Rais Dr. Magufuli na Mhe. Majaliwa: Karata za CCM kisiasa, zitafanikiwa?

Natazama kuteuliwa kugombea na baadaye kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kwa Dr. Magufuli kwa tiketi ya CCM kama karata muhimu iliyochangwa na kuchezwa na CCM katika uchaguzi uliopita. Iko wazi kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani Tanzania, kilijijenga vya kutosha katika maeneo ya Kanda ya Ziwa yenye mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera. Kitendo cha kusimamishwa kwa Dr. Magufuli ni kitendo cha kutikisa ngome ya CHADEMA.

Dr. Magufuli ni mwenyeji wa kanda hiyo kwakuwa amezaliwa, kukua, kufanya kazi na kuwa Mbunge huko Chato mkoani Geita. CHADEMA iliachwa mkono na wananchi wa kanda ya ziwa si kwakuwa ilipoteza umaarufu. Iliachwa mkono kwakuwa tu wananchi wa kanda ya ziwa waliona mwaka huu ni 'zamu yao' kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani kabila kubwa kuliko yote nchini-wasukuma.

Kuibuliwa kwa Dr.Magufuli ni karata ya kukata nguvu za upinzani-hasa CHADEMA katika Kanda ya Ziwa iliyoonja ladha ya operesheni mbalimbali za kichama katika kujenga na kuimarisha CHADEMA. Kama hiyo haitoshi, CCM imecheza karata nyingine leo kupitia kwa Rais Magufuli kumteua Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kanda ya kusini inasemwa kama kanda iliyo nyuma kuliko zote kimaendeleo.

Pia kanda hiyo ina vuguvugu la gesi asilia lililopelekea wananchi wa huko kupunguza kuipenda na kuishabikia CCM. Kuteuliwa kwa Mhe. Majaliwa ni kuwapa nafasi watu wa Kanda ya Kusini kujisogeza kimaendeleo na kuonyesha kuwa CCM inawajali na kuwathamini wananchi wa huko na hivyo wananchi wa huko wasahau madhila na vuguvugu la gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wawili hawa (Dr. Magufuli na Mhe. Majaliwa) hawakupata nafasi zao kwa bahati mbaya ila ni karata muhimu kwa CCM. Karata hizi zitafanikiwa?
Last edited by Petro E. Mselewa;

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BASI HAPO KWISHNEHI CHADEMA ,KWA ASILIMIA KARIBIA ZOTE, NGOJENI MUONE WAZIRI WA MADINI NA NGUVU ZA NISHATI HAPO NDIO MTASALIMU SANA ,,,, JIPANGRNI SANA MPAKA LABDA BAADA YA MIAKA 20 IJAYO BYE BYE CHADEMA, MLALE SALAMA

    ReplyDelete
  2. Kumbe CCM kuna ukabila na ukanda

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani mwenzetu upo nchi gani? hivi hauoni CHADEMA imevuma sana mikoa gani? bado haujapata picha tu?

      Delete
    2. Kanda ya ziwa hatukutaka kufanya hivyo na ndio'mana Lowasa alipokuja huku na barabara tulideki, lakini katikati ya kampeni 'tukastuka' kumbe 'wenzetu' wanatumia ukabila na ukanda, hasa pale Regina Lowasa alipowahutubia watu wake akiwasisitizia wachaga na 'wakaskazini' popote pale walipo wampe kura Lowasa, ndipo hapo na 'sisi' tukabadili kibao. Yaani tungekuwa wajinga kweli kama tungemwangusha JPJM....DAWA YA MOTO NI MOTO

      Delete
    3. CHADEMA IMEPATA KURA NA VITI VINGI VYA UBUNGE NA UDIWANI KTK KANDA YA KASKAZINI, INANISHANGAZA WANAPOSEMA ETI WAMEIBIWA KURA.......KANDA YA ZIWA TULIWANYIMA KWELI, WALA HAWAKUIBIWA

      Delete
  3. Mdau ulikuwa haujui kuwa bongo underground ukabila upo kama kawa juu ya juhudi alizofanya Nyerere lakini hakufanikiwa sasa hivi ndio upo open huo ukabila

    ReplyDelete
  4. ulikuwa hujui mbona watu wa kaskazini ona ambavo hawakutaka kumchagua magufuli bora hata kanda ya ziwa angalau walikuwa wanapishana kidogo fikiria lowasa alikua anampita kama laki moja sio ukabila huoooo tena watu wa kaskazin mna ukabila hata msiongee angalia chama cha chadema viongozi wote ni waukanda wa kaskazini kama unabisha fatilia..............hapakazitu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad