TANZANIA, CONGO NA BURUNDI WAUNDA MUUNGANO WAO BAADA YA KUTENGENGWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.
  
Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.

Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.
Mkutano wa ujirani mwema
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.
Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.
Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC,” alisema Sitta.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.
Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo,” alisema Sitta.
Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.
Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwel achana nao!

    ReplyDelete
  2. Kuwa kwenye jumuiya hakumaanishi kusiwe na health competition wanachofanya Kenya ni kuipa bandari ya Mombasa cost advantage kuliko competitor wake yaanai port of dsm inabidi miundo mbinu ya rail iwe ya kisasa kama walovyofanya jirani jana kuwa na standard gauge ili time taken from the port iwe reduced by almost 70 pct kama hilo halitafanyika hata hao drc in the future watatumia mombasa this is a waking call to our decision maker lets them be more aggressive and make wise and focused decisions kuliko kibaki kulalama na kureact

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau Mbona unachanganya ligha!

      Delete

Top Post Ad