Aziz Ki atua Dar, Atolewa Kininja Uwanja wa ndege

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Aziz Ki atua Dar, Atolewa Kininja Uwanja wa ndege

Taarifa itakayowashusha presha mashabiki wa Yanga ni kwamba hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephanie Aziz KI, amewasili nchini huku akitolewa Uwanja wa Ndege kininja.


Aziz Ki, amewasili nchini alfajiri ya leo Julai 10, 2024 akitokea mapumzikoni kwao Burkina Faso kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia lakini akatoka kimkakati uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere terminal 3.


Alichofanya Azizi Ki, kwanza akamtanguliza mfanyakazi mmoja wa Uwanja wa Ndege mbele na mabegi yake makubwa sita aliyotua nayo.


Hatua ya pili ikawa Ofisa mmoja wa Yanga Godlisten Anderson 'Chicharito' aliyekuja kumpokea uwanjani hapo kumpenyezea kofia maarufu kwa jina la kepu, ambayo kiungo huyo ilipomfikia akatoka akiwa ameishusha kijanja mithili ya mtu asiyetaka kujulikana.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad