Wajue Masupasta 10 Waliofariki Kwa Ugonjwa wa UKIMWI

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Kwa Mujibu wa WHO inasadikika karibia watu milioni 35 wanaishi na VVU na kati ya hao 1.5m ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15.Inasadikikia pia 24.7mils yao wapo kusini mwa jangwa la sahara.Mpaka sasa karibia watu 19milioni wameshafariki tangia ugonjwa huo ulipoanza kuua mwaka ya 1981.

Ifuatayo ni Baadhi ya Masupasta wakubwa waliofariki kwa AIDS Related Complications.

1. Rock Hudson(November 17, 1925 – October 2, 1985)
Alikuwa ni Msanii wa filamu kutoka marekani,alitamba sana na movie zake kama pillow talk,giant na magnficient obsession .Mbali na kuwa mcheza filamu pia alikuwa na vipindi vya Television miaka ya 70s na 80s iliyojulikana kama MacMillan and wife.Mpaka anafariki ametengeneza filamu karibia 70.Hudson alifariki 1985.
Hudson.jpg
2. Erick Wright(September 7, 1963 – March 26, 1995)
Alikuwa anajulikana Zaidi kama Eazy-E,mwanzilishi wa Ruthless record,ndiye aliyemtoa msanii na producer billionea Dr.Dre miaka ya 80s.Eazy –E alikuwa mmoja wa mwanamuziki waliounda kundi la N.W.A na wenzake Ice Cube na Dr. Dre.Alitamba na vibao vyake maarufu kama Eazy Duz it,Eazy-er Said than Dunn and Real Muthaphuckin’ Gs.Eazy E alifariki mwaka 1995.
Erick Wright.jpg

3. Kevin Peter Hall(May 9, 1955 – April 10, 1991)
Alikuwa mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Alifahamika sana kwa kucheza kwake katika filamu kama vile Misfits of Science, Prophecy, Without Warning, na Harry and the Hendersons. Alitambulika mno kwa kucheza uhusika wa filamu ya Predator almaarufu Anodi ya Jini.Yeye ndiye aliyeigiza kama Jini.Kevin alifariki mwaka 1991.
Kevin Hall.jpg

4. Freddie Mercury (5 Septemba 1946 – 24 Novemba 1991)
Alikuwa mwimbaji wa bendi ya Queen, ambayo inapiga muziki wa rock. Freddie Mercury ni mtanzania alizaliwa mjini Zanzibar katika familia ya Waparsi yenye asili ya Uhindi, lakini yeye na familia yake walihamia Uingereza baada ya mapinduzi ya Zanzibar alipokuwa bwana mdogo. Yeye, Brian May, Roger Taylor na John Deacon waliumba Queen mwaka 1970. Kwa Queen aliandika nyimbo zingi maarafu, kama "Bohemian Rhapsody", "Killer Queen", "Somebody to Love", "Don't Stop Me Now", "Crazy Little Thing Called Love" na "We Are the Champions".Freddie alikufa mwaka 1991.
freddie_main.jpg

5. Willi Smith((February 29, 1948 – April 17, 1990)
Mzaliwa wa Philadefia,USA,Alikuwa mmoja wa Mbunifu wa mavazi kijana mdogo wa kimarekani mwenye mafanikio makubwa.Kampuni yake ya mavazi WilliWear ilikuwa ikiuza mavazi yenye thamani ya usd 25mils kwa mwaka.Smith alianza kazi ya ubunifu miaka ya 1967.Smith alifariki mwaka 1990 kwa sababu ya Aids related complications.
Willi Smith.jpg

6. Fela Kuti(15 Oktoba 1938 – 2 Agosti 1997)
Alikuwa mwanamuziki wa Nigeria. Jina lake la kuzaliwa ni Olufela Olusegun Oludotun Ransome-Kuti. Alikuwa anapiga muziki wa ki-afrika(Afrobeat).Fela alitamba na vibao kibao miaka ya 70s kama why blackmen they suffer,open and close,gentlemen,afrodisica n.k.Alifariki mwaka 1997,Mmoja wa wanawe ni Femi kuti,mwanamziki mkubwa chini uingereza.
Fela Kuti.jpg

7. Arthur Ashe(July 10, 1943 – February 6, 1993)
Alizaliwa Richmond Virginia,Alikuwa ndio ,Mchezaji wa kwanza Duniani wa tenis wa kulipwa.Aliwahi shinda tunzo tatu za Grand Slam ambazo zilimfanya kuwa mchezaji wa kutisha sana barani amerika.Arthur ndiye alikuwa mweusi wa kwanza ulimwenguni kushinda tunzo ya US Open na Australian Open.Alifariki mwaka 1993.
ASHE_Arthur.jpg

8. Jermaine Stewart (September 7, 1957 – March 17, 1997)
Alikuwa ni mwanamziki wa kimarekani aliyetingisha na kibao kikali cha “we don’t have to take clothes off” miaka ya 80s na kushika number mbili katika chati ya UK na Canada na namba 5 U.S Billboards.Pia alikuwa member wa kundi la muziki maarufu sana Shalamar kundi ambalo lilitamba na kibao kama A night to remember(Get ready tonight),Mbali na kuwa mwanamziki pia Alikuwa ni Dancer katika Kipindi cha television kijulikanacho kama Soul Train.
JermaineStewartDM.jpg

9. Gia Marie Carangi (January 29, 1960 – November 18, 1986)
ALizaliwa philadephia na ndio inaaminika alikuwa the first supermodel miaka ya 70s na 80s.Gia ameonekana sana front page kwenye majarida makubwa kama Vogue, na Cosmopolitan miaka ya late 70s na mwanzoni mwa 80s.Alishafanya kazi na makampuni makubwa ya mitindo kama Arman,,Christioan Dior,Versace na Saint Laurent.Alipata ukimwi kutokana na kuchangia sindano alizokuwa anajidunga za heroin.Angelina Jolie alifanya movie iliyoigiza maisha yake inajulikana kama Gia aliitoa 1998.
Gia Model.jpg

10. David Bryon Cole (June 3, 1962 - January 24, 1995)
Alikuwa producer na mmoja wa mwanamzuki waliounda kundi la C&C Musica Factory waliotamba ni vibao hatari kama,Everybody dance now na Gonna make you sweat miaka ya 90s.Cole alishawatengenezea ngoma kali wanamuziki kadhaa pia akiwemo Mariah carey,James Brown,Aretha Franklin n.k Mariah Carey alitunga kibao cha One Sweetday february 1995 kama kumbukumbu kwa producer wake David Cole.
David COle.jpg
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad