Yanga Yashtukia Mtego, Gamondi aitisha kikao kizito na mastaa wake

 

Yanga Yashtukia Mtego, Gamondi aitisha kikao kizito na mastaa wake

Mashabiki wameshaanza kushona jezi za Ubingwa wa Yanga msimu huu, lakini Kocha Miguel Gamondi ameshtukia mechi mbili zinazofuata zina mtego mkubwa kwao na akawaweka chini wachezaji wake.


Gamondi amesema amewasisitiza wachezaji wake wasijisahau kwani wanakwenda kucheza na timu ambazo zimechukua tahadhari kubwa kuliko kawaida na zina malengo mengi.


Kocha huyo amesisitiza anaamini kila mchezaji kambini amemwelewa na anajua nini cha kufanya kwenye mechi hizo mbili dhidi ya Mtibwa na Dodoma Jiji.


Anasema ukiachana na ugumu ambao amekutana nao wa makosa ya waamuzi, anaamini kesho dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa ni mechi ya jasho na damu kwani wenyeji watabadilika kabisa kimbinu kama walivyowafunga Tabora ili kuinusuru roho yao.


Gamondi amesema nidhamu ya upambanaji iliyoonyeshwa na wachezaji wake amewasisitiza wasijisahau wanapokutana na mechi ngumu kama hizo za timu zinazowania kubaki kwenye ligi dakika za mwisho na wao wakipambana kufunga hesabu.


Gamondi amesema wachezaji wake wamemuahidi  ujasiri wa kutokata tamaa na watahakikisha ushindi kwenye mchezo huo wa Jumatatu Mei 13, pia mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya Dodoma Jiji.


“Unapokwenda kukutana na timu inayopambana na janga kama hili la kutoshuka, hiyo ni mechi ngumu, tunawaheshimu Mtibwa Sugar lakini lazima tujipange kitofauti na mechi za namna hii,” alisema Gamondi.


“Kitu ambacho nakifurahia kwa wachezaji wangu ni namna wanavyopambana kijasiri na kutokukata tamaa kwenye mazingira magumu kama ambayo tumekutana nayo kwenye mechi zilizopita ngumu ambazo tumelazimika kuziamua mwishoni.


“Unaona kila mchezaji anatamani kuona hataki muda umalizike bila Yanga kupata pointi tatu sio wale wanaoanza hata wale ambao wamekuwa nje ndio maana unaona kuna mechi tumeziamua na wale walioanza au hata wale ambao wataingia.


“Mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Dodoma kwao na hata tukiwa nyumbani zimekuwa ngumu, kwa hiyo tumejiandaa kukutana na ugumu huo lakini tumejiandaa kupambana na mazingira yote ili tupate ushindi na kujihakikishia ubingwa mapema bila kujali changamoto tutakazokutana nazo.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad