MARAIS MUSEVENI NA KENYATTA WAISHANGAA TANZANIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ametetea mazungumzo ya kile kinachoitwa ushirika wa hiari unaohusisha nchi tatu za Uganda, Rwanda na Kenya, huku akiishangaa Tanzania kuhusu madai yake ya kutengwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Museveni alidhihirisha mshangao wake huo jana mjini hapa, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo yaliyowahusisha Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Katika kikao hicho, Museveni alidai majadiliano hayo ni sahihi kwa kuwa nchi hizo zinachojadili ni miradi ya miundombinu kwa ajili ya ukanda wa kaskazini.

Museveni alidai Tanzania itahusishwa wakati majadiliano yatakapohamia ukanda wa kusini, ambako ndiko lilipo taifa hilo lenye eneo kubwa zaidi miongoni mwa wanachama wa EAC.

Kauli kama ya Museveni pia ilitolewa na Rais Kenyatta wakati akizungumza na Wakenya waishio nchini Rwanda, akipuuza hofu iliyojengeka kuwa jumuiya hiyo inaelekea kuvunjika.

Rais Kenyatta alisema utekelezaji wa miundombinu ya kimaendeleo unaohusisha nchi hizo pamoja na Sudani Kusini, hauhujumu mtangamano wa jumuiya hiyo.

“Tumedhamiria katika malengo yetu ya mtangamano wa eneo hili na kulifanya listawi. Kwa sasa tunatarajia kaka na dada zetu wa Sudan Kusini kuungana nasi muda si mrefu na kuifanya EAC istawi na kuwa na nguvu zaidi,” alisema.

Aliendelea kueleza kwamba, tofauti na kinachoelezwa na ‘maadui’ wa mtangamano wa EAC, wanachama wote wa jumuiya hiyo bado wamedhamiria kuungana.

“Kutokana na wasiwasi wa majirani zetu, niliamua kuchukua hatua zilizofanikisha kupunguza siku za kusafirisha bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kigali kutoka siku 22 hadi nane,” alisema.

Aidha alisema Serikali yake imeondoa vikwazo vyote vya usafirishaji mizigo na anatarajia mizigo itasafirishwa kwa kasi na urahisi zaidi katika nchi zote jirani.

Hata hivyo, viongozi hao walikwepa kuzungumzia suala nyeti zaidi ambalo nchi hizo katika mikutano miwili ya nyuma ziligawana majukumu ikiwamo kushughulikia suala la katiba ya shirikisho la kisiasa, viza moja, ushuru wa forodha na mengineyo ambayo yamo ndani ya mipango ya EAC.

Hivi karibuni, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alieleza msimamo wa Serikali ya Tanzania kutokana na kitendo cha nchi hizo kujiundia utatu wa hiari ndani ya EAC.

Akijibu moja ya maswali ya wabunge mjini Dodoma hivi karibuni kuhusu mwelekeo huo unaotishia mustakabali wa jumuiya hiyo, Sitta alisema Serikali imeamua kutohudhuria mikutano yenye ajenda ambazo nchi hizo tatu zimeshaweka msimamo wa peke yao. 

Sitta ambaye awali aliwahi kuonya kwamba kinachofanywa na nchi hizo ni kinyume na makubaliano na mkataba wa EAC, alienda mbali akisema Serikali imeshaanza mazungumzo na Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ili kuanzisha ushirikiano wao.

Aidha alifafanua kauli ya hivi karibuni ya waziri mwenzake wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwamba Tanzania inasubiri talaka, akisema yenyewe ndiyo yenye uwezo wa kutoa talaka kwa jumuiya hiyo kwa kuwa inamiliki asilimia 52 ya eneo lote, huku nchi zilizobakia zikigawana asilimia 48 iliyobakia.

“Hawa wenzetu wanafanya utoto wa kutuzunguka, sisi tunatumia hekima ya Mzee Mwinyi aliyesema ‘mwongo, mwongoze.’ Kama wao wana hila zozote juu yetu, siku si nyingi tutazibaini, kama ni ndoa ya kwenye jumuiya basi sisi ndiyo tutakuwa tumeoa. Hivyo tutatoa talaka sisi,” alisema.

Hata hivyo, Rais Museveni alipoulizwa na mmoja wa wanahabari wakati wa mkutano wake mjini Kigali, alidai kuwa hana taarifa ya malalamiko yanayotolewa na Tanzania kuhusu utatu wa nchi zao.

“Hadi nitakapopata barua rasmi kutoka Serikali ya Tanzania ndipo nitakapoamini, vinginevyo nahesabu kile ninachoshuhudia katika vyombo vya habari ni uongo,” alisema.

