IMEGUNDULIKA MISSION YA AL SHABAAB NI KUUWA WAKENYA NA WAMAREKANI TU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtandao wa Mail Online wa Uingereza umeripoti kuwa mwanamke mmoja miongoni mwa waliofanikiwa kuachiwa na magaidi wa Al-Shabaab kutoka katika mall ya Westgate iliyoko Nairobi iliyotekwa toka jana, amesema kuwa magaidi hao walimwambia lengo lao ni kuwauwa Wakenya na Wamarekani.

Mwanamke huyo raia wa Ufaransa aliyejitambulisha kwa jina moja la Pauline amesema alifanikiwa kujiokoa kutoka katika mall ya Westgate akiwa na watoto wake wawili wadogo ambao walipewa Chocolate na magaidi hao.

Habari hiyo inaendelea kusema mama huyo wa watoto wawili, ambaye alikuwa katika mall ya Westgate wakati mashambulizi hayo yanaanza, alisema baada ya kuwaambia magaidi hao kuwa ‘Waislamu sio watu wabaya’, magaidi waliwapatia Chocolate watoto wake wawili Emily (6), na Eliot (4).

Pauline amedai kuwa aliombwa msamamaha na magaidi hao waliomwambia kuwa wao sio monsters “we are not monsters”.


Aliongeza kuwa magaidi hao wenye silaha walimwambia kuwa wanahitaji kuwauwa wakenya na wamarekani pekee na wakamwambia abadilishe dini awe Muislam kisha wakamuomba msamaha mwanamke huyo “do you forgive us? do you forgive us?’.

Mwanamke huyo amesema alifanikiwa kujiokoa na watoto wengine wawili, akiwemo mvulana wa miaka 12 ambaye mama yake aliuwawa katika mashambulizi hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jaman inatishaa kama muv ujue hawa watu wana laana jaman Mungu awasaidie

    ReplyDelete
  2. inatisha na inasikitisha jamani...hawa watoto hawasahau hili tukio maishani mwao. Hebu angalia pembeni maiti ile jamani...oooh Mungu tusaidie jamani wabadilishe hao magaidi mioyo yao

    ReplyDelete

Top Post Ad