Imefichuka,Kumbe Wasumbiji Wanawafukuza Watanzania Nchini Kwao kwa Sababu Hizi,Ikiwemo Umbeya na Majungu..!!!


Mara baada ya kupata taarifa za Watanzania wenzetu ' kufurumushwa ' nchini Msumbiji niliweza kufanya mazungumzo na Mtanzania mmoja aitwae Bwana Hamidu ni Mfanyabiashara mkubwa kati ya Tanzania, Msumbiji na Afrika ya Kusini na kwa Wale Watanzania muishio Afrika ya Kusini hasa mji wa Cape Town kati ya Mtaa wa Mowbry na Randebosch mtakuwa mnamjua sana huyu Hamidu na amewahi pia kuishi mno Kibiashara nchini Msumbiji.

Mazungumzo yangu na Kaka Hamidu yalilenga hasa katika kutaka kujua nini ' Kiini ' cha kilichowakuta Ndugu zetu Watanzania huko ugenini nchini Msumbiji na ndipo akaniambia sababu kadhaa ambazo naziweka hapa Kwenu ili mzijue na ikiwezekana tuzijadili.

Na ikumbukwe nimesukumwa pia kulifuatilia hili suala hasa kwa kuangali Uhusiano mzuri katika tena wa Kindugu ambao uliwekwa vizuri kabisa na Waasisi wa nchi zetu hizi mbili Hayati Mwalimu Nyerere na mwenzake Hayati Samora Machael.

Bwana Hamidu alisema kuwa vinavyotugharimu Watanzania hasa tuwapo ugenini na ndivyo pia vimewagharimu wenzetu waliokuwa nchini Msumbiji ni vifuatavyo:

Uwizi uliotukuka na hasa wa Simu na Magari, Matusi na kuwadharau Wazawa.

Uuzaji uliotukuka kabisa wa Dawa za Kulevya na hasa hasa Bangi / Bange.

Kuendekeza ' ushirikina ' wetu tuliotoka nao Tanzania na kuwaroga Wenyeji bila huruma.

Kutopenda kufanya Kazi na kuishi kwa ' kuomba omba ' sana hadi wametuchoka.

Umalaya na hapa hakuficha akasema kuwa Wanaume wa Kitanzania wanapenda sana ' kuwabandulia ' Wasumbiji wake zao na Wanawake wa Kitanzania ni ' maarufu ' kwa kupenda ' kubanduana ' na Wanaume wa Msumbiji.

Majungu. Hapa alisema kuwa Watanzania wakiwa wanatafuta Kazi au wawapo Kazini huku hupenda mno kuwapiga ' Majungu ' wazawa kwa Matajiri ili wafukuzwe Kazi kisha wabakizwe wao na ambapo na Wao pia huwaleta Ndugu zao wengi kutoka nchini Tanzania.

Utapeli uliotukuka kwa wanaowafanyia Wazawa wananchi wa Msumbiji. Na katika hili Bwana Hamidu alisema kuwa si jambo geni uwapo nchini Msumbiji kumsikia Mtanzania uliyemjua tokea huku huku Bongo akiitwa Kassim lakini huyo huyo ukikutana nae Maputo huko anaitwa George na ukibahatika tena kukutana nae mji wa Cabo Delgado utasikia anaitwa Benjamin na wamekuwa wakiwatapeli Wasumbiji huku wakihama hama miji ili kujificha na wasijulikane na waweze kufanikisha wanachokitaka na maisha yanaendelea.

Wandugu hizo ndizo sababu ambazo Mmoja wa Watanzania ambaye ameishi sana huko Bwana Hamidu amenipa na kasema kuwa hakuna Watu ' Wavumilivu ' kama Wasumbiji ila kwa vitendo hivyo saba ( 7 ) nilivyoviorodhesha hapo uvumilivu wao Kwetu Watanzania umewashinda na kama ' mbwai mbwai ' tu.

Naomba kuwasilisha na nimshukuru tu Bwana Hamidu wa Cape Town Afrika ya Kusini kwa ushirikiano wake mkubwa juu ya kunifunulia nini hasa kiini cha tatizo la Watanzania wenzetu ' kufurumushwa ' nchini Msumbiji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad