BINTI WA MIAKA 8 AOGELEA NA KICHANGA HADI UFUKWENI KUJIOKOA BAADA YA BOTI KUZAMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANAFUNZI wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kipwa mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa mwenye miaka minane ameweza kujiokoa yeye na mtoto wa dada yake mwenye umri wa miezi mitano kwa kuogelea hadi ufukweni baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye ziwa Tanganyika.

Manusura huyo aliyefahamika kwa jina moja la Prisca akiwa miongoni mwa wengine 15 walinusurika kufa maji ama kwa kuogelea au kuokolewa alipoona mtumbwi huo ukizama, inadaiwa alipiga mbizi majini akiwa na mtoto huyo mchanga mgongoni mwake na kuweza kuogelea kwa saa kadhaa hadi ufukweni wote wakiwa hai.

Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kipwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika , Benson Silinjile alithibitisha mkasa huo wa aina yake akisema msichana huyo Prisca alikuwa amempeleka mtoto huyo kupata chanjo katika kituo cha afya kijijini Kapele kwa kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa mgonjwa hivyo alimwomba msaada huo.

Licha ya msichana huyo kuweza kujiokoa yeye na mtoto huyo mchanga kwa kuogelea hadi ufukweni pia nahodha wa mtumbwi huo uliopata ajali hiyo iliyosababisa vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake na watoto wenye umri chini ya miaka mitano , Lazaro Sikapote (26) aliweza kuokoa familia yake akiwemo mama yake mzazi Rose Sikapote , mkewe Rakadia Sikazwe na mwanae aliyefahamika kama Nazaro Sikapote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii FUTUHI sasa, watu kumi na tatu wafe kenyee ndo kajiokoe na KICHANGA mgongoni wakiogelea zaidi ya masaa..!!!?????
    Haijaniingia akilini bado njoo kwa staili nyingine.

    ReplyDelete
  2. Sio kosa lako ni kutokuwa na roho ya iman na uelewa wako pia mdogo maana,inawezekana sana kwan hukuona yule mtt kwenye ajal ya mel ya nungwi alivyookolewa anaelea majin huku yeye kalala?

    ReplyDelete
  3. Acha ushamba ni kujua tu kuswim at young age ingia YouTube search water babies utakoma na roho yako uone vitoto vidogo vya miezi kadhaa hadi miaka 2 vinavyojua kupiga mbizi na vinageuka kuvuta pumzi halafu vinaendelea utajibeba Kama hujui kuogelea utakufa maji

    ReplyDelete
  4. mipango ya mungu. kufa kwa wale ickupoteze iman. yakufaa umpongeze kwa ujacli alio nao mtto huyo.

    ReplyDelete
  5. Jaman achen kudanganyana mtoto wa miaka 8 hawez kuogelea kwa zaid ya saa huku akiwa na mtoto mwingine!!

    ReplyDelete
  6. Tatizo Wabongo swimming 0 watoto good swimmer kuliko kujifunza ukubwani.

    ReplyDelete
  7. INAWEZEKANA KABISA HUYO MTOTO AKOGELEA NA KUJIOKOA NI MAZINGIRA ALIYYAZOEA.MBNA KUNA WATOTO WA MIAKA KAMA HIYO ANAISH MBAGALA HALAFU ANAENDA KUSOMA TEGETA?

    ReplyDelete
  8. KWA NINI HUYO MTOTO ASIANDALIWE ILI MWAKA 2020 AKASHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI KULE JAPAN???????????????????????????????????????????????????????ANAWEZA AKAVUNJA REKODI YA DUNIAI. Wewe unayesoma hii comenti hata ukiwekwa kwenye Beseni utakufa.

    ReplyDelete

Top Post Ad