Yanga: Ndoto ya Manji inakwenda kutimia hivi karibuni

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Yanga: Ndoto ya Manji inakwenda kutimia hivi karibuni

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga Afrika, Ali Kamwe amesema kuwa ndoto ya mfadhili na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Yusufu ManJi inakwenda kutimia siku si nyingi.


Amesema Manji alikuwa na ndoto ya kuona Yanga inatwaa ubingwa wa Afrikana kwamba timu hiyo inaendelea kujipanga kutimiza ndoto hiyo. Manji alifariki dunia hivi laribuni nchini Marekani alikokuwa akitibiwa.


Kufuatia kifo hicho, Kamwe ametoa salamu za pole kwa mashabiki wote nawapenzi wa Yanga na kumwombea mapumziko mema huko alikotangulia.


"Kwa níaba ya viongozi wa Young Africans, kamati ya utendaji yote, sekretarieti, wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga tumepokea kwa mshtuko sana taarifa ya msiba huus. Sisi Yanga tutaendelea kumwenzi ManJi na tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi," amesema Kamwe.


Kamwe amesema hayo leo Julai 1, 2024 katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusherehekea ujio wa Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama ambaye Jana alimaliza mkataba wakena Klabu ya Simba na leo ametangazwa rasmi kwa ni 'Mwananchi'.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad