Daktari bingwa wa masikio, pua na koo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila Dkt. Jonas Ndasika amesema matumizi ya kuchangia kwenye vifaa vya sauti kama vile 'headphones' na 'earphones' yanasababisha maambukizi kwenye masikio.
Vifaa hivyo pia vimetajwa kusababisha matatizo ya usikivu kutokana na kuweka sauti iliyopitiliza kiwango kinachoshauriwa na wataalamu wakati wa kuvitumia.
Dkt. Ndasika ameongeza kuwa sikio lina uwezo wa kujisafisha lenyewe na kwamba haishauriwi kitaalamu kulisafisha kwa mtindo ambao watu wameuzoea wa kutumia vijiti vyenye pamba na kuviingiza sikioni.
Amesema kufanya hivyo kunausukuma uchafu uliopo ndani ya sikio ambao mwisho wake hujilundika na kuwa mwingi jambo ambalo linasababisha sikio kupoteza uwezo wake wa usikivu.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA