Zifahamu Faida Mbalimbali za Tangawizi Katika Mwili Wako

Hicho ni kiungo kinachotokana na mzizi wa mmea unaoitwa Tangawizi. Ni mmea unaofanana sana na binzari, ikiwa bado haijamenywa maganda yake.

Pia, ni bidhaa inayopatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi, anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au hata kilo akipenda.

Hivi karibuni akiwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye sasa ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliendesha kampeni kubwa ya uzalishaji wa tangaweizi wilayani humo, ikiwa sehemu ya zao la biashara.

Mmea huo unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu katika mtindo wa mazoea, lakini ni kiungo kinachotumiwa kama dawa.

Pia, kiungo hicho kinaweza kutumika kikiwa ama kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa katika mfumo wa unga.

Faida zake

Tangawizi ni kati ya mimea mingi yenye maajabu. Unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa zaidi ya 72 mwilini mwa mwanadamu.

Ina faida zaidi hasa kwa wagonjwa walioathirika na maambukizi ya Ukimwi. Hivyo, kwa wale wenye matatizo ya aina hiyo, wanaweza kufaidika zaidi na maaajabu ya mmea huo - tangawizi.

Namna ya kutumia katika nafasi yake ya dawa, ikiwa imesagwa au mbichi imepondwa, inaweza kutumika kama kinywaji na imezoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia tangawizi ni katika chai. Inakuwa mbadala wako wa majani ambayo yenyewe huwa na vimelea vya kafeini, ambavyo vinachangia magonjwa mengi mwilini.

Pia, inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mboga zingine, kuongezwa katika ‘juisi freshi’ na kuleta ladha nzuri ambayo ni dawa.

Kuna mambo yafuatayo yanatokana na matumizi ya tangawizi:

-Kuongeza hamu ya kula.
-Kupunguza kichefuchefu.
-Kutapika na kuharisha.
-Inatibu kisukari.
-Shinikizo la damu.
-Kuongeza msukumo wa damu.
-Kutoa sumu mwilini.
-Maumivu ya tumbo.
-Gesi tumboni.

Pia,tangawizi inasaidia kuyeyusha chakula tumboni mwa binadamu. Vilevile, ina nafasi ya kusaidia matatizo ya mafua na magonjwa mengineyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad