R Kelly atatumikia kifungo cha mwaka mmoja zaidi kwa mashtaka yanayohusiana na picha zisizofaa za watoto na unyanyasaji wa Kingonio baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka 30 cha ulaghai alichohukumiwa mwanzo.
Mwimbaji huyo wa R&B, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, amekumiwa kifungo cha miaka 20 jela siku ya Alhamisi, lakini atatumikia takriban hukumu zote kwa wakati mmoja pamoja na kifungo alichopata mwaka wa 2022.
Mwaka 2022 R Kelly alihukumiwa jela miaka 30 kwa unnyanyasaji wa Kingono lakini pia leo amehukumiwa miaka 20 jela kwa kesi iliyoitwa ulaghai wa kingono.
Watu wengi wamekuwa wakiuliza maswali sasa itakuwaje wakati R.Kelly alishahukumiwa miaka 30 jela na sasa amehukimiwa miaka mingine 20??
Jibu ni kwamba R.Kelly atatumikia miaka yote kwa wakati mmoja na badala yake ataongezewa mwaka mmoja jela yaani itakuwa miaka 31.
Adhabu hii ya ziada ina maana kwamba Kelly atatumikia si zaidi ya miaka 31. Atastahiki kuachiliwa akiwa na umri wa karibu miaka 80.
Swali kuu lililohusu hukumu hiyo lilikuwa kama Jaji Harry Leinenweber angeamuru kijana huyo mwenye umri wa miaka 56 kutumikia kifungo hicho cha ziada kwa wakati mmoja na au baada ya kumaliza miaka 30 tu yaani endapo angemaliza miaka 30 angeongeza miaka mingine 20 lakini jaji aliweka wazi kuwa ataitumikia kwa wakati mmoja ila ni hukumu mbili tofauti na badala yake atakapomaliza miaka 30 jela ile ya mwanzo basi ataongezewa mwaka mmoja kufidia hukumu ya miaka hii 20 aliyohukumiwa leo.
Kama jaji asingetoa ufafanuzi kwa maana hiyo ingekuwa sawa na kifungo cha maisha.