Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51 baada ya ndege ya kijeshi aliyokuwa akisafiria kuanguka katika msitu kaskazini mwa nchi hiyo.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo lenye ukungu la Msitu wa Chikangawa, imepatikana baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mzuzu, Kaskazini mwa Malawi, jana asubuhi saa 4:00.
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ametangaza kuwa mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka, iliyokuwa imewabeba Makamu wa Rais, Saulos Chilima, na wengine tisa aliokuwa akisafiri nao, yamepatikana bila manusura.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA