Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amesema sherehe ya harusi yoyote itakayokuwa inafanyika Mkoani Arusha na kuhusisha wasiokuwa Wakazi wa Mkoa wa Arusha, Serikali ya Mkoa chini yake itagharamia ukumbi popote ndani ya Mkoa huo ili kufanikisha harusi hiyo.
Makonda amesema hayo wakati akiongea na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Arusha leo July 08,2024 ambapo amesema lengo ni kuvutia zaidi Wageni na Watalii kufika Mkoani Arusha ili kuwa chachu ya kukuza uchumi wa Mkoa huo.
“Lengo letu sisi ni hatutaki kuwa na high season au low season, tunataka kutengeneza shughuli na matukio mbalimbali kuhakikisha kuwa muda wote uchumi unakuwa na kuendelea ili Mama wa mboga, bodaboda na kila Mtu anufaike na ugeni unaofika hapa Arusha”
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA