Showing posts with label Uchumi. Show all posts
Showing posts with label Uchumi. Show all posts

5/04/2022

Bei Mpya za Mafuta ya Gari Zilizoanza Kutumika Leo Hizi Hapa


Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji Tanzania (Ewura) imetangaza kuanza kutumika kwa bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kuanzia leo Jumatano Mei 4, 2022 ambapo bei ya nishati hiyo imeendelea kuongezeka.


Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Jumanne Mei 3, 2022 bei ya mafuta ya petroli katika Jiji la Dar es Salaam itakuwa Sh3, 148 na dizeli Sh3,264 kwa lita.Mkoa wa Tanga bei ya petroli itakuwa Sh3,161 wakati dizeli itakuwa Sh3,264 huku mkoa wa Mtwara peroli ikiuzwa Sh3,177 na dizeli Sh3,309 kwa lita.Ewura imesema bei ya mafuta ya taa katika Jiji la Dar es Salaam itakuwa ni Sh3112 kwa lita na kwamba mabadiliko ya bei za mafuta nchini yanatokana na kuongezeka kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia
Share:

10/03/2021

TRA Yatoa Taarifa Ya Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Robo Ya Kwanza Ya Mwaka Wa Fedha 2021/22
TRA Yatoa Taarifa Ya Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Robo Ya Kwanza Ya Mwaka Wa Fedha 2021/22
Share:

5/25/2021

Tanzania yaweka rekodi mauzo ya dhahabuTANZANIA imeuza nje dhahabu yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni tatu (takribani shilingi trilioni 7 za Tanzania) kuanzia Aprili mwaka jana hadi Machi mwaka huu.

Kati ya mwaka 2019 hadi 2020 Tanzania iliuza nje dhahabu ya Dola za Marekani bilioni 2.3.

Katibu Mtendaji wa chemba ya migodi Tanzania, Gerald Mturi alisema hayo alipozungumza na HabariLEO.

Mturi alisema, uchambuzi uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni kulinganisha kipindi kilichopita cha kuanzia Aprili 2020 na kipindi hiki kilichoishia Machi mwaka huu ikiwa ni sawa na miezi 12.


 
Kwa mujibu wa Mturi kiasi hicho cha mauzo hakijawahi kufikiwa tangu Tanzania ianze kuuza dhahabu nje ya nchi.

Alisema mauzo makubwa ya dhahabu nje ya nchi yalianza baada ya kufunguliwa kwa migodi mikubwa hasa kuanzia mwaka 1999.

Mturi alisema mambo yaliyochangia kuongezeka kwa mauzo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji kutoka kwa wachimbaji wadogo na janga la ugonjwa wa Covid-19 kuanzia Desemba mwaka 2019 nchini China na madhara yake kuanza kujitokeza nchini Machi mwaka jana.


Mturi alisema kuanzia wakati huo bei ya dhahabu ilianza kupanda kwa sababu katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani, Uingereza, Japan, Australia na nchi nyingine za Ulaya, wawekezaji wanawekeza fedha kwenye masoko ya hisa.

Alisema katika nchi hizo uwekezaji mkubwa unafanyika kwenye masoko ya hisa kama ilivyo kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ambako watu hununua hisa za kampuni.

“Sasa kunapotokea majanga ya kidunia  kama ugonjwa wa corona au vita, thamani ya hisa kwenye masoko hayo huwa zinaporomoka, siku zote huwa hivyo, sasa zinapoporomoka thamani ya hisa zinasababisha wawekezaji kutoa hela zao kule, wanakimbilia kununua dhahabu kwa sababu inaaminika kwamba dhahabu ina uwezo wa kutunza thamani ya fedha,”alisema Mturi na kuongeza;

“Kwa hiyo unanunua dhahabu unakaa nayo miaka miwili au mitatu baadaye unaiuza, sasa kwa kuwa wengi walikuwa wanatoa fedha zao kwenye masoko ya hisa na kuwekeza kwenye kununua dhahabu, ikalazamisha bei ya dhahabu kupanda juu kutokana na uhitaji na mpaka sasa hivi bei bado iko juu.”


 
Mturi alisema bei ya dhahabu itaendelea kuwa juu mpaka ugonjwa wa Covid-19 utakapodhibitiwa ndipo uwekezaji mkubwa utarejea kwenye masoko ya hisa na kusababisha bei ya dhahabu kushuka.

Alisema wakati bei ilipoanza kupanda, wakia moja ilikuwa inauzwa kwa Dola za Marekani 1,300 Desemba 2019 na kwa sasa bei ya wakia moja ni Dola za Marekani 1,800 ingawa kuna wakati bei ilipanda hadi kufikia Dola 2,000 za Marekani kwa wakia moja.
Share:

4/11/2021

Mashahidi 18 kutoa ushahidi kesi ya kusafirisha kilo 19 za heroinMashahidi 18 na vielelezo zaidi ya sita, vinatarajiwa kutolewa katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kg 19, inayowabili raia watatu wa kigeni kutoka nchi zao Latvia na Nigeria.


Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni raia wawili wa Latvia, Linda Mazure na mpenzi wake Martins Plavins, pamoja na raia wa Nigeria, Henry Ozoemena.Mashahidi hao wanatarajia kutoa ushahidi wao, Mahakama Kuu, Kitengo Cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.Ni baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na washtakiwa hao kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo(Committal Proceeding).Akisoma maelezo yao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kassian Matembele, wakili Mzava amedai, Linda alikamatwa Aprili 17, 2019, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  Dar es Salaam(JNIA), akisafirisha dawa za kulevya ndani ya mabegi mawili yenye rangi ya udongo na nyeusi.Amedai akiwa katika  eneo la kuondokea ndege, alipitisha mabegi yake kwenye mashine ya kukagulia mizigo na ndipo mkaguzi alipoyatilia shaka baada ya kuona vitu visivyo vya kawaida kupitia mashine hiyo.Baada ya mabegi hayo kupita Linda alijitokeza kuyachukua na ndipo mlinzi alipomtaka asubiri na baadaye alitakiwa kufungua mabegi hayo ili yakaguliwe tena."Linda alifanya hivyo na kutoa vitu vyote ikiwemo nguo zake kisha mabegi hayo yakiwa matupu yalipitishwa tena katika mashine, na iliendelea kubaini kuwepo vitu vingine na ndio ilipoamriwa mabegi hayo kuchanwa na kukutwa na kiasi hicho cha madawa hayo aina ya heroin," amedai wakili Mzava.Amedai baada ya hapo Linda alikamatiwa na kuhojiwa na jeshi la polisi.Mzava ameendelea kudai kuwa, Aprili 19, 2019 alikamatwa Plavins eneo la Kariakoo Dar es Salaam na alikiri kumsafirisha Linda kutoka Lativia kuja Tanzania kuchukua dawa hizo za kulevya na walikuwa wakiishi wote King's Hotel.Muda mfupi baadae, alikamatwa, Ozoemena na katika mahojiano na jeshi la polisi alikiri kumpatia Linda begi moja lilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kg 15, wakati walipokutana Plavins hotelini.Mbali shtaka la kusafirisha dawa za kulevya, Ozoemena anakabiliwa na shtaka la kuishi nchini bila kuwa na kubaki kwani aliingia nchini Julai mosi, 2017 na wakati anakamatwa kibali chake cha matembezi kilikuwa kimeisha muda mrefu.Washtakiwa baada ya kusomewa maelezo yao na ya mashahidi, walikubali majina yao, siku walipofikishwa mahakamani, lakini walikana mashtaka yanayowakabili.Washtakiwa baada ya kusomewa maelezo hayo, Hakimu Matembele amesema, kesi hiyo ameihamishia Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu uchumini na Makosa ya Rushwa kwa ajili ya usikilizwaji. 

Share:

2/03/2021

Petroli, Dizeli Bei Juu

Watumiaji wa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa watatakiwa kuongeza kiasi cha pesa zaidi kila watakapohitaji bidhaa hizo baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza ongezeko la bei.


Kwa mujibu wa taarifa mamlaka hiyo, mabadiliko ya bei ya mafuta katika Februari, 2021 yanayoingizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa viwango tofauti huku ikitajwa kuchangiwa na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji.Sasa wanunuzi wa rejareja wa mafuta ya petroli watatakiwa kuongezeka Sh53 zaidi kwa kila lita watakayonunua, kuongeza Sh134 zaidi kwa kila lita ya dizeli huku watumiaji wa mafuta ya taa wakitakiwa kuongeza Sh119 kwa lita ikilinganishwa na bei ya mwezi Januari, 2021.Katika Jiji la Dar es Salaam wanunuzi wa rejareja watanunua petroli kwa Sh1,887, dizeli kwa Sh1,829 na mafuta ya taa kwa Sh1,769.Pia wanunuzi wa mafuta kwa jumla watatakiwa kuongeza Sh52.90 sawa na asilimia 3.10 kwa kila lita ya petroli, Sh133.36 sawa na asilimia 8.51 kwa kila lita ya dizeli na Sh118.31 sawa na asilimia 7.77 kwa kila lita ya mafuta ya taa.Kwa mujibu wa Ewura pia bei ya jumla na rejareja za petroli na dizeli katika mikoa ya kaskazini yaani Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara nayo imebadilika ikilinganishwa na toleo la mwezi Januari.Bei ya rejareja ya petroli na dizeli katika mikoa hiyo imeongezeka kwa Sh91 kwa lita na Sh80 kwa lita katika mtiririko wa awali huku bei ya jumla ya mafuta ya petroli na dizeli ikiongezeka kwa Sh90.92 kwa lita na Sh79.48 kwa lita katika mtiririko wa awali.Hata hivyo, bei ya mafuta ya taa katika mikoa hiyo itaendelea kubaki kama ilivyokuwa mwezi Januari kwa sababu hakukuwa na shehena ya mafuta hayo iliyopokelewa katika bandari ya Tanga Januari 2021.Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa wakazi wa Tanga watanunua petroli na dizeli kwa Sh1,919 na Sh1,834, Kilimanjaro - Moshi (Sh1,966 na Sh1,880), Arusha (Sh1,976 na Sh1,890), huku wakazi wa Manyara – Babati wakinunua mafuta kwa (Sh2,010 na Sh1,924).Hali ya kuongezeka kwa bei pia imeonekana pia katika mikoa ya kusini ambapo bei ya rejareja ya petroli na dizeli zitapaa kwa Sh71 kwa lita sawa na Sh76 kwa lita katika mtiririko wa awali.Sasa wakazi wa Mtwara watalipa Sh1903 kwa kila lita ya petroli na Sh1829 kwa kila lita ya dizeli, wakazi wa Lindi watanunua kwa Sh1,917 na Sh1,842 huku wakazi wa Ruvuma- Songea wakilipa Sh1,989 kwa lita na Sh1,914 katika mtiririko uleuleBei za mafuta pia katika mikoa mingine kama Mwanza itakuwa Sh2,037 kwa petroli na Sh1,979 kwa dizeli, Mbeya itakuwa Sh1,994 na Sh1,936, Dodoma Sh1,935 na Sh1,888 huku Geita ikiwa ni Sh2,054 na Sh1,995 kwa dizeliKatika taarifa yake Ewura imesema kampuni za mafuta ziko huru kuuza petroli kwa kuzingatia bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni iliyopitishwa.“Pia vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika,” inaeleza taarifa hiyo“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja,”

Share:

1/23/2021

Shilingi Trilioni 18 zinapita kwenye huduma ya fedha mtandao kwa mwezi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa kiasi cha shilingi trilioni 18 zinapita kwenye mitandao kwa mwezi wakati wa kikao chake na kamati hiyo kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA -CCC) na Tume ya TEHAMA (ICTC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma
Dkt. Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kiasi cha miamala milioni 300 inafanyika kwa mwezi mtandaoni na Serikali inapata shilingi bilioni 80 kwa mwezi za tozo kutokana na fedha zinazopita mtandaoni na mzunguko huo wa fedha mtandaoni kwa mwezi, miamala inayofanyika na tozo ambazo Serikali inapata ni kutokana na kuwepo kwa matumizi ya TEHAMA

Amefafanua kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni ambapo Wizara imejipanga kuandaa ramani ya njia ya  miundombinu huo ili kufanikisha mwingiliano wa ujenzi na upanuzi wake pale inapokutana na njia za miundombinu mingine kama vile ya barabara, maji, umeme na reliNaye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuongeza udhibiti na usimamizi wa huduma za mawasiliano kwenye suala la fedha mtandao ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuweza kuongeza mchango wa tozo Serikalini zaidi ya shilingi bilioni 80 kwa mwezi kwa kuwa miamala mingi ya fedha inafanyika na fedha nyingi zinapita kwenye mtandao ili TEHAMA iongeze mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi na kuchangia zaidi pato la taifa.

Usikubali Kupitwa na Udaku wa Mjini INSTALL App ya UDAKU Special >HAPA ili Tuwe Tunakutumia Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Wizara itaipa ushirikiano wa kutosha Kamati hiyo ili kwa pamoja Serikali kupitia Wizara hii na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wote kwa pamoja wanamhudumia mwananchi
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Wizara itaendelea kusimamia na kuendesha vema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za mawasiliano na TEHAMA inatumika kurahisisha maisha yao ya kila siku katika nyanja ya kiuchumi na kijamii
Share:

8/05/2020

Ndege Kubwa Kubwa za Kimataifa Zaendelea Kutua Tanzania Licha ya Corona Kuitesa Dunia

Tanzania inaendelea kushuhudia ndege kubwa za kimataifa zikiendelea kuwasili katika viwanja vyake vya ndege tangu Rais @MagufuliJP kutangaza na kuruhusu viwanja vya ndege kufunguliwa baada ya changamoto ya Janga la Corona.

Unazoziona ni Baadhi ya ndege kubwa kama zilivyokutwa leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam.

Share:

7/31/2020

Masoko ya Hisa Duniani YaporomokaMasoko ya hisa duniani na masoko ya hisa nchini Marekani yamelegalega baada ya hazina ya Marekani kuonya kwamba janga la virusi vya corona huenda likatishia uchumi uliorejea katika hali ya kawaida uliyoweka viwango vya riba karibu ya sifuri.

Kuanguka kwa hisa kuliongezeka kwa kasi katika mataifa ya Ulaya baada ya Ujerumani kusema uchumi wake ulinywea kwa asilimia 10 katika robo ya pili kwenye kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Viwango vya chini vya riba na matarajio ya wawekezaji juu ya uwezekano wa kupatikana kwa chanjo dhidi ya virusi vya corona vilisaidia masoko ya dunia kuwa kwenye hali nzuri katika sehemu kubwa ya mwaka huu.
Share:

China na Urusi Zawekewa Vikwazo na Umoja wa UlayaUmoja wa Ulaya umeziwekea China, Urusi na Korea Kaskazini vikwazo kwa kuwapiga marufuku maafisa wa idara za ujasusi za nchi hizo kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umechukua hatua hiyo kutokana na idara hizo kutuhumiwa kushiriki katika shughuli za udukuzi wa kimtandao duniani kote.

Idara hizo za ujasusi zinatuhumiwa kujaribu kufanya udukuzi kwenye shirika la kudhibiti silaha za nyuklia. Waliowekewa vikwazo hiyvo ni maafisa sita na taasisi kadhaa za nchi hizo tatu.

Na kwa ajili ya kujihami dhidi ya hujuma za kimtandao Umoja wa Ulaya ulipitisha utaratibu wa kisheria wa kuuwezesha kuweka vikwazo. Vikwazo vya Umoja wa Ulaya pia vitahusu kuzuia mali za watu na hata za taasisi.
Share:

7/30/2020

Mahakama Manyara yataifisha Madini ya Tanzanite yaliyokamatwa Simanjiro


Julai 29,2020, Mahakama mkoani Manyara imeyataifisha Madini ya Tanzanite gramu 132.64 yenye  thamani ya shilingi Milioni 18,446,894.14 yaliyokutwa kwa mfanyabiashara wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, kinyume na Sheria. 


Mfanyabiashara huyo  wa madini ya Tanzanite wilayani humo Lucas Liaseki amekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara mbele ya hakimu mkazi Simon Kobelo baada ya kujaribu kutorosha madini ya Tanzanite katika geti la ukaguzi wa madini hayo Mirerani. 


Wakili wa serikali mwandamizi ambaye pia ni mkuu wa mashtaka mkoa wa Manyara Mutalemwa Kishenyi amesema mfanya bishara huyo alikamatwa kwa kosa la kutokuwa na kibali cha ambapo serikali imeyataifisha. 


Aidha amesema mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi 12 na kumuamuru asifanye kosa lolote kwa kipindi hicho.


Share:

7/01/2020

Kimenuka..Kampuni ya Moil Yalipa Faini ya Tsh Milioni 10 Kwa Kuhujumu MafutaMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha na kulipishwa faini ya Tsh. Milioni 10

EWURA imesema kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Olympic Petroleum lipo pale pale baada ya kukaidi maelekezo. Iliamriwa hadi jana saa 11 jioni iwe imesambaza mafuta katika maeneo waliyoelekezwa

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema kutokana na taarifa za uhaba wa mafuta nchini, wamekuwa wakifuatilia hali ya upatikanaji wake kwa kutumia wakaguzi wake na kupata taarifa kutoka kwa Viongozi wa Wilaya au Mikoa
Share:

6/05/2020

Shirika la ndege la Qatar kuanza safari Nchini Tanzania
Shirika la Ndege la Qatar limetangaza kurejesha safari za ndege nchini Tanzania kuanzia Juni 16, baada ya miezi miwili kupita tangu shirika hilo lilipotangaza kusimamisha safari kutokana na janga la COVID-19.

Share:

6/01/2020

PICHA: Muonekano wa Barabara za juu Ubungo, Vyombo vya Usafiri vyaanza KupitaNi Mei 30, 2020 ambapo Barabara za juu (Flyover ) iliyojengwa Ubungo Dar es Salaam  imeanza kufanya kazi ambapo vyombo vy usafiri vimeruhusiwa kupitia, hapa nimekusogezea picha 11 ujionee.
Share:

5/30/2020

Abiria 200 Wasafiri Kutoka Tanzania Kwenda India Kwa Air Tanzania
Hatimaye abiria 200 wakiwemo raia wa India jana usiku wamefanikiwa kusafiri kwa ndege ya Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka hapa nchini kuelekea India kutokana na juhudi za ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya India kupitia Balozi zote mbili ili raia hao waweze kuungana tena na familia zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Lebris Laanyuni amesema kuwa huu ni muendelezo wa jitihada za Serikali kuamua kuwarejesha nyumbani abiria walioshindwa kusafiri kutokana na zuio lililosababishwa na janga la Covid-19 na kwamba hapo awali walifanikiwa kuwarudisha nchini Tanzania abiria 246 waliokwama nchini India.


Share:

5/24/2020

Habari Njema....Ndege ya Kwanza ya Watalii Yatua Uwanja wa Ndege ya KiaWAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema ndege ya kwanza iliyobeba watalii ikitokea Ugiriki imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai jana.

Aidha, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inakamilisha taratibu za kuanza kubeba na kupeleka mizigo Ulaya kwa ajili ya biashara.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamwelwe alisema ndege iliyobeba watu saba wakiwemo watalii wanne kutoka Ugiriki, ilitua KIA jana saa 3:30 asubuhi, ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutangaza kufungua anga lake, lililokuwa limefungwa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Hii ni hatua ya mwanzo ya kurejea kwa usafiri wa anga kwa ndege za kimataifa nchini, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu anga la Tanzania lifungwe.

“Ndege iliyotua ilikuwa na watalii wanne na crew ya watu watatu na wametua tayari wamepokelewa na wameenda kuangalia wanyama,” alieleza Kamwelwe.

Aliongeza kuwa tayari kuna ratiba ya ndege, zitakazofanya safari zake kuja Tanzania na nafasi zimejaa. Alisisitiza kuwa ifikapo Mei, 28 mwaka huu ndege nyingi zaidi zitatua.

“Yapo mashirika ya ndege yalishajiandaa kama Emirates, Ethiopian na KLM. Kwa upande wa ndege za mizigo tulianza na Rwanda Airline kuanza kubeba minofu ya samaki, leo (jana) tumeongeza ndege nyingine Ethiopian Airlines ambayo itabeba tani 19 za minofu ya samaki,” alieleza.

Alisema pia Jumapili hii Ethiopian Airlines, itarudi tena jijini Mwanza kubeba tani 40 ya minofu ya samaki.

“Uwanja wa Mwanza umefunguka na kwa kuwa ni uwanja wa kimataifa, ndege zitaruka kimataifa kwa ajili ya kubeba mizigo na tunaendelea kuongea na Waziri wa Mifugo na Uvuvi ili nyama ianze kusafirishwa,” alisema waziri huyo mwenye dhamana ya Uchukuzi.


Share:

5/19/2020

Serikali Yatangaza Utaratibu Mpya Kwa Watalii “Hawarudi Nyumbani Mwezi Mmoja”Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, ametangaza kufunguliwa kwa anga la Ndege la Tanzania, ambapo kwa sasa Ndege za Kitalii, na kibiashara zitaruhusiwa kuingia nchini.

Aidha ameitaka ATCL kujipanga ili kurejesha huduma za usafiri.

Wakati huohuo akizungumza Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kuanzia sasa watalii wanaruhusiwa kuingia nchini na kupimwa.

Dr. Kigwangalla amesema katika zoezi hilo wahudumu wa Viwanja vya Ndege, pamoja na wahudumu wa  watalii watalazimika kupimwa Corona kila mara pindi wanapoingia Tanzania.

Aidha Waziri Kigwangalla amesema, Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, zitasimamia miongozo maalumu iliyowekwa ikiwamo kufungua anga ili kuruhusu ndege zianze kuingia.
Share:

5/16/2020

Habari Njema Kwa Watanzania..PATO la Taifa Lapanda kwa Asilimia 7


Habari Njema Kwa Watanzania..PATO la Taifa Lapanda kwa Asilimia 7

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema pato la taifa limekuwa kwa asilimia 7 kwa mwaka 2019 sawa na ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kueleza sekta ambazo zinaongoza kwa ukuaji nchini.
Amezitaja sekta zilizoongoza katika ukuaji ni pamoja na uchimbaji wa madini na mawe kwa asilimia 17.7, ujenzi kwa asilimia 14.1, sanaa na burudani asilimia 11.2, usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.7.
Katika hatua nyingine Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai aliikataa hotuba ya bajeti ya fedha na mipango ya kambi ya upinzani kutokana na Waziri Kivuli Mh. Halima Mdee kutokuwepo bungeni wakati baadhi ya wabunge waliokuwa wamejiweka karantini wamerejea bungeni.
Share:

5/13/2020

Wafanyabiashara Simiyu Wakubali Kuuza Sukari 1,900


Wafanyabiashara wa sukari Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, wametangaza kushusha bei ya bidhaa hiyo kutoka Sh 3,200 kwa kilo moja ilivyokuwa ikiuzwa awali, hadi Sh 1,900, ili kutii maagizo ya Serikali.


Sukari

Hatua hiyo imekuja kufuatia kikao cha pamoja, baina ya wafanyabiashara wa sukari wa rejareja na jumla na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, kikicholenga kujadili mstakabari wa bei ya bidhaa hiyo.

Katika kikao hicho, Serikali ilisema kuanzia leo Jumanne, itaanza kuwakamata wafanyabiashara watakaobainika kuuza sukari juu ya Sh 1,900, ambayo ni bei elekezi ya mamlaka, na hii ndiyo kauli za Serikali.
Share:

5/09/2020

Serikali Itumie Mdororo wa Bei ya Mafuta Duniani Kuwekea AkibaKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, imeishauri serikali kutumia vyema mdororo wa bei ya mafuta duniani, ili kupata mafuta kwa masharti nafuu na kuanzisha hifadhi ya mafuta kimkakati kwa ajili ya siku zijazo.

 

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dunstun Kitandula, alisema ni vyema kwa wakati huu serikali ikazungumza na nchi rafiki zinazozalisha mafuta ili kupata mafuta hayo.

 

Alisema katika kutekeleza hilo ni vyema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) liwezeshwe ili kupokea akiba hiyo ya mafuta.

 

Alisema tayari ulimwengu umeanza kushuhudia Sekta za Usafiri wa Anga na Utalii zikisimama, biashara na uzalishaji viwandani kushuka na hivyo kushuka kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mafuta na bei yake kuporomoka.

 

“Kufuatia mkanganyiko huu na mwenendo usiotabirika wa soko la mafuta ulimwenguni, ipo haja kwa nchi yetu kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha wakati wote,” alisema.

 

Kitandula alisema kamati pia ilichambua taarifa kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta nchini na kubaini kuwa, kwa kipindi chote cha Julai 2019 hadi Februari 2020, hali ya upatikanaji wa nishati hiyo ilikuwa nzuri na nchi ilikuwa na akiba ya mafuta ya kutosha kwa wastani wa zaidi ya siku 40 kwa kila aina ya mafuta.

 

“Hii ni ongezeko la asilimia 55 kulinganishwa na siku 15 za akiba ya mafuta zinazotakiwa kwa mujibu wa kanuni,” alibainisha.

 

Alisema mfumo wa BPS (Bulk procurement System) umewezesha kupungua kwa gharama za meli kusubiri kupakua mafuta kutokana na upangaji na usimamizi mzuri wa uletaji meli za mafuta (laycan) ambao umepelekea muda wa meli kusubiri kupungua kutoka wastani wa siku 45 kwa siku za nyuma hadi wastani wa siku tano kwa sasa.

 

“Kamati ilibaini kuwa, kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, gharama za meli kusubiri imepungua kwa asilimia 18.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2018/2019,”alifafanua.

 

Alisema jumla ya lita 4,161,067,814.92 za mafuta ya dizeli, petroli, ndege na taa ziliingizwa kwa matumizi ya ndani ya nchi (local) na nchi za jirani (transit) kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020.

 

Kitandula ambaye ni Mbunge wa Mkinga, alisema katika kiasi hicho cha mafuta, jumla ya lita 2,398,969,342.12 sawa na asilimia 58 kilikuwa kwa ajili ya matumizi ya ndani, na lita 1,762,098,472.80 sawa na asilimia 42 kwa ajili ya nchi za jirani.

 

Vilevile, alisema kamati imeridhishwa na hali ya upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na usimamizi mzuri wa uagizaji wa mafuta unaofanywa na wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) kwa kushirikiana na mamlaka nyingine.
Share:

4/21/2020

Bei ya Mafuta Yashuka....


Bei ya mafuta imeshuka kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana kwa zaidi ya miongo miwili wakati wafanyabiashara wakizidi kuingiwa na wasiwasi kwamba hifadhi zao zinaelekea kufikia kikomo.

Dalili zinazonesha kwamba nchi za Ulaya na Marekani ambazo zimezongwa na janga la virusi vya Corona huenda zimeshindwa kuzisaidia hisa za nchi za Asia kuongeza viwango vyao vya bei za hivi karibuni.

Wachambuzi wanasema hatua ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi huu kati ya wazalishaji wakuu wa mafuta duniani ya kupunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 10 kwa siku imeleta matokeo machache katika mgogoro wa mafuta kutokana na kuwepo hatua za nchi kufunga shughuli za kibiashara pamoja na kusimama kwa safari za ndege, hatua ambazo zimewafanya mabilioni ya watu kubakia majumbani.
Share:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger