Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga imesema imepokea Majeruhi 37 waliotokana na ajali ya leo asubuhi ya Basi la abiria la ‘mwendokasi’ kugongana na gari dogo eneo la Kisutu Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Neema Mwangomo amesema kati ya Majeruhi hao, Wanafunzi ni 24 na Watu wazima ni 13 na kuongeza kuwa hawajapokea kifo.
“Mpaka sasa walioruhusiwa kwenda nyumbani ni 27, saba wamepewa rufaa ya kwenda MOI kwa matibabu zaidi na Watu watatu wamelazwa Muhimbili”
Kuhusu hali ya Mwanaume anayeonekana kwenye video ya CCTV akigongwa na basi la mwendokasi, Neema amesema atatoa ripoti kumuhusu baadaye.