Ukweli Kuhusu Kipini Cha Diamond Huu Hapa...Maneja wake Afunguka Ukweli....

Kwa masaa kadhaa picha ya Diamond Plutnumz akiwa na kipini puani, imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na kuwaacha mashabiki wake njia panda.

Mashabiki wengi walionekana kumkosoa kwa uamuzi wake wa kubandika kipini puani huku wengine wakionekana kuwa waelewa wa kile alichokifanya.

Swali ambalo linazunguka kwenye vichwa vya mashabiki na wapenzi wengi wa muziki je, ni kweli Chibu katoga pua yake?

Meneja wake Sallam, aliamua kutegua kitendawili hicho na kaamua kuandika kwenye mtandao wa kijamii, akisema msanii wake huyo aliamua tu kuwashtua watu si kweli kwamba ametoboa pua.
“Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo,” aliandika Sallam

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hivyo vidole hiyo ni sign ya 'freemason', hebu tuamshe na hilo maana tumelala usingidhi wa pono msee!!

    ReplyDelete
  2. Bora kama hajatoboa, maana nina salam zake kutoka kwenye dala dala nililopanda leo wamama wameongea chafu na lawama nyingine zikaenda kwa bi. mkubwa wake mama Dai, kwamba alikuwa nae ulaya wakati anatoboa pua na hakusema kitu!! na wakaenda mbele zaidi kwa kusema siku atakayo kanyaga Dar live watamletea zawadi nyingine ya shanga ili akamilike kabisa!! sasa aone ni jinsi gani alivyowaudhi watu!

    ReplyDelete
  3. Asijaribu kanisa

    ReplyDelete
  4. kwani akifirwa atawaambia hao mameneja wake?

    ReplyDelete
  5. Ah dalili ya mvua ni?Naona anazo tayari shanga kama ametoa kidole..tusubiri mkono .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad