Jeshi la Polisi Mwanza Lazungumzia Tukio la 'Kutekwa' Mkuu wa Chuo cha Nyakato Islamic Institute, Sheikh Bashir Gora

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna ameeleza juu ya tukio la kupotea kwa Mkuu wa Chuo  cha Nyakato Islamic Institute kilichopo chini ya Taasisi ya Elimu ya The Registered Trustees of Islamic, Sheikh Bashir Gora na kudai jeshi linaendelea kumtafuta.

Kamanda Shanna amesema ni kweli wamepokea taarifa za kupotea kwa Sheikh huyo hivyo ameagiza kufungwa kwa mipaka yote ya Mkoa wa Mwanza ili kuhakikisha kiongozi huyo anapatikana mapema iwezekanavyo.

"Ni kweli tumezipata taarifa za kupotea kwake, lakini unajua mtu akipotea huwezi kujua tatizo ni nini, na hatujui kwanini hapatikani na tumemtafuta kila mahali hapatikani, tumeshafunga mitambo yetu kwenye maeneo yetu yote."

Akizungumza hivi karibuni, Katibu wa Bodi wa taasisi hiyo, Sadik Mchola alisema tukio hilo lilitokea Disemba 6 chuoni hapo ambapo alikuja kijana mmoja kuulizia nafasi za kujiunga na chuo kwaajili ya mdogo wake.

“Kijana huyo alitukuta ofisini, Sheikh akamwambia aje Januari mwakani atapewa utaratibu, kijana aliondoka lakini baada ya muda kidogo akarudi tena kuulizia malipo, Sheikh akamwambia Januari ndiyo tutakueleza kila kitu, akaondoka."

“Baada ya hapo wakawa wanazungumza na Sheikh huku anamsindikiza kumbe walikuwa wameegesha gari yao nyuma ya chuo walipoikaribia, alitoka kijana mwingine kwenye gari hiyo wakambeba Sheikh na kumuingiza ndani kisha gari likaondoka kwa speed (mwendo) mkali,” alisimulia.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad