TAFSIRI YA KISWAILI YA MAHOJIANO YA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA UVAMIZI NA MAUAJI YA WATU KENYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.

JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?

Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu. Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.

JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo. Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.

JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
 Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.

JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?

Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.

JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?

Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.

JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?

Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.

JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
 Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.

JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?

Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.

JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia. Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya ngoja tuone pozi za wakenya itakuwaje hapo, all shabaabu watawakamua mavi mpaka wakome, nawachukia sana watu hawa most of them wanadharau sana na maringo na wanatutukana sana watz bila saabu yeyote, kwao wenyewe njaa tupu, vita, udini, ukabila mpaka wana hotels na bar za kikabila bt hawaishi kututkana bana kisa eti hatujui kiingereza! i cant imagine how stupid a black man can be kuringia lugha ya mzungu khaaaaa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mbaya kushangilia mwenzako akipata tatizo ila una point kabisa wanatudharau mnoooo

      Delete
    2. Pole kwa yaliyowafika ila sure jirani zetu wanatudharau sn!hasa kipindi kile tunapita njia yao Mwanza-Dar lol.!! Tulipata shidaaaa!!! Mmmmh

      Delete
    3. Nashangaa dada zetu kuwashobokea wakenya, amini msiamini mtajutia hilo cku moja, majuzi hapa tz ilitanga kuiunga mkono kenyajuu ya kushtakiwa viongozi wake mahakama ya kimataifa, imagine jambo jema kama lile bt duuuuh walitutukana hao, eti ooooh mlikuwa wapi cku zote hamkututetea, mara oooh mtaongea nn the hague na lugha hamjui, mara oooh mmesoma na kuelewa vipi mambo hayo na yanaandikwa kiingereza, matusi, matusi mpaka basi. sasa hilo lilikuwa jambo jema kabisa tukatukanwa, sasa c ajabu hata hili ukiwapa pole watakutukana zaidi kwamba hatuna hata Mall tunajua nn habari ya mall, labda hatuna hata jeshi na c ajabu watakwambia kiingereza hujui utaongeaje na wao . Jamani kwa kifupi mi nimeishi kenya mombasa nafanya kazi miaka miwili hivi na nilitembea sehemu mbali mbali i know them very well, hao watu ni majanga, wachache sana wenye utu, watu husema tembea uone na kama hujatembea nakuambia hivi ringa sana kuzaliwa tz unabahati sana na mshukuru Mungu, linda amani iliopo, kwa wenzetu ni shida, vita na mauaji kila cku vile hawapendani, ni ukabila tu. mauji kenya yapo kila cku ila hili linaonekana kubwa kwa vile limetokea mjini na wageni wameuawa ndio maana.

      Delete
  2. Na huyo msemaji wa magaid anasema mungu akipenda!!!! Hakuna mungu anaempenda mtu anaeua watu,huyo amwombe shetan

    ReplyDelete
  3. Wakenya wamezidi kujifa wao wanajua kila kitu asa ilo limewakuta siwaombei mabaya bt kwa ili mtakoma...ndo muache jeuri,ao wanajua lugha zote watawakomesha kumamake

    ReplyDelete
  4. Ndugu zangu,tuwe na huruma kwa wenzetu.Watoto wameuwawa ama kujeruhiwa viumbe wasiokuwa na hatia,wamezaliwa majuzi hawajui lolote.Najua sehemu yeyote ile kuna wabaya na tunatofautiana.Waombeeni mema waweze kupona na mengine tumuachie Mungu maanake yeye ndiye muweza yote.Usishangae huenda wanaowakwaza wale mnapoenda kule utakuta hata ni wa nchi nyingine na sio wakenya.

    VM
    Tanzania

    ReplyDelete
  5. hebu kuwa na ubinadam na wale watoto pia walikutukana?? binadamu tupendane haijalishi kama kenya wanazarau but kwa hili binadam wote tuungane coz ni tukio la kinyama sana

    ReplyDelete
  6. Mi nawapa pole. Kiburi, jeuri , maringo , ubaguzi ni wao. Karibuni Tanzania!

    ReplyDelete
  7. hizi ni fitina tu hazina faida ila kumwaga damu na uislam unatilia nguvu kuhami watu na kwa hali uoyote hakuna ruhusa ya kuua watu wasio na hatia

    ReplyDelete

Top Post Ad