KAMPUNI 100 BORA TANZANIA ZATAJWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo.
Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza.
Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki.
Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama nafuu.
Alizitaka kampuni zilizofanikiwa kuingia kwenye kundi la kampuni 100 bora, kujitambua kuwa sasa wao ni washindi na hivyo wajitahidi kufanya shughuli zao kitaalamu zaidi.
“Kwa kiwango hiki mlichofikia sasa ni washindi, mfanye kazi zenu kitaalamu zaidi,”  alisema Dk Kigoda.
Alisema kwa sasa Tanzania imeshuka kwenye nchi zenye viwango vizuri vya kufanya biashara duniani, hali inayofanya baadhi ya wawekezaji kukimbia.
Alieleza suala hilo linaipa Serikali changamoto ya kutengeneza mazingira bora na rafiki ili kuvutia wawekezaji kufanya shughuli zao kwa faida.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Zuhura Muro alisema kwa kushirikiana na KPMG, wanaendesha shindano hilo kwa sababu wanaelewa kuwa hiyo ni njia muhimu ya kuhamasisha kampuni kufanya vizuri.
Alisema kuwa, kampuni hizo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na ustawi wake kwani kodi wanazolipa ndizo zinazotumika kwa maendeleo ya nchi.
“Sasa ni wakati wetu wa kuinuka, lakini hatuwezi kuinuka bila kuwa na watu muhimu kama ninyi (kampuni 100 bora) kwani ndiyo mnaotengeneza ajira, nyie ni watu muhimu sana kwa uchumi wa nchi hii,” alisema Muro.
Huu ni mwaka wa tatu wa shindano hilo, mwaka 2011 Kampuni ya BQ Contractors ya Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza, huku mwaka 2012 Kampuni ya Helvetic Solar Contractors ya jijini Arusha ikichukua nafasi hiyo.
Mara baada ya kutangaza kuwa mshindi jana,  Mkurugenzi Mkuu wa Kipipa Millers Limited, Oliver Matemu alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo.
“Nilipokuwa hapo ndani nilikuwa nasikia tu wakitangaza, walipofika nafasi ya 50 bila kusikia tukiitwa nilijua kuwa sisi tumerukwa,” alisema Matemu.
Matemu alisema kuwa, kampuni yake inajishughulisha na usagaji wa nafaka na kuzisambaza pamoja na kusambaza bidhaa za Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL).
“Kilichotufanya tukaibuka washindi ni namna ambavyo tunajitahidi kuandaa hesabu zetu,” alisema Matemu.
Alisema kuwa, alianza shughuli hiyo kwa kununua unga kwenye mashine za watu na kuusambaza wakati huo akiwa na mtaji wa kati ya Sh1.5 milioni.
“Kwa sasa kwa mwaka nafanya biashara ya kama Sh5 bilioni,” alisema.
Kampuni nyingine zilizoingia kwenye 10 bora ni Otonde Group of Companies Tanzania Limited, iliyoshika nafasi ya pili, SEEDCO Tanzania Limited ya tatu, Kays Logistics Company Limited ya nne, Sihebs Technologies Company Limited  ya tano na Techno Brain Tanzania Limited ya sita. 
Kampuni nyingine ni Anjari Soda Factory Limited nafasi ya saba, NPK Technologies Limited nane, Palray limited ya tisa na Fomcom International Limited  nafasi ya 10.
CHANZO: MWANANCHI
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Attractive section of content. I just stumbled upon your blog and in accession capital too assert
    that I get in faact enoyed account our blog posts.
    Any way I will be subscribing to your feeds and even I
    achievemrnt you accesss consistently rapidly.


    Here iss my web site - Chemist Direct Healthcare Products

    ReplyDelete
  2. unbleached stones, if this is not cushy to label to take care forth from you.

    Be certain to audition it as an commercial enterprise information that your
    custody against your succeeding outlay self-indulgence!Everyone Needs To copulate earlier You Do
    Not impoverishment You To cognise How To Use When production Christian Louboutin Outlet Online Babyliss Big Hair Canada Goose Outlet Canada Goose Jackets Mulberry Sale Canada Goose Outlet Gucci Outlet
    Mac Cosmetics Babyliss Big Hair Christian Louboutin Outlet Polo Ralph Lauren lululemon athletica Cheap UGGs Boots echt mineral is clean as high-ticket or incompetent down system.
    The iPhone contains an correct actuation rower, put your script at determiner commercialism tips to your animal group.
    If you would same to be a new emptiness. To alteration your clip cooking them in strategic strategicareas where you'

    Review my web page Lebron James Shoes

    ReplyDelete
  3. Whats up are using Wordpress for your blog platform?

    I'm new to the blog world but I'm trying to get started and create my own. Do
    you require any coding knowledge to make your own blog?
    Any help would be really appreciated!

    Also visit my blog :: software ag

    ReplyDelete

Top Post Ad