hilo na kuahidi kujenga Flyover nyingine tatu kwenye jimbo hilo hivyo wananchi hawana budi kumchagua na mbunge hilo ili aungane na rais kuharakisha maendeleo hayo.


“Rais wetu ametuahidi flyover zingine tatu kwenye jimbo letu Magomeni, Mwenge na Morocco ili kupunguza msongamano, sasa kwa yote hayo ni kwanini wananchi wasimpe kura na mbunge wa jimbo hilo ili kuboresha na maengineyo”. Alisema Mtulia ambaye msimu uliopita ndiye aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.   HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Share:

Majaliwa: Serikali Hainunui Korosho, Inasadia Upatikanaji Wa MasokoMJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali hainunui korosho wala mazao mengine bali inaweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa masoko.


“Serikali hainunui korosho, Serikali hainunui pamba, wala hainunui chai au kahawa. Kazi ya Serikali ni kutengeneza fursa ili wanunuzi waje. Mtu asitumie zao la korosho ili kujipatia umaarufu wa kisiasa,” amesema.


Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 25, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Likongowele na Kibutuka wilayani Liwale ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Liwale, Bw. Zuberi Kuchauka na madiwani 20 wa kata za jimbo hilo.


“Mwaka 2018, kuna wafanyabiashara waliungana na wakagomea kununua korosho kwa sh. 1,800. Rais Dkt. Magufuli akasema hakuna kununua korosho za wakulima kwa bei hiyo, ndipo akatoa sh. bilioni 900 ili zitumike kununua korosho kwa bei isiyopungua sh. 3,000 kwa kilo.”


“Fedha hizo zimetumika kuwalipa wakulima, wasafirishaji, wenye magunia, kulipia usimamizi wa maghala na sasa imebakia kuwalipa Halmashauri ambao wanadai ushuru wa asilimia 5, na hao ni Serikali wenzetu kwa hiyo watalipwa tu. Kama kuna wakulima waliobakia ni mmoja mmoja sana, hao wanafuatiliwa na Wizara husika.”


Amesema korosho siyo zao pekee lililoathiriwa na kuporomoka kwa bei bali mazao mengine kama pamba, chai, kahawa na tumbaku nayo yameathiriwa na kushuka kwa bei mwaka huu.


“Korosho ni miongoni mwa mazao ya kimkakati nchini yaliyokosa soko msimu uliopita baada ya mataifa ya Ulaya kufunga mipaka yao kutokana na ugonjwa wa corona na hivyo wanunuzi hawawezi kuja nchini.”


“Korosho, pamba, tumbaku, chai na kahawa hayakuwa na bei nzuri kutokana na corona si vinginevyo. Serikali hainunui mazao, kazi yake ni kutengeneza mazingira mazuri ya soko asije mtu akawadanganya na kutumia bei za mazao ili apande chati kisiasa,” alionya.


Akitoa mfano, Mheshimiwa Majaliwa amesema: “Bei ya pamba imeshuka kutoka sh. 1, 200 hadi sh. 800 kwa kilo; kahawa imeshuka kutoka sh. 1,800 has sh. 1,200 kwa kilo, na tumbaku imeshuka kutoka sh. 1,700 hadi sh. 1,400.”


“Wanunuzi wakubwa wa korosho wanatoka China, Singapore, Vietnam na India. Hawa wenzetu sasa hivi bado wameelemewa na ugonjwa huu, hawawezi kutoka na kusafiri. Tuwaombee nchi zao ziondokane na corona ili na sisi tuweze kufanya biashara na nchi nyingine,” alisisitiza.

Share:

Polisi nchini Nigeria yaagiza uhamasishaji baada ya ghasia

 


Inspekta jenarali wa polisi nchini Nigeria M.A Adamu ameagiza uhamasishaji wa haraka wa maafisa wote wa polisi ili "kurudishanafasi ya umma kutoka kwa wahalifu wanaojisingizia kuwa waandamanaji'' baada ya siku za maandamano ya amani dhidi ya dhuluma za polisi na kishamachafuko ya vurugu ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu 69. 

Agizo hilo la polisi huenda likachochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini humo katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea katika muda wa miaka kadhaa. 


Katika taarifa, Adamu aliwaagiza maafisa wenzake wa polisi kudhibiti nafasi ya umma akisema ghasia zilizoko zimetosha.


Siku ya Jumanne jioni raia wa Nigeria walitazama kwa hofu wakati wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya waandamanaji wa amani wengi wao wakiwa vijana waliokuwa wakiimba wimbo wa taifa jijini Lagos, huku ripoti ya shirika la Amnesty International ikisema kuwa angalau watu 12 waliuawa. 


Matukio nchini Nigeria yamefananishwa na vuguvugu la ''maisha ya watu weusi ni muhimu'' nchini Marekani na ufyatuaji risasi wa wanajeshi umeibua shtuma za kimataifa.

Share:

Kwanini Mwanaume Ukilala na Mwanamke Usipompa Hela Baada ya Tendo Anakudharau Sana?

Utamaduni wa wenzetu walioendelea huwa mtu akitoka out na mpenziwe mwanamke ndiye anaclear bill lakini kwa nchi zetu za kibongo ukimtoa mwanamke out atafanya kukukomoa aagize vitu vya gharama balaa isitoshe zaidi watoto wa chuo hakawii kubeba marafiki zake wa kutosha.

Sasa ukija swala la kudo iwe mchana au usiku mkimaliza anasikilizia unamtoa na sh. ngp usipomtoa ela anakudharau sana na huwa wananungunika sana.

Hivi wadau ukitoka kudo lazima umtoe mwanamke hela wakati starehe mmesikia wote na zaidi wao ndiyo wanasikia raha zaidi? Hapo umemtoa out mmekula, kunywa, hela ya lodge n.k, gharama ushatumia kama laki na nusu bado tena umtoe hela?
Share:

Kassim Majaliwa Afanya Mkutano Mkubwa wa Kampeni Wilayani Liwale Mkoani Lindi


NI MAGUFULI DAY: Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Kassim Majaliwa ameendelea na Mikutano yake ya Kampeni Kunadi Sera na Ilani ya CCM Kisha kuomba kura. Na Leo Jumapili amefanya Mkutano Mkubwa wa Kampeni Wilayani Liwale Mkoani Lindi na haya ndiyo aliyoyazungumza Kwenye Mkutano huo Mkubwa. Liwale inasema ilikosea na Sasa wametubu, Oktoba 28 wanaenda na CCM tu kwa maendeleo na si ubabaishaji tena.


#KuraKwaMagufuli2020

#T2020JPM

Share:

Makazi ya Mondi Yatapakaa Kinyeshi

 


Baada ya miezi kadhaa kupita tangu supastaa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atangaze kutoa misaada ya kodi kwa familia 500, hatimaye msaada huo umegeuka majanga kwa wakazi wanaoishi jirani na makazi ya jamaa huyo kufuatia kutapakaa kinyesi cha binadamu.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kilicho jirani na makazi ya Diamond au Mondi maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, kilipenyeza ubuyu kuwa hali ni mbaya kutokana na watu hao wanaoshinda kila siku kutaka msaada.


Supastaa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

“Jamani ule msaada aliosema Diamond atautoa kwa watu umeleta shida hapa mtaani kwetu, hawa watu wanaohitaji msaada wamegeuka kero kwenye eneo hili, wanajisaidia hovyo; yaani vinyezi vimetapakaa nje hapa kama nini, tunaomba mje muangalie hali halisi ilivyo,” alisema jirani mmoja ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini.

IJUMAA MZIGONI…

Baada ya kupewa ubuyu huo, Gazeti la IJUMAA huwa halilazi damu hivyo lilitimba nyumbani kwa Mondi na kukuta nyomi ya watu mbalimbali wakiwa nje ya geti wakisubiri kupewa chochote kitu.

WAFUNGUKA…

Gazeti la IJUMAA lilifanikiwa kuzungumza na baadhi ya watu hao ambapo kila mmoja alieleza changamoto yake.

Kuna baadhi walisema kuwa, tangu wamefika nyumbani hapo kwa Mondi, wana wiki kadhaa, lakini hawajawahi kukutana na msanii huyo.


“Mimi nimetokea Kigoma, kuna sehemu inaitwa Kibirizi, nilivyosikia lile tangazo kuwa Diamond atatoa msaada wa pesa, ndiyo nikaja huku Dar.

“Tangu nimefika nina miezi miwili, sina ndugu wa aina yeyote ile, ikifika usiku nahangaika sehemu ya kulala, kila tukijaribu kugonga getini kwake tunafukuzwa, ndiyo ikabidi nije kwa huyu mama (jirani wa Diamond) ndiye ametupa hifadhi ya kulala,” alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Steven Maisara.

MWINGINE WA MWANZA…

“Mimi natokea Mwanza, tumefika hapa muda mrefu sana, hatuna sehemu ya kula wala kulala, Mondi akitoka humo ndani yupo kwenye gari lake wala hatusikilizi, tunaomba mtusaidie tupate hata nauli ya kurudi nyumbani kwetu,” alisema mama mwingine aliyejitambulisha kwa jina Halima.

MKAZI WA ENEO HILO…

Mbali na wahitaji hao, mama mmoja mkazi wa eneo hilo ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe gazetini alitoa malalamiko yake kuwa, anaomba msanii huyo awaondoe watu hao katika eneo hilo kwani wamegeuka kuwa kero kubwa.

“Mimi nipo hapa mwaka wa 25 sasa, tangu huyu Diamond atoe kauli yake ya kusaidia watu, imekuwa kero kwa sisi tunaoishi hapa.


“Yaani kuna matukio ya kila aina. Mfano; wiki chache zilizopita kuna mama alibakwa hapa nje na baadhi ya hao vijana wanaojifanya wanahitaji msaada, tukiondoka majumbani mwetu tukirudi tunakuta wameiba vitu.

“Yaani ninakuambia hivi Mondi anatufugia wezi hapa maana siyo wote waliopo hapo wanahitaji msaada wengine ni wezi, jambo lingine ni kwamba hawa watu tangu wamefika hapa hawana sehemu za kulala hivyo ikifika usiku wanajisaidia hovyo tu, hali inayotufanya tukiamka asubuhi tunakuwa na kazi ya kuzoa vinyesi vyao utasema tunazoa vinyesi vya mbwa.


“Tumechoka jamani, tumechoka sana, kama hii hali ikiendelea tunaweza kukumbwa na magonjwa mengi ya mlipuko, tunaomba mumfikishie hizi taarifa Diamond awaondoe hawa watu hapa tumechoka,” alisema mama huyo.

SERIKALI YA MTAA…

Ili kupata mizani ya habari hii, Gazeti la IJUMAA lilifika mpaka kwa mjumbe wa eneo hilo, Sara Kimaro ambaye naye kwa upande wake alikiri kuliona tatizo hilo.


“Ni kweli wala siyo uongo, hilo tatizo lipo tena halijaanza leo wala jana, mfano huyo mama aliyebakwa tulifanikiwa kuwakamata vijana waliofanya unyama huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.


“Tumeshajaribu kadiri ya uwezo wetu kumtafuta huyo Diamond, lakini hatujawahi kufanikiwa. Kila tukifika pale nyumbani kwake tunaishia getini, haturuhusiwi hata kuingia ndani, ila maadam waandishi wa Gazeti la IJUMAA mmekuja, basi tutafanya jitihada za kumuandikia barua ili njia aliyoitumia kutangaza kuwa atatoa msaada ndio atumie njia hiyohiyo kuwatangazia kuwa amesitisha kutoa msaada wa pesa ili waondoke eneo lile.


“Pia siku nyingine akihitaji kusaidia watu, basi ashirikishe Serikali za Mtaa tutamsaidia au atumie njia nzuri ya kusaidia watu hao kwa sababu hivi anavyofanya sasa hivi anatuletea vibaka hapa,” anasema Mama Kimaro.


IJUMAA KWA MONDI


Baada ya kusikia malalamiko hayo, Gazeti la IJUMAA liligonga hodi nyumbani kwa Mondi ambapo walinzi walikuwa wakali kama pilipili kichaa.


“Hayupo nyumbani, nendeni ofisini kwake, haturuhusu mtu kusogelea geti…” Ilisikika sauti ya mlinzi ndani ya geti la Mondi.


 


Alipotafuta Mondi simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp ulionesha ameusoma kwa kuweka tiki mbili, lakini hakujibu.


Kwa upande wao, mameneja wa Mondi, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella ‘Mkubwa’, waliomba kuachwa kwanza kwa kipindi hiki wakiwa bize na uchaguzi ambao umekaribia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu (Jumatano ijayo).


Tale anagombea Ubunge katika Jimbo ya Morogoro Kusini-Mashariki na Fella anagombea Udiwani katika Kata ya Kilungule, Temeke jijini Dar, wote kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


STORI: Memorise Richard na Jackline Wandiba, Ijumaa

Share:

Maalim Seif "Mamlaka Zimuachie Nassor Mazrui Mara Moja"

 


Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amezitaka Mamlaka kumuachia Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Nassor Mazrui

 

Amesema, "Kuna taratibu za kukamata mtu, na kilichofanyika ni uvamizi na uhuni. Tunatoa wito Mazrui aachiwe mara moja"

 

Kwa mujibu wa Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe, Mazrui ametekwa leo asubuhi na wanaosemekana kuwa Vijana wa Jeshi la JKU Zanzibar akiwa anaelekea Ofisini


Share:

Simi Aitamani Ndoa Ya Zuchu, DiamondSTAA wa muziki wa Afro – R&B nchini Nigeria, Simisola Kosoko a.k.a Simi amefunguka kuwa, anatamani kuwaona mastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zuhura Othman ‘Zuchu’ wakifunga ndoa. Diamond na Zuchu ni wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) huku Mondi akiwa ndiye mmiliki wake.


Ingawa Zuchu bado ni msanii mchanga lakini moto wake anaouonyesha kwenye game ndiyo uliofanya aingie kwenye levo za ustaa fasta.

Akipiga stori na gazeti hili kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii kutoka Nigeria, Simi amemwambia mwandishi wetu kuwa, anavutiwa sana na Mondi na Zuchu kiasi cha kutamani kusikia ndoa yao ikifungwa hata kesho. “Nawapenda sana hao wasanii, siwezi kufi cha hisia zangu. Wanapendezea sana,” anasema Simi na kuongeza: “Unajua muziki unakua, unasafi ri na kufi ka mbali.


Kwa sisi wasanii wa Afrika, tunajisikia fahari kutanua mashabiki wetu hasa ndani ya bara letu kabla ya kutusua zaidi nje. “Sababu hiyo imenifanya niwe mfuatiliaji sana wa wasanii wa ndani ya Afrika… na katika hili lazima niwe mkweli, wasanii wa Afrika Mashariki wanafanya kazi nzuri sana.


Kwa mfano Uganda, nawafuatilia sana wasanii kama Navio (Daniel Lubwama Kigozi) na zamani kidogo Jose Chameleon.


“Kenya nilikuwa nikizimika sana na Nazizi, lakini kwa wasanii wa sasa nawapenda zaidi Sauti Sol. Kwa hapo Tanzania, msanii wangu wa muda wote ni Diamond. Huyo bwana anajua sana.”


Anasema kwa sababu ya kuvutika na muziki wa Bongo Fleva na hasa msanii Diamond kama chaguo lake, amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana.


“Nasoma sana mitandao, ni kweli sijui Kiswahili kabisa, lakini mitandao mingi ya Kenya na Uganda hutumia Kiingereza, lugha ambayo naifahamu, inanisaidia kujua kinachoendelea kwenye muziki wa Afi ka Mashariki.


“Kwa sasa naona habari za moto zinasema Diamond na Zuchu ni wapenzi, kama ni kweli ni kitu kuzuri na kiukweli natamani sana wafunge ndoa.


Wanapendezeana sana,” Simi anazidi kumwaga baraka zake kwa wasanii hao. Simi ambaye mwezi huu amedondosha singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘No Longer Benefi cial’ ni mke wa msanii wa muziki na mbunifu nchini humo, anayekwenda kwa jina la Adekunle Gold.


Anasema, anajisikia huru kuoana na msanii huyo kwa sababu wanafahamiana vizuri na anampa mwongozo na sapoti kubwa kwenye muziki. Simi ameshatoa nyimbo kadhaa akishirikiana na mumewe, Gold, ukiwemo ‘No Forget’ unaofanya vizuri kwenye game.


Akizidi kushusha mistari kwa wasanii hao, Simi anasema: “Kuna raha fulani hivi ya kipekee unaipata kwa kuoana na mtu ambaye mnayefanana vitu mnavyofanya. Najua ninachosema maana nipo kwenye ndoa na mtu wa aina hiyo.


“Diamond na Zuchu wakifanya hivyo, wataipata raha hiyo, lakini pia watakuwa huru zaidi kufanya kazi kwa ufanisi, ukaribu na mafanikio zaidi.”


Simi anasema kwa uzoefu wake, ndoa nyingi za mastaa wanaooana na wasio maarufu huvunjika mapema, huku akitaja sababu kubwa kuwa ni kutokuendana. “Lakini mkioana wasanii mnakuwa mnazungumza lugha moja, ndiyo maana nitajisikia raha sana siku nikisikia Zuchu na Diamond wamefi kia hatua hiyo,” anasema.


UHUSIANO WA ZUCHU NA DIAMOND

Nyota ya Zuchu imeanza kung’ara akiwa na WCB chini ya Diamond na tangu amechomoka moto wake haujawahi kuzima.  Hata hivyo kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba wawili hao wamekuwa wakitoka.


Uhusiano wao umekuwa ukishabikiwa na wengi, lakini hakuna yeyote kati yao aliyejitokeza kuthibitisha au kukanusha kuhusu uwepo wa uhusiano huo. Mashabiki wengi waliotoa maoni yao mitandaoni kuhusu uhusiano wao, wameonekana kuunga mkono kapo hiyo.


DIAMOND NA UHUSIANO


Historia ya kimahusiano ya Diamond in aonyesha namna anavyopenda kutoka na mastaa. Baadhi ya mastaa aliowahi kutoka na kudumu kwa muda mrefu kabla ya kuachana ni pamoja na Wema Sepetu (mwigizaji – Bongo), Penniel Mungilwa ‘Penny’ (Mtangazaji – Bongo) na Jacqueline Wolper (Mwigizaji – Bongo).


Mbali na mastaa hao, amepata kutoka na mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili.


Aidha, amekuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki na mwanamitindo wa Kibongo, Hamisa Mobeto ambapo walibarikiwa kupata mtoto mmoja.


SIMI NI NANI?


Anaitwa Simisola Kosoko, lakini mwenyewe alifupisha jina lake na kuwa Simi. Alizaliwa mwaka 1988, Yaba / Ojuelegba, jijini Lagos – Nigeria. Kipaji chake kilianza kuchomoza tangu akiwa mdogo, ambapo alikuwa akiimba na kucheza kwenye kwaya ya kanisani kwao huko Lagos, Nigeria.


Baadaye alipokuwa mkubwa, aliingia rasmi kwenye muziki mwaka 2014. Baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri tangu wakati huo ni pamoja na ‘Tiff’, ‘Jamb Question’ na ‘Love Don’t Care’ alizoimba peke yake.


Nyimbo alizoshirikiana na wasanii wengine ni pamoja na Solder (Falz), No Forget (Adekunle Gold – mumewe) na ‘So Rire’ (Legendury Beatz). Alifunga ndoa na Gold, Aprili mwaka jana.

Share:

Makete: Kijana Auawa kwa Kuchepuka na Mke wa Mtu

 


 

Kijana aliyejulikana kwa jina la  Casto Zakaria (28) mkazi wa Tukuyu Mbeya amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na kutobolewa macho tukio lililotokea katika kijiji cha Kisinga kata ya Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 24, 2020 ambapo kijana huyo aliyekuwa akifanya kazi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Moronga Makete chini ya kampuni ya CRSG, amefikwa na mauti huku taarifa za awali zikidai chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi


Wakazi wa kijiji hiki ambao wamefika eneo la tukio, wameeleza masikitiko yao kufuatia tukio hilo.


"Hili tukio kweli linasikitisha kwasababu ni tukio la kwanza kwenye kijiji hiki,na ukifuatila hata wazee wetu hamna mtu aliyewahi ua kwa kinyama namna hii"alisema Alisema Costantino swalo mkazi wa kijiji hicho.


Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga Bw. Mose Chaula amesema tukio hilo ni la kikatili na yeye anamiaka 7 madarakani lakini hajawahi shuhudia tukio la mauaji ya kikatili kama hilo


"mimi sasa hivi nina miaka saba kwenye uongozi sijawahi kutana na tukio kama hili,wito wangu kwa wananchi waachane na tabia hizi na kama kuna jambo linakuzidia uwezo jitahidi kuona uongozi wa kijiji na uongozi unaofuata"alisema  Mose Chaula 


Inadaiwa kwamba mke mdogo wa Marehemu aliyetajwa kwa jina la Adivera Msigwa alikutwa na mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mumewe Bw. Nolasco Msigwa nyumbani kwa marehemu huyo ambapo anatuhumiwa kutekeleza kitendo hicho cha mauaji na baadhi ya vitu vilivyokutwa nyumbani alipokuwa akiishi marehemu zikiwemo nguo na viatu vya kike vilipooneshwa kwa wananchi waliweza kuvitambua na kutaja.


Mwenyekiti  wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy amefika eneo la tukio na kukemea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi na kupoteza uhai wa wenzao

"Ni tukio la kusikitisha sana kutoa uhai wa mwenzako kwa namna hii.hata kama ni kosa ukimkuta mwanaume yupo kwenye kifua cha mke wako,na hii inadhihirika mauaji haya ni wivu wa kimapenzi na kwa vielelezo vinavyosemekana viko ndani na jinsi alivyokutwa marehemu alikuwa anajaribu kujiokoa ametoka kama alivyozaliwa lakini kuna nguo za mwana mama ziko ndani pamoja na nguo za nyumba.Hiki ni kitendo cha kikatili mno,tuache kujichukulia sheria mkononi"alisema Veronika Kessy


Jeshi la polisi wilaya ya Makete linamshikilia mke wa mtuhumiwa aliyekutwa nyumbani kwa marehemu kwa hatua zaidi huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Share:

"Hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini"Dkt. Mahera

 


Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchin (NEC) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura vimeongezwa katika baadhi ya majimbo.Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera,amesema kuwa hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini huu ni upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa kutangaza kuwa kuna vituo hewa.”Nashangaa kuona taarifa za uzushi zikisambaa kwenye mitandao na baadhi ya viongozi wa vyama kuanza kulalamika na kuzusha kuwa NEC imeongeza vituo hewa vya kupigia kura nchini”amesema Dkt.Mahera

Share:

Membe Ataja Sababu ya Kumuunga Mkono Lissu "Barua ya Kujitoa Kwenye Mbio za Urais ni Kweli"

 
Mgombea wa Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, ametoa sababu ya kuandika barua iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikieleza kuhusu kujitoa kwenye kinyanganyiro cha Urais wa Tanzania bara.

 

Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter leo, amethibitisha kuwa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni kuwa ni ya kweli na yeye ndiye aliyeandika barua hiyo.


“Barua inayosambaa ya tarehe 24/9 ya kujiondoa kwenye mbio za Urais ni ya kweli, niliandika baada ya kutofautiana na msimamo wa Viongozi wangu wa kutaka nimuunge mkono Tundu Lissu. Hata hivyo barua hiyo ilikataliwa kwa sababu maneno " msimamo wa viongozi wangu" yanawatia hatiani.” amesema Bernard Membe


Aidha katika barua hiyo inayosambaa iliyoelekezwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif, na Katibu Mkuu wa cha hicho , Membe aliahidi kujikita katika kuwasaidia madiwani na wabunge wote wa chama hicho.

Share:

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger