Wastara "Mama Sajuki Aanza Kunifanyia Visa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

IKIWA ni takribani siku siku 47 tangu alipofariki staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kuna madai kuwa tayari visa vimeanza kati ya mkewe Wastara Juma na mama yake mzazi yaani mkwewe, Ijumaa Wikienda limetonywa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Sajuki amekuwa akidaiwa kumfuatilia Wastara kwa kila anachokifanya hadi kufikia hatua ya kuwaambia watu wamchunguze.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wastara na mama Sajuki walifikia hatua ya kurushiana maneno mbele za watu huku ulemavu wa mjane huyo wa Sajuki ukitajwatajwa.
“Unaambiwa wakija watu kumuombea dua Wastara na kumwambia atapata mwanaume mwingine, mama Sajuki anashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio,” kilidai chanzo hicho.

Mama mzazi wa Sajuki.

Kiliendelea kudai kuwa siku moja Wastara alitembelewa na watu kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya nyumba anayoishi, Tabata-Bima, Dar ambapo mama Sajuki alidaiwa kuwafuatilia watu hao akitaka kujua mazungumzo waliyokuwa wakifanya na mkwewe huyo.
Kiliendelea kutiririsha madai kuwa siku ya arobaini ya Sajuki, mama Sajuki aliwaka mbele ya kadamnasi akikasirishwa na kitendo cha Wastara kupiga picha akidai huko ni kujitangaza.

HUYU HAPA WASTARA
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa sakata hilo lilihamishiwa usiku kwani Wastara naye alikuja juu akiomba waweke kikao ili kuweka mambo sawa mbele ya baba Sajuki, mzee Juma Kilowoko.
Baada ya kujazwa habari hizo, dawati la Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wastara ili kusikia upande wake juu ya ishu hiyo ambapo alisema kuwa pamoja na yote, kwa upande wake anamheshimu mama mkwe wake.

MAMA SAJUKI ALIKUWA NA HAYA
Alipotafutwa mama, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilipata uchungu sana wakati wa arobaini kwani mama aliyekuwa akiendesha dua (Mariam Dedesi), alikuwa akisema tumuombee Wastara apate mwanaume mwingine, kama mzazi ni kweli nililia kwa uchungu na kutamka maneno mazito,” alisema mama Sajuki.
Wastara Juma.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani huyu dada hayuko Edda?? Edda huwa mwanamke wa kiislamu anapo fiwa na mume ni lazima akae ndani miezi minne na siku kumi bila ya kuonekana na mwanamume yeyote ambae anaeza kumuoa,, nashangaa nikiskia amepiga picha na kuianika mara watu wamemtembelea kwa offisi ni mapema sana kwake kujiingiza katika scandal kama hizi, yeye ni muislamu akae edda ajistiri inavyotakikana, kama jina lake "WASTARA" atulie na kama ni kuolewa tena sioni kama kuna ubaya ila kwa sasa afwate sheria ya kidini Amkalie edda mumewe kipenzi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sure!! Na issue ya bi mkubwa ni ubinadam tu! inaonekana hamfatilii kwa ubaya ni mapenzi alonayo kwa Wastara anaposkia wanamwombea apate mume anaumia anatamani angekua mkwewe cku zote.

      Delete
  2. hata iweje atapata m2 mwingine, na hayo mambo mengine hayamuhusu yeyote mwacheni mtoto wa wa2 apumue jaman

    ReplyDelete

Top Post Ad