Hata hivyo, wanadiplomasia wa Tanzania wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kuhusu kuachwa katika mipango ya jumuiya hiyo, wakisema haikualikwa kushiriki na wanatarajia kulifikisha suala hilo katika kikao cha wakuu wa EAC kitakachofanyika mjini Kampala, Uganda mwishoni mwa Novemba mwaka huu.
-Mtanzania
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna tatizo kubwa kwa sisi wabongo hasa kwenye decision and management ukiangalia ktk kila partnership tuliyofanua haziendi vizuri mfano mzuri ni Tazara hata huko sadc tunapojivunia ni majanga matupu tujiulize kwa nini ni sisi kila wakati sidhani kweli watu wanatuonea wivu viongozi wetu wana mapungufu makubwa na wanataka kutumia ufinyu wetu wa masuala ya integration kuficha udhaifu wao. Viongozi wengi wanaomshauri Raisi uwezo wao ni mdogo sana ukilinganishwa na wenzetu na ni wakato umefika sasa tukubaliane kwamba hata kama tuko kwenye economic blocks lakini hii haiondoi ushindani wa haki ni vizuri watanzania wakalielewa hilo kwamba Dsm port na mombasa siku zote zitakiwa ktk ushindani tujipange tutumie vizuri nafasi yetu strategically kunufaika kuliko kila kukicha kubaki tunalalama usiku na mchana

    ReplyDelete
  2. Wala sio swala la kulalamika mdau wa kwanza, wanasema kwamba hawajatujumuisha sababu wanashughulikia miundo mbinu ya north, mbona burundi hawaijumuishi saa hizi, hawa marais watatu tabia zao ni moja ni wanafiki wakubwa wala usiwatete nothing wrong with tz ktk hili.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili upo sahihi sana maana hawa marais watatu ni nyoka kabisa,watuache tulale sie

    ReplyDelete
  4. Madu wa kwanza bado upo gizan. Toboa ki2ndu upate mwanga bado jua linawaka

    ReplyDelete
  5. hawa jamaa pumbavu walihic tutaingia kichwakichwa coz taget yao ilikuwa ardhi sasa wameoba tunakomaa wmeanza unfiki wao! tujitoe thn tuone watakavyopigika coz idadiya raia wao ealio katika nchi yetu ni wengi ukilinganisha na wetu, hata liuchumi na kisiasa tuna mchanho mkubwa sana kwao wajinga hawa! watuache tulale na nyumbani kwetu tz!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa kwanza atakuwa Myarandwa mwenye asili ya Uganda na akamia Kenya

    ReplyDelete
  7. huyu mzee ndo maana aavaaga kofia mm sijawhi muona kavua kofia ndo leo mwe

    ReplyDelete
  8. Watanzania wenzangu nafikiri tuache kuchukulia mambo juu juu hapa kuna tatizo, pande zote zina matatizo na zaidi ni sisi. Hakuna ndo ya zaidi ya mke mmoja iliyo na AMANI zaidi ni UNAFIKI tu. Sie tuko EAC na sie haohao tuko SADC na kote huko kuna masharti amaboyo inabidi tuyafuate baadhi ya masharti hayo yanakinzana yaani ya EAC/SADC viongozi wetu wamekwama hawajui wafuate yepi. Kwa msingi huo SADC hatuko EAC hatuko na tusipojiangalia tutakosa kote. Tukae chini tujifikirie na tuamua wapi tuna manufaa nako zaidi na tushike huko.

    ReplyDelete
  9. Pia ndugu zangu tuonyeshe ustaarabu wetu wa Kitanzania wakati wa kutoa maoni matusi hayatusaidii chochote HAO wazee licha ya kuwa ni viongozi kiumri ni kama wazazi kama sio kaka zetu. Tutoe maoni ambayo hata kama wakibahatika kuyasoma (NAJUA WANASOMA HATA KAMA SIO WAO MOJA KWA MOJA) waone kuwa tuna nia gani juu ya jumuia na umoja wa wana EAST AFRICA. Tukumbuke sie sote ni ndugu hizi siasa zisitufanye kuwa maadui. HAMJUI TATIZO LA JK na PK ni nini au matatizo ya JK UTATU wa PK/UK/YKM (M7) Ni nini hayo tuwachie wenyewe sie wananchi tujadili yale yalio ya manufaa kwetu hawa viongozi muda wao ukifika wataondoka madarakani sie tutabaki kuwa wananchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad