Wenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa 2023 (AFCON), Timu ya #IvoryCoast wanaweza kuishia Hatua ya Makundi baada ya kukubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Equatorial Guinea ambayo imeingia Hatua ya 16 Bora toka Kundi A
Timu nyingine iliyosonga mbele katika Kundi hilo ni Nigeria ambayo imeifunga Guinea-Bissau goli 1-0, matumaini ya Ivory Coast kusonga mbele yatategemea Faida ya ‘Best Loser’ yaani timu ya tatu ambayo itakuwa na matokeo mazuri
Hivyo, Msimamo wa Kundi A, Equatorial Guinea pointi 7, Nigeria (7), Ivory Coast (3) na Guinea-Bissau (0